Bi. Asha na WomenofSubstanc,
Dada zangu, ndugu zangu hizi habari za 50/50 ni hadithi ambazo zimeandikwa na wanaume kuwapozeni tu. Kitu hiki hakiwezekani sii leo wala kesho ni bora sana kupoteza muda wetu ktk maswala ambayo yanawezekana na yanajenga nchi badala ya kufikiri Uuwiano wa swala zito kama hili.. Hiyo Marekani na nchi za magharibi itachukua miaka 100 ijayo kufikia hata asilimia 40 ya Wabunge wanawake..
Tatizo langu hapa ni uwakilishi, kitu kinachotakiwa ni nafasi sawa meaning hiyo 50/50 inalenga kutazamia UWEZEKANO wa uwakilishi, kuwa mwanamke habaguliwi isipokuwa ana 50/50 chance za kuiandikisha/kugombea na hata Ku win kiti..
Kwa mfano hadi leo hii nchi nyingi zinapuuza na pengine kuondoa majina ya wagombea wanawake..na utakuta nchi za magharibi wanajaribu kwa kiola njia kuboresha mfumo mzima wa Uchaguzi kwa ngazi za vyama hadi Kitaifa lakini sio kulazimisha mfumo utumike ktk swala ambalo linahitaji baraka za wananchi unaowaongoza.
Binafsi naamini kabisa kwamba wanawake wana uwezo sawa kabisa na wanaume ktk uwakilishi wa Wabunge na nina hakika kama vyama vitawaandikisha zaidi ktk kila majimbo kuna uwezekano mkubwa wa wanawake kushinda kutokana na kipaji chao kikubwa ktk ushawishi..
Sasa tunapotaka kutumia kile kinachotokea bungeni na kukilazimisha kuwa sababu ya msingi kuwapa nafasi wanawake kwa sababu tu ni wanawake tunakuwa tunapotosha maana na nguvu ya wanawake ktk jumuiya zetu. Ni kosa kubwa kwa mwanamke kufikiria gender kama sababu ya kugombania kitu ambacho yeye mwenyewe hana mbinu ya kukitatua..Hivyo sababu kubwa ya kuwepo kwa wanawake Bungeni inatanguliwa na sifa na uwezo wa mtu huyo kuwakilisha kwa sababu matatizo mengi ya ndani, mwanamke ndiye yupo karibu zaidi ya mwanaume...
Ni hoja ambayo ina mjadala mkubwa lakini ndio ukweli kama vile majumbani mwa watu. Matatizo mengi ya ndani ya nyumba huyajua mwanamke na ndiye mwakilishi bora wa matatizo ya ndani ikiwa ni pamoja na watoto kuliko mwanaume..lakini huwezi kutambua ubora wa nyumba moja kutokana na uwakilishi wa mtu mmoja, kila nyumba na kila familia ina mwakilishi bora wa matatizo yake kuliko mzazi mwingine..
Na mwisho mtanisamehe, ktk hili nalokusudia kusema...Mwanamke fisadi ni hatari zaidi kuliko mwanamme..kwa sababu she controls the house!..
Waswahili wanasema ni bora mtoto anayeteswa na baba wa kambo kuliko yule anayeteswa na mama wa kambo!