Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huenda wanafikiri watakaa madarakani mileleccm wanatatizo gani...hiyo ni katiba ya nchi sio chama
Kama kutakuwepo na suala la kupiga kura kwa wabunge basi watakuwa wamejipanga.Ndio maana kuna makada wengi humo achilia mbali wale watakaonunuliwa
uwezo wa warioba kufikiria ni mkubwa kuliko wa nape anayefikiria maswala ya kichama zaidi
Nape ajilinganishe na wakina prof maji marefu na sio warioba
wamebaki kulalama tu, hoja za kwa nini serikali mbili hawana... Warioba yeye katoa hoja, tena alizozikusanya toka lwa wananchi, na zina mashiko hasa
CCM inaangalia masilahi yake kwanza masilahi ya Taifa badae.
domo kubwa point bilabila mh kazi tunayo watz ,
Kitu pekee kinachonipa faraja ni kwamba Nape ana umri mdogo,atazeeka na majuto na masikitiko kwa kusimamia uongo na uovu..malipo ya unafiki hapahapa duniani.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Hski ya Mungu sikujua kama Nape ana akili ndogo hivyo! Yaani MABORESHO NI KUONGEZA CHUMBA- kwa mfano wake aliotoa! Ni mtu wa kufikiria uwingi na sio viwango (yaani Quantity na sio Quality) Bure kabisa. KUBORESHA KAMWE SIO KUBADILI na hili halina utata katika lugha zetu mbili kiingereza na kiswahili. Unaweza kubadili mtaala kwa maana ya kufanya kitu kipya kabisa lakini unaboresha kwa kuongeza au kupunguza baadhi ya masomo au muundo wa kufundisha! Huyu ni aibu kwa Chama Cha Mapinduzi! CCM wamekosa watu wenye akili zaidi ya huyo? puuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Kama Bunge linaweza kufanya yote hayo (Ikiwa ni pamoja na kutunga KATIBA kwa maana ya kutozingatia mawazo ya Wananchi); kamati ya Rasimu ya Katiba iliundwa kufanya nini????
Hii nimeipenda sana
Jaji anamaanisha kwamba rasimu ni mawazo ya watz, hivyo kama bunge litabadili litakua limehodhi mawazo ya watz
Logical question
Very true; hawajamaa wanaandaa mazingira ya kubadirisha maoni ya waTanzania.
Nape ni vuvuzela, unategemea mtu aliye pata div four awe na mchango wa maana kwenye hili taifa??
Mwisho wa nape utakuwa wa aibu sana! Hicho "cheo cha msimu" kimempa kiburi sana, sasa anafikia hadi hatua ya kutukana wazalendo wa kweli wa taifa hili.!
Sasa jamani tulitegemea aseme nini wakati chama chake kinaamini kwenye serikali mbili na ufisadi?Tumsamehe bure ila tumuelimishe tu.
"Mantiki ni kuzuia Bunge Maalumu kunyang'anya madaraka ya wananchi, yaani "act of popular sovereignty". Wataalamu wa masuala ya Katiba wanaeleza kuwa madaraka ya Bunge Maalumu katika mazingira haya ni kuboresha Rasimu ya Katiba.
"Kwa mujibu wa Kifungu cha 25(1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, Bunge Maalumu limepewa madaraka ya kujadili na kupitisha masharti ya Katiba, kutunga Sheria ya Masharti ya Mpito na Masharti yatokanayo na kabla ya kuanza kazi hiyo, Bunge Maalumu litapitisha Kanuni za Bunge Maalumu ambazo zitaongoza utekelezaji wa mamlaka ya Bunge Maalumu."
Bado tunamgeuza Warioba mbuzi wa kafara na kusahau maoni tuliyotoa watz wenyewe?
usisahau kamati ya warioba ndiyo mchakato wenyewe wa wananchi, nawewe nikuulize, kama kuna bunge kwa nini tuwe na kura ya maoni?
anachokisema warioba ndiyo maoni ya watz,tume ilikuwa field na ndicho kilichosemwa! huyo nepi yeye ni vuvuzela tu,anabwabwaja ili mkono uende kinywani tu!
wamekula kodi zetu bure walichotoa hakina maana!!
ila wenyewe wanadai kamati ya rasimu kazi yake ilikuwa ni kutoa tu mwanga wa kianzio, eti bunge hilo ndo litatunga katiba
Nape ndio tank thinker wa C.c.m?inasikitisha sana!rasimu ya katiba ni mawazo ya wananchi,bunge halina uhalali wa kubadili maoni na matakwa ya wananchi,bali ni kuboresha
Binafsi tangu mwanzo sikuona umuhimu wa hilo Bunge, ni ufujaji wa kodi zetu bure. Ilitakiwa maoni ya kamati ya warioba yaletwe kwa wananchi moja kwa moja kwa ajili ya kura ya maoni, period!
