Napata Ukakasi wa Kumuita Magufuli kwa kibwagizo cha SHUJAA alipatwa na Umauti Kizembe sana

Napata Ukakasi wa Kumuita Magufuli kwa kibwagizo cha SHUJAA alipatwa na Umauti Kizembe sana

Mungu alitupa uwezo thabiti wa kufikiria, kujidhatiti, kuchukua tahadhari, kujilinda na mambo kadha wa kadha. Adui hasamehewi kirahisi na usimpe fursa ya ukaribu, ukizubaa anakumoa bila huruma.

Ushujaa ni neno zito sana na linahitaji kutumika kwa wapigania uhuru na mwenye harakati za kujikomboa,

Sioni mantiki ya Magufuli kuitea SHUJAA kwa lipi hasa wakati alikufa katika mazingira ya kizembe sana.

Tuache kuwapa watu majina ambayo hawana sifa nayo, Magufuli haikuwa na ushujaa wowote labda mtumie neno jasiri ama mbabe nje na hapo msichafue kamusi ya tafsiri ya neno SHUJAA.

Tupambane kwa hoja na sio vinginevyo, ukija kwa hoja nakubatua kwa hoja ukija kwa vijembe ntakupa nginja nginja kama zote.

"Mwewe mwenda kasi halali njaa"

Wadiz

Chief Wadiz a.k.a Chief Mapenzi
Umesema ukweli kabisa mwamba! Wewe unajielewa sana! Eti shujaa? Mshamba sana yule!
 
Back
Top Bottom