Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ndiyo swali la kujiuliza, kama Tume ya Waryoba ndiyo kila kitu , kwa nini Bunge la Katiba? tuache mbwembwe, Bunge la Katiba inaweza kukubaliana/ kubadili na hata kukataa kabisa kilichomo kwenye rasimu zote mbili. Kile ndicho chombo cha kutunga sheria na hakiwezi kupitisha kila kitu ambacho wananchi wengine walitoa maoni yao waliandaliwa kwa maslahi ya baadhi ya watu wachache. BIG NO.wamekula kodi zetu bure walichotoa hakina maana!!
ila wenyewe wanadai kamati ya rasimu kazi yake ilikuwa ni kutoa tu mwanga wa kianzio, eti bunge hilo ndo litatunga katiba
Safi sana Mkuu, na warejee miswada ya serikali ambayo imekuwa ikiwasilishwa bungeni , siyo yote inayopita kama ilivyowasilishwa na wakati mwingine hukataliwa kabisa na kurudishwa. Nawashangaa sana wanaoabudu rasimu wakati ile ni sawa na mswada tu.
Nape ndio tank thinker wa C.c.m?inasikitisha sana!rasimu ya katiba ni mawazo ya wananchi,bunge halina uhalali wa kubadili maoni na matakwa ya wananchi,bali ni kuboresha
Umeipenda kwa kutoju kasema nini. Na kama Kamati ya WARYOBA ndiyo kila kitu, kwa nini Bunge la Katiba kimeundwa?
Kama Bunge linaweza kufanya yote hayo (Ikiwa ni pamoja na kutunga KATIBA kwa maana ya kutozingatia mawazo ya Wananchi); kamati ya Rasimu ya Katiba iliundwa kufanya nini????
Ni kweli kabisa, lakini kutulazimisha serikali2 na sisi wananchi tuna uhuru wa kukataa serikali2, sawa na wale wanaokataa 3, sawa na wale wanaokataa 1. Kura ya maoni itaamua.! Hatutaki kuhubiri kulinda Muungano kwa viini macho na hadaa, tunataka dhati kutoka moyoni. Dhati halali kuliko zote ni Serikali1, 3 zenyewe nazo ni mashaka, 2 ndo kelele nyingi sana kama wote tunavyofahamu.
Ni kweli kabisa, lakini kutulazimisha serikali2 na sisi wananchi tuna uhuru wa kukataa serikali2, sawa na wale wanaokataa 3, sawa na wale wanaokataa 1. Kura ya maoni itaamua.! Hatutaki kuhubiri kulinda Muungano kwa viini macho na hadaa, tunataka dhati kutoka moyoni. Dhati halali kuliko zote ni Serikali1, 3 zenyewe nazo ni mashaka, 2 ndo kelele nyingi sana kama wote tunavyofahamu.
Ni akili ya matope sana kuamini kuwa mabadiliko ya Kipengele kimoja cha Katiba tena kwa personal interests za watu eti ndiyo mabadiliko. Pole sana Dada yangu.
Binafsi tangu mwanzo sikuona umuhimu wa hilo Bunge, ni ufujaji wa kodi zetu bure. Ilitakiwa maoni ya kamati ya warioba yaletwe kwa wananchi moja kwa moja kwa ajili ya kura ya maoni, period!
Hahaaa, sasa wanakwenda kufanya nini DODOMA? safari hii mtalia sana , MBOWE hana nafasi tena ya kugoma bungeni akiondoka tu bado kuna takribani wabune zaidi ya 500 watafanya vizuri sana hiyo kazi.
ndiyo swali la kujiuliza, kama Tume ya Waryoba ndiyo kila kitu , kwa nini Bunge la Katiba? tuache mbwembwe, Bunge la Katiba inaweza kukubaliana/ kubadili na hata kukataa kabisa kilichomo kwenye rasimu zote mbili. Kile ndicho chombo cha kutunga sheria na hakiwezi kupitisha kila kitu ambacho wananchi wengine walitoa maoni yao waliandaliwa kwa maslahi ya baadhi ya watu wachache. BIG NO.
