Khakha
JF-Expert Member
- Jul 15, 2009
- 2,981
- 1,009
Wanaotaka serikali tatu wanasukumwa na uroho wa madaraka.
Nenda msalani maana ndo mahali pako rasmi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanaotaka serikali tatu wanasukumwa na uroho wa madaraka.
Wanaotaka serikali tatu wanasukumwa na uroho wa madaraka.
Mbona tanzania ni wazoefu wa serikali 3?.
1.serikali za mitaa.
2.serikali ya zanzibar.
3.serikali ya muungano.
hofu iko wapi?
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema Bunge Maalumu la Katiba,litatekeleza majukumu yake kwa kufuata Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si mawazo ya mtu yeyote.
Kauli hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa litakuwa jambo lisilo la kawaida kwa Bunge hilo kubadili hoja ya msingi iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba, akisisitiza kuwa jukumu lake ni kuifanyia marekebisho.
Warioba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),kuhusu tafakuri na maridhiano kuelekea katika Katiba Mpya.
Alisema kama Bunge Maalumu la Katiba likipewa jukumu la kuandika Katiba linaweza kubadili mambo mengi, lakini kama Katiba itakuwa imeandaliwa na
chombo kingine, Bunge hilo linatakiwa kutobadili hoja za msingi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Nape alisema: "Mchakato wote wa Katiba Mpya unasimamiwa na sheria na sio maneno ya Warioba. Sheria inazungumzia haki, wajibu na mamlaka ya Bunge hilo, hivyo inawezekana kabisa kuboreshwa na hata kubadilishwa kwa hoja."
Nape alisema kulingana na sheria hiyo,Bunge hilo lina mamlaka ya kufanya jambo lolote katika Rasimu hiyo, ikiwa ni pamoja na kuifanyia maboresho kadri itakavyoonekana kuwa inafaa.
"Bunge haliwezi kutishwa na mtu yeyote kwa sababu lipo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi. Ndiyo maana baada ya Bunge hilo kwisha wananchi watapiga kura yamaoni," alisema.
Akitolea ufafanuzi kauli ya Jaji Warioba kwamba Bunge hilo lifanye maboresho na si kubadili hoja za msingi, Nape alisema:"Maboresho maana yake ni kubadili.
Ukiwa na nyumba ya vyumba vinne na kuiboresha kwa kuweka chumba kimoja si umeibadili?"
Alisema Bunge hilo linatakiwa lisiingiliwe katika uamuzi wake.
Source: Mwananchi.
Sidhani kama CCM hawalijui hilo, inaelekea kuwa hata huko kwenye kura ya wananchi wamejiandaa kisawasawa ikiwemo wizi wa kura.Waache wapige kura zao, ikipigwa kura ya maoni na Wananchi tutaikataa tutoke bila bila waanze upya.
Hilo sahau, labda kura kama hazitakuwa za siri... Wana CCM wengi chama ndo kinawabana..... Kwani Nimrodi Mkono na wenzie hawakupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu..?? kama ni mimi, hela nachukuwa na kura hupati...Kama kutakuwepo na suala la kupiga kura kwa wabunge basi watakuwa wamejipanga.Ndio maana kuna makada wengi humo achilia mbali wale watakaonunuliwa
Kama Bunge linaweza kufanya yote hayo (Ikiwa ni pamoja na kutunga KATIBA kwa maana ya kutozingatia mawazo ya Wananchi); kamati ya Rasimu ya Katiba iliundwa kufanya nini????
Kama Bunge linaweza kufanya yote hayo (Ikiwa ni pamoja na kutunga KATIBA kwa maana ya kutozingatia mawazo ya Wananchi); kamati ya Rasimu ya Katiba iliundwa kufanya nini????
Jaji anamaanisha kwamba rasimu ni mawazo ya watz, hivyo kama bunge litabadili litakua limehodhi mawazo ya watz
Nape ni vuvuzela, unategemea mtu aliye pata div four awe na mchango wa maana kwenye hili taifa??Kama Bunge linaweza kufanya yote hayo (Ikiwa ni pamoja na kutunga KATIBA kwa maana ya kutozingatia mawazo ya Wananchi); kamati ya Rasimu ya Katiba iliundwa kufanya nini????
Aliyo ongea Jaji Warioba juzi
"Kazi ya Bunge la katiba sio kubadili Rasimu" Joseph Sinde Warioba aliongea juzi haya
Majibu ya Nape jana
Nape Nnauye "Mchakato wa Katiba unasimamiwa na sheria na sio maneno ya Warioba; Bunge linaweza kuboresha na hata kubadilisha Rasimu."
WE REPORT, YOU DECIDE
Mwisho wa nape utakuwa wa aibu sana! Hicho "cheo cha msimu" kimempa kiburi sana, sasa anafikia hadi hatua ya kutukana wazalendo wa kweli wa taifa hili.!