Nape atofautiana na Jaji Warioba Bunge la Katiba

Nape atofautiana na Jaji Warioba Bunge la Katiba

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,418
Reaction score
9,209
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema Bunge Maalumu la Katiba,litatekeleza majukumu yake kwa kufuata Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si mawazo ya mtu yeyote.

Kauli hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa litakuwa jambo lisilo la kawaida kwa Bunge hilo kubadili hoja ya msingi iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba, akisisitiza kuwa jukumu lake ni kuifanyia marekebisho.

Warioba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),kuhusu tafakuri na maridhiano kuelekea katika Katiba Mpya.

Alisema kama Bunge Maalumu la Katiba likipewa jukumu la kuandika Katiba linaweza kubadili mambo mengi, lakini kama Katiba itakuwa imeandaliwa na
chombo kingine, Bunge hilo linatakiwa kutobadili hoja za msingi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Nape alisema: "Mchakato wote wa Katiba Mpya unasimamiwa na sheria na sio maneno ya Warioba. Sheria inazungumzia haki, wajibu na mamlaka ya Bunge hilo, hivyo inawezekana kabisa kuboreshwa na hata kubadilishwa kwa hoja."

Nape alisema kulingana na sheria hiyo,Bunge hilo lina mamlaka ya kufanya jambo lolote katika Rasimu hiyo, ikiwa ni pamoja na kuifanyia maboresho kadri itakavyoonekana kuwa inafaa.

"Bunge haliwezi kutishwa na mtu yeyote kwa sababu lipo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi. Ndiyo maana baada ya Bunge hilo kwisha wananchi watapiga kura yamaoni," alisema.

Akitolea ufafanuzi kauli ya Jaji Warioba kwamba Bunge hilo lifanye maboresho na si kubadili hoja za msingi, Nape alisema:"Maboresho maana yake ni kubadili.

Ukiwa na nyumba ya vyumba vinne na kuiboresha kwa kuweka chumba kimoja si umeibadili?"

Alisema Bunge hilo linatakiwa lisiingiliwe katika uamuzi wake.

Source: Mwananchi.
 
Kama kutakuwepo na suala la kupiga kura kwa wabunge basi watakuwa wamejipanga.Ndio maana kuna makada wengi humo achilia mbali wale watakaonunuliwa
 
Kama kutakuwepo na suala la kupiga kura kwa wabunge basi watakuwa wamejipanga.Ndio maana kuna makada wengi humo achilia mbali wale watakaonunuliwa
Natamani huo utaratibu wa kupiga kura usiwepo. Huwa najiuliza hivi mtu unaweza kabisa kujitoa fahamu na kujifanya hamnazo kana kwamba tz si yako bali wewe ni mali ya chama fulani.
 
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape
Nnauye, amesema Bunge Maalumu la Katiba,
litatekeleza majukumu yake kwa kufuata
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si mawazo
ya mtu yeyote.
Kauli hiyo ya Nape imekuja siku moja baada
ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa
litakuwa jambo lisilo la kawaida kwa Bunge
hilo kubadili hoja ya msingi iliyopo kwenye
Rasimu ya Katiba, akisisitiza kuwa jukumu
lake ni kuifanyia marekebisho.
Warioba alisema hayo juzi alipokuwa
akizungumza katika mkutano ulioandaliwa
na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),
kuhusu tafakuri na maridhiano kuelekea
katika Katiba Mpya.
Alisema kama Bunge Maalumu la Katiba
likipewa jukumu la kuandika Katiba
linaweza kubadili mambo mengi, lakini
kama Katiba itakuwa imeandaliwa na
chombo kingine, Bunge hilo linatakiwa
kutobadili hoja za msingi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Nape
alisema: “Mchakato wote wa Katiba Mpya
unasimamiwa na sheria na sio maneno ya
Warioba. Sheria inazungumzia haki, wajibu
na mamlaka ya Bunge hilo, hivyo
inawezekana kabisa kuboreshwa na hata
kubadilishwa kwa hoja.”
Nape alisema kulingana na sheria hiyo,
Bunge hilo lina mamlaka ya kufanya jambo
lolote katika Rasimu hiyo, ikiwa ni pamoja
na kuifanyia maboresho kadri
itakavyoonekana kuwa inafaa.
“Bunge haliwezi kutishwa na mtu yeyote
kwa sababu lipo kwa ajili ya kuwawakilisha
wananchi. Ndiyo maana baada ya Bunge
hilo kwisha wananchi watapiga kura ya
maoni,” alisema.
Akitolea ufafanuzi kauli ya Jaji Warioba
kwamba Bunge hilo lifanye maboresho na si
kubadili hoja za msingi, Nape alisema:
“Maboresho maana yake ni kubadili. Ukiwa
na nyumba ya vyumba vinne na kuiboresha
kwa kuweka chumba kimoja si umeibadili?”
Alisema Bunge hilo linatakiwa lisiingiliwe
katika uamuzi wake.
Source Mwananchi.