Ni kweli kabisa, lakini kutulazimisha serikali2 na sisi wananchi tuna uhuru wa kukataa serikali2, sawa na wale wanaokataa 3, sawa na wale wanaokataa 1. Kura ya maoni itaamua.! Hatutaki kuhubiri kulinda Muungano kwa viini macho na hadaa, tunataka dhati kutoka moyoni. Dhati halali kuliko zote ni Serikali1, 3 zenyewe nazo ni mashaka, 2 ndo kelele nyingi sana kama wote tunavyofahamu.
Kwangu mimi ukiangalia maneno yako yanakutafsiri tabia uliyonayo,so kubishana na wewe au kuendelea kukujibu nitapoteza muda wangu.Ni bora kuitwa nina akili ya matope lakini mwisho wa siku nina kubali mabadiliko na pia nina uzalendo na utaifa,kwangu mie utaifa kwanza ubabaishaji baadaye,tunachohitaji ni KATIBA ya watanzania na si KATIBA ya CCM.
Kwa jinsi watanzania tulio wengi tulivyo (shule ndogo, hatufuatilii kinachoendelea katika siasa, hatujitokezi kupiga kura, etc), hata hilo la serikali mbili litapita tena kwa kura nyingi tu.
Me sizungumzii unachowaza wewe,nazungumzia maoni waliyotoa Watanzania juu ya katiba waitakayo,na sheria iliyowekwa juu kuongoza rasimu ya katiba!hizo porojo unazoleta mimi sipo huko
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema Bunge Maalumu la Katiba,litatekeleza majukumu yake kwa kufuata Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si mawazo ya mtu yeyote.
Kauli hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa litakuwa jambo lisilo la kawaida kwa Bunge hilo kubadili hoja ya msingi iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba, akisisitiza kuwa jukumu lake ni kuifanyia marekebisho.
Warioba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),kuhusu tafakuri na maridhiano kuelekea katika Katiba Mpya.
Alisema kama Bunge Maalumu la Katiba likipewa jukumu la kuandika Katiba linaweza kubadili mambo mengi, lakini kama Katiba itakuwa imeandaliwa na
chombo kingine, Bunge hilo linatakiwa kutobadili hoja za msingi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Nape alisema: Mchakato wote wa Katiba Mpya unasimamiwa na sheria na sio maneno ya Warioba. Sheria inazungumzia haki, wajibu na mamlaka ya Bunge hilo, hivyo inawezekana kabisa kuboreshwa na hata kubadilishwa kwa hoja.
Nape alisema kulingana na sheria hiyo,Bunge hilo lina mamlaka ya kufanya jambo lolote katika Rasimu hiyo, ikiwa ni pamoja na kuifanyia maboresho kadri itakavyoonekana kuwa inafaa.
Bunge haliwezi kutishwa na mtu yeyote kwa sababu lipo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi. Ndiyo maana baada ya Bunge hilo kwisha wananchi watapiga kura yamaoni, alisema.
Akitolea ufafanuzi kauli ya Jaji Warioba kwamba Bunge hilo lifanye maboresho na si kubadili hoja za msingi, Nape alisema:Maboresho maana yake ni kubadili.
Ukiwa na nyumba ya vyumba vinne na kuiboresha kwa kuweka chumba kimoja si umeibadili?
Alisema Bunge hilo linatakiwa lisiingiliwe katika uamuzi wake.
Source: Mwananchi.
Ukumbuke kuwa hata serikali imekuwa ikiwasilisha miswada ya sheria mbalimbali bungueni na siyo yote inayopitishwa, ipo inayofanyiwa marekebisho na ipo inayokataliwa kabisa. Usijifanye kuwa haujui uhusiano uliopo kati bunge na mihimili mingine mkuu. Unajitengenezea upofu usio wa lazima kawa sbabu tu una-personal interest fulani.