Napataje mawazo mazuri ya kuanzisha biashara? Kufikiria mwenyewe haitoshi kunipa wazo sahihi kwa asilimia 100.

Nimefanya kidogo biashara ya nafaka,kitu cha kuzingatiaa ni wapi unachukulia mzigo na wapi solo lako na je faida yake ni asilimia ngapi? Usidhani kila nafaka ukiitoa kijijini utanunua Kwa bei ya chini na ukiileta mjini utaiuza bei ya juu na kupata faida,bei ya mazao shambani na sokoni usipokuwa makini unaweza dhani ni kubwa,mfano unaweza kuta mchele unauzwa kamsamba Kwa 2000 ukileta Dar unauza Kwa 2800 sasa faida ya 800 Kwa kilo sio ndogo inategemea Una kilo ngapi,zingatia hicho kitu pia ubora WA bidhaa yako! Ukiweza Kwa hiyo 1.5 kununua mpunga Kwa wakulima Kwa bei ya chini then ukobowe ulete sokoni Ila zingatia tofauti ya bei uliponunulia na bei gani utaenda kuuza sokoni,na je soko lipo kweli ni uhakika? Nimesha wahi nunua mahindi singida vijinini Kwa 45000 gunia alafu mpaka siku naleta sokoni nakuta bei imeshuka watu wananunua Kwa 43000, hasa Dar,usilete bidhaa mpaka umejua soko la uhakika,mchele unaweza kuwa adimu huko shamba ukahisi Kwa kuwa umeadimika huku shamba Basi Dar au sokoni ukadhani huku ndio hamna kabisa,kumbuka Dar kuna mchele WA kutoka kila sehem Tanzania ila kamsamba hamna mchele unaoingia toka nje ya kamsamba zaidi ya kamsamba yenyewe! Fanya tafiti vizuri,cheza na namba vizuri utafanikiwa! Huwa nasikia pia mchele Zanzibar unalipa japo sina hakika! Kwa huo mtaji Anza na zao Moja Kwanza
Nimekuelewa ndugu*
 
Biashara zetu nyingi zinakufa kwa sababu tunakuwa hatuna ''business plan'' ambayo ingeelezea namna ya kushughulika na changamoto mbali mbali, wengi tunaanzisha biashara kwa kuigana tu, leo mimi nimefungua na wewe kesho umetamani umefungua.
Ni sawa, lakini kuna muda maisha hayana formula. Kuna waliofungua biashara kwa kuigana na wametusua. Kikubwa ni consistency ktk kusimamia unachokiamini hata dunia nzima ikikupinga, utakapofanikiwa utaona kila mtu anajifanya alikuwa anakupa ushauri mzuri sana.
 
Biashara tunazo zifungua tunatakiwa tuzipe miaka 20 mbele, kwamba zinatakiwa zitupeleke wapi, na kufanikisha hili itakulazimu kuwa 'business plan'​
 
Kumradhi Ndugu yangu.

Nawaza kuanzisha biashara ila sijafikia muafaka mawazo yangu.

Sijazaliwa kwenye familia yenye umaridadi sana na biashara, ila hii haimanishi kwamba siwezi kufanya biashara.

Naamini naweza kuwa Maridadi sana kwenye Biashara.

Nahitaji data na mawazo Yako, Ndugu yangu, nahitaji kujua Kutoka kwako, kama Kuna engo ya biashara unauzoefu nayo au Kuna biashara unaielewa vizuri, naomba nishirikishe mawazo Yako.

Mimi nahitaji nipate pakuanzia mawazo yangu, kama nilivyotangulia kusema Sina Msingi mzuri wa mawazo ya biashara.

Nahitaji Msaada wako Ndugu yangu, Rafiki yangu, MwanaJamiiForum Mwenzangu
Biashara ya ajabu sana
Unaweza kuwa expert kabisa na ukala za uso vile vile

🤗🤗🤗
 
Kumradhi Ndugu yangu.

Nawaza kuanzisha biashara ila sijafikia muafaka mawazo yangu.

Sijazaliwa kwenye familia yenye umaridadi sana na biashara, ila hii haimanishi kwamba siwezi kufanya biashara.

Naamini naweza kuwa Maridadi sana kwenye Biashara.

Nahitaji data na mawazo Yako, Ndugu yangu, nahitaji kujua Kutoka kwako, kama Kuna engo ya biashara unauzoefu nayo au Kuna biashara unaielewa vizuri, naomba nishirikishe mawazo Yako.

Mimi nahitaji nipate pakuanzia mawazo yangu, kama nilivyotangulia kusema Sina Msingi mzuri wa mawazo ya biashara.

Nahitaji Msaada wako Ndugu yangu, Rafiki yangu, MwanaJamiiForum Mwenzangu
Ukiingia vitani tegemea kushinda una 1.5M wenzako wanatafuta 100K or 50K waanze na mkaa biashara yoyote ni wewe mwenyewe jinsi gani ulivojipanga na kupambana zaidi usifanye kitu kwa kuiga angalia wapi UNANUA NA UNAUZA WAPIIIII.
 
Ulikuwa unatamani ufanye biashara gani, na unategemea kuanza na mtaji kiasi gani?
Swali zuri lakini nijuavyo mimi mtaji siyo lazima kitu cha msingi ni wazo la biashara ambalo atalifanyia utafiti na hatimaye kuliandikia mpango wa biashara

Unaweza kuanza biashara kwa mtaji kidogo sana ikibidi, hakika bila mtaji, hahaaa wengi watasema nimechanganyikiwa,

unaweza ukawa na mtaji lakini bila mpango wa biashara pesa yote uliyo nayo itaishia kwenye matatizo ya uanzishaji biashara,
 
Hii Falsafa.🥱
 
Zamani nlikua nikisoma hii kwamba mtaji sio jambo la kwanza nlikua sielewi afu naona kama jamaa wanatuona sie watoto 😹 sa utaanza biashara bila mtaji.

Siku za karibuni nlienda kutafuta frem mahali mfukoni nna buku tu ya maji hata hela ya dalali sikua nayo....

Naamini mtaji unakuja baadae baada ya kuwa na wazo la biashara na utayari wa kuifanya.
 
Back
Top Bottom