Napataje mawazo mazuri ya kuanzisha biashara? Kufikiria mwenyewe haitoshi kunipa wazo sahihi kwa asilimia 100.

Nimekuelewa ndugu*
 
Biashara zetu nyingi zinakufa kwa sababu tunakuwa hatuna ''business plan'' ambayo ingeelezea namna ya kushughulika na changamoto mbali mbali, wengi tunaanzisha biashara kwa kuigana tu, leo mimi nimefungua na wewe kesho umetamani umefungua.
Ni sawa, lakini kuna muda maisha hayana formula. Kuna waliofungua biashara kwa kuigana na wametusua. Kikubwa ni consistency ktk kusimamia unachokiamini hata dunia nzima ikikupinga, utakapofanikiwa utaona kila mtu anajifanya alikuwa anakupa ushauri mzuri sana.
 
Biashara tunazo zifungua tunatakiwa tuzipe miaka 20 mbele, kwamba zinatakiwa zitupeleke wapi, na kufanikisha hili itakulazimu kuwa 'business plan'​
 
Biashara ya ajabu sana
Unaweza kuwa expert kabisa na ukala za uso vile vile

🤗🤗🤗
 
Ukiingia vitani tegemea kushinda una 1.5M wenzako wanatafuta 100K or 50K waanze na mkaa biashara yoyote ni wewe mwenyewe jinsi gani ulivojipanga na kupambana zaidi usifanye kitu kwa kuiga angalia wapi UNANUA NA UNAUZA WAPIIIII.
 
Ulikuwa unatamani ufanye biashara gani, na unategemea kuanza na mtaji kiasi gani?
Swali zuri lakini nijuavyo mimi mtaji siyo lazima kitu cha msingi ni wazo la biashara ambalo atalifanyia utafiti na hatimaye kuliandikia mpango wa biashara

Unaweza kuanza biashara kwa mtaji kidogo sana ikibidi, hakika bila mtaji, hahaaa wengi watasema nimechanganyikiwa,

unaweza ukawa na mtaji lakini bila mpango wa biashara pesa yote uliyo nayo itaishia kwenye matatizo ya uanzishaji biashara,
 
Hii Falsafa.🥱
 
Zamani nlikua nikisoma hii kwamba mtaji sio jambo la kwanza nlikua sielewi afu naona kama jamaa wanatuona sie watoto 😹 sa utaanza biashara bila mtaji.

Siku za karibuni nlienda kutafuta frem mahali mfukoni nna buku tu ya maji hata hela ya dalali sikua nayo....

Naamini mtaji unakuja baadae baada ya kuwa na wazo la biashara na utayari wa kuifanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…