Napata Wasiwasi Sana Na Uelekeo Wa "DiamondPlatnumz"

Napata Wasiwasi Sana Na Uelekeo Wa "DiamondPlatnumz"

Diamond anawaza mbali sana... Anajua Marry you bado inasumbua sana nchi za nje, hivyo hizi nyimbo ametoa kupunguza kiu ya mashabiki tu, ila naamini kuna kitu kikubwa anaandaa ila muda wake bado... by the way nyimbo nzuri!
Ni kweli mkuu, marry me inasumbua sana nchi za nje, juzi nilikua korea kaskazini kwa kiduku wimbo wa marry me unapigwa sana kwenye club za mjini pyongyang.Top ten za moscow inashika namba 6, Somalia ndio kama wimbo wa taifa wa Alshabab, Gaza ndio wimbo wa kuitia kwenye sim ya Mahamud Abbas, Italy ndio usiseme kila wiki unashika namba 2 kwenye top ten yao. Wimbo bado unafanya vizuri.

Tembelea maeneo ya Mosul, Raqa, Islamabad kote huko unatamba. Diamond sio wa nchi hii.
 
Maneno kama haya watu walisema sana kwenye kidogo ikaja marry you Jamaa anazidi kuchanja mbuga tu!
 
kabisa mkuu,Natamani wasanii wetu wangekua kama wenzetu,tungekua mbali sana
Hawafugiki....wakiota mkia tu haoooo, hata kabla mabawa hayajatoka.

clouds inawasakanya huko majalalani, wakitolewa kutu tu kabla hata hawajapakwa rangi tayali wameota mapembe mhxxxx. .....!!
 
Ni kweli mkuu, marry me inasumbua sana nchi za nje, juzi nilikua korea kaskazini kwa kiduku wimbo wa marry me unapigwa sana kwenye club za mjini pyongyang.Top ten za moscow inashika namba 6, Somalia ndio kama wimbo wa taifa wa Alshabab, Gaza ndio wimbo wa kuitia kwenye sim ya Mahamud Abbas, Italy ndio usiseme kila wiki unashika namba 2 kwenye top ten yao. Wimbo bado unafanya vizuri.

Tembelea maeneo ya Mosul, Raqa, Islamabad kote huko unatamba. Diamond sio wa nchi hii.
Kote huko ulikua unazunguka na ungo na kutua sehemu zenye mziki?
 
Ingawaje kwenye huu uzi tayari kuna wenye roho za kishetani ambao wao wapo standby kusubiri waone mtu anadondoka, concern ya Traveller X nimeielewa sana!!! Naamini hana nia mbaya...

Hata hivyo Traveller X nina wasiwasi hujalifahamu vizuri soko la muziki wa Tanzania na Afrika kwa ujumla! In short, ukitaka kubaki kwenye game kwenye eneo fulani ni lazima uwe umekita mizizi yako eneo husika! Tanzania hakuna msanii hata mmoja ambae ameshakita mizizi yake Afrika!!

Diamond ame-hit Afrika lakini bado hajakita mizizi yake!! Sehemu pekee ambayo majority watakaa standby kusubiri ngoma mpya ya Diamond hata akikaa miaka 3 kimya ni East Africa peke yake kwa sababu tayari amekita mizizi yake eneo hilo!

Kwahiyo itakuwa kosa sana eti kuachana jumla na collabo za Afrika wakati bado anatakiwa kuendelea kujizaititi zaidi Afrika na hatimae kukita mizizi yake!!!

Ku-hit kwa Diamond Afrika hakuna tofauti yoyote na ku-hit kwa Darasa Tanzania!! Bado Darasa hajakita mizizi yake Tanzania na kwahiyo, akipotea kidogo tu, watu wanamsahau jumla!!! Same to Diamond, akipotea kidogo tu kwenye muziki wa Afrika, watu nje ya Afrika Mashariki watamsahau jumla unless kama ana uhakika hizo collabo za US zita-hit US na hatimae kuiambukiza Afrika!!

Asikudanganye mtu... si kazi ndogo ku-hit USA! Lile zari za WizKid halitokei mara mbili! Ndo vile tu alipata zari la yeye kushirikishwa na mtu aliye hot USA! Kuna tofauti kubwa sana kati ya kumshirikisha mwanamuziki wa USA na kushirikishwa na mwanamuziki wa USA!
 
MKUU YEYE KAMA YEYE NI VIGUMU KUPAMBANA NA WANIGERIA.INAHITAJIKA NGUVU YA PAMOJA.WASANII WA NIGERIA WANA PEANA SUPPORT SANA.BIFU NI NJE YA KAZI.DIAMOND KAONESHA NJIA BADALA YAKE WATU WENGI WANAMWONA ADUI.HUU NI UNAFIKI SANA.
MTU KAMA TECNO NI PRODUCER MKALI SANA NA NI MSANII MZURI.TECNO ANAMTENGENEZEA NGOMA DAVIDO NA WAKATI HUO HUO TECNO ANASUKIWA NGOMA NA SELEBOBO.HII NI KUONESHA WANAVYOPEANA SUPPORT.
wivu wa maendeleo,majungu na kutokuthamini vya kwetu ni chanzo cha muziki wetu kudumaa miaka ya karibuni.
 
Ila kusema ukweli ukisikiliza ngoma kama IF na FALL za Davido, ukaja kusikiliza na hizi za wasanii wetu, utagundua kuwa jamaa wametuacha mbali sana.
Halafu kuna mjinga anamlinganisha Davido na diamond kweli? Niache mziki mzuri nikomae na nyimbo mbaya kisa eti uzalendo? WTF nipo zangu club nashangaa zinapigwa nyimbo za Davido tena za juzi hapa na watu wanazielewa utadhani nipo Nigeria, wasanii waache kiki wapige kaziiiiiiii! Tunataka mziki mzuri tutasapoti la sivyo wasitupangie
 
Wimbo wake mzuri wa mwisho ulikuwa ni Mawazo. Baada ya hapo ni drama tu.

Ila cha muhimu ni pesa na anazipata. Kuimba sana kama kina Gurumo (R.I.P.) na mfukoni hauna kitu haina maana.
Kiukweli kwa ukimya alokaa nao mda wote tulitarajia aachie bonge la hit ila badala yake katoa boko..!
 
Back
Top Bottom