Kama ambavyo pia Bunge la katiba pia halitaburuzwa kufuata matakwa ya kulazimishwa na serikali mbili. Ama hoja kwamba kuna hatari ya kuvunja Muungano, ningeona wanamashiko ya Ukweli kutoka moyoni kama wangesimamia serikali1. Ila hili la serikali2 huwez kuleta hoja inayoeleweka zaidi ya mambo ya hisia tu. Kwa hiyo mh Nape ajue kwamba ni kweli Bunge linaweza kufanya maboresho ya rasimu, lakini ikionekana kuna hila za kisiasa, wajue tutakutana kwenye Refurendum! Lazima ifahamike hivyo.
 
Mmh, inafika mahali natamani kuchukua fimbo niwatandike hawa ma CCM ili akili zao ziwe na akili na kuifanyia kazi.
 
Yani kusema ukweli sijawahi kuona jitu linaloropoka kama nape.eti kuongeza chumba kwenye nyumba ni kubadili na sio kuboresha.alete hoja na sio kubwabwaja!
 
Kama kutakuwepo na suala la kupiga kura kwa wabunge basi watakuwa wamejipanga.Ndio maana kuna makada wengi humo achilia mbali wale watakaonunuliwa

Waache wapige kura zao, ikipigwa kura ya maoni na Wananchi tutaikataa tutoke bila bila waanze upya.
 
Watanzania kwa ujumla tumekuwa wavumilivu mno, ila hili la katiba njia mbadala lazima kukabiliana na hawa "wandazimu".
 
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape
Nnauye, amesema Bunge Maalumu la Katiba,
litatekeleza majukumu yake kwa kufuata
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si mawazo
ya mtu yeyote.
Kauli hiyo ya Nape imekuja siku moja baada
ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa
litakuwa jambo lisilo la kawaida kwa Bunge
hilo kubadili hoja ya msingi iliyopo kwenye
Rasimu ya Katiba, akisisitiza kuwa jukumu
lake ni kuifanyia marekebisho.
Warioba alisema hayo juzi alipokuwa
akizungumza katika mkutano ulioandaliwa
na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),
kuhusu tafakuri na maridhiano kuelekea
katika Katiba Mpya.
Alisema kama Bunge Maalumu la Katiba
likipewa jukumu la kuandika Katiba
linaweza kubadili mambo mengi, lakini
kama Katiba itakuwa imeandaliwa na
chombo kingine, Bunge hilo linatakiwa
kutobadili hoja za msingi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Nape
alisema: “Mchakato wote wa Katiba Mpya
unasimamiwa na sheria na sio maneno ya
Warioba. Sheria inazungumzia haki, wajibu
na mamlaka ya Bunge hilo, hivyo
inawezekana kabisa kuboreshwa na hata
kubadilishwa kwa hoja.”
Nape alisema kulingana na sheria hiyo,
Bunge hilo lina mamlaka ya kufanya jambo
lolote katika Rasimu hiyo, ikiwa ni pamoja
na kuifanyia maboresho kadri
itakavyoonekana kuwa inafaa.
“Bunge haliwezi kutishwa na mtu yeyote
kwa sababu lipo kwa ajili ya kuwawakilisha
wananchi. Ndiyo maana baada ya Bunge
hilo kwisha wananchi watapiga kura ya
maoni,” alisema.
Akitolea ufafanuzi kauli ya Jaji Warioba
kwamba Bunge hilo lifanye maboresho na si
kubadili hoja za msingi, Nape alisema:
“Maboresho maana yake ni kubadili. Ukiwa
na nyumba ya vyumba vinne na kuiboresha
kwa kuweka chumba kimoja si umeibadili?”
Alisema Bunge hilo linatakiwa lisiingiliwe
katika uamuzi wake.
Source Mwananchi.

serkali tatu ni lazima! ima muungano ufe!
 
Sidhani kama ni kweli kuongeza chumba kwenye nyumba ni kubaili! Ila ninachojua hayo ni maboresho! Ukibomoa nyumba yako yenye vyumba viwili na ukajenga nyingine ya vyumba vitatu hayo ndiyo mabadiliko kwa kuwa hata msingi hautakuwa wa kuungaunga na nyumba itaonekana moja na sio yenye viraka! Sasa bwana nape anataka kuwadanganya watanzania kwamba kuongeza chumba ni mabadiliko na siyo maboreesho! Ina maana hata nyumba ukipaka rangi yatakuwa ni mabadiliko si itaonekana tofauti na awali!
 
Back
Top Bottom