Swali zuri sana.
Kwangu mimi ukiangalia maneno yako yanakutafsiri tabia uliyonayo,so kubishana na wewe au kuendelea kukujibu nitapoteza muda wangu.Ni bora kuitwa nina akili ya matope lakini mwisho wa siku nina kubali mabadiliko na pia nina uzalendo na utaifa,kwangu mie utaifa kwanza ubabaishaji baadaye,tunachohitaji ni KATIBA ya watanzania na si KATIBA ya CCM.
Binafsi tangu mwanzo sikuona umuhimu wa hilo Bunge, ni ufujaji wa kodi zetu bure. Ilitakiwa maoni ya kamati ya warioba yaletwe kwa wananchi moja kwa moja kwa ajili ya kura ya maoni, period!
Uelewa wa Nape na akili yake kwa ujumla hana uwezo hata kidogo wa kubishana na Mhe. Jaji Warioba. Anachoweza Nape ni kuongea pumba majukwaani, kupiga ngoma ama gitaa na kukoleza maharage kwa wali pekee. Hayo mambo ya kitaalam na yanayohitaji weledi na akili iliyotulia awaachie wahusika wenyewe.
kuna tofauti kubwa kati ya uandaaji wa miswada ya serikali na hili la katiba mpya! kumbuka kuwa bunge huwakilisha maoni ya wananchi na hii huwa pale wananchi wenyewe hawawezi kupata fursa ya kutoa maoni yao,tofauti na sasa ambapo tayari wananchi wenyewe wametoa maoni yao kupitia tume ya mabadiliko!!!! Hivi wabunge watawezaje kutuwakilisha ili hali sisi wenyewe tumetoa maoni yetu?????
Bunge la katiba ni kwa ajili ya kurekebisha dosari ndogondogo tu na si kubadili maudhui ya rasimu ambayo kimsingi ndiyo maoni ya watz!
Nape acha tuamue sisi
Huenda wanafikiri watakaa madarakani milele
Ama kweli kwenda shule sio kuelimika. Nape Nnauye pamoja na kuungaunga elimu ya UPE hadi ametunukiwa shahada ya uzamili lakini reasoning yake ni mbovu sana hata msomi wa kidato cha nne anaweza kujemga hoja kuliko yeye.
Kubadili na kuboresha ni vitu viwili tofauti kabisa na mimi nashindwa kumshangaa mwenezi wa ccm anaposhindwa kuyatofautisha mambo hayo mawili.
Jamani NAPE amechoka ni wa kusamehe bureee!! Ikifika hatua kijana mdogo kama huyu hawezi kutofautisha kuboresha na kubadili kwa kweli amechoka, yaani kwa ufupi amezeeka kuliko umri wake.
Warioba anaongozwa na Udini tu hana lolote. Kama kweli ni mkerekwetwa wa Maslahi ya Nchi, aeleze kwa nini amedharau Maoni ya Waislamu walio wengi katika nchi hii. Nape amemkumbusha Warioba yale yale alio yasema Raisi, kua Bunge la katiba linamamlaka makubwa zaidi ya Tume ya Warioba, hivyo inaweza kubadilisha na kurekebisha chochote. Hapa hatuongelei uchama, tunaongolea maslahi ya Taifa.
Makubwa! Tunaongelea Maslahi ya Taifa- ambayo ni....sasa hukumalizia, maana umeanza na ...amedharau maoni ya waislamu..." ungeendelea ukaeleza maoni ya kina nani amezingatia, na ndipo uje useme kwa ajili hii - rasimu haina maslahi ya taifa....Lakini nadhani una hekima zaidi ya hapo- usije ukasema maoni ya waislamu yakizingatiwa basi rasimu inaongelea maslahi ya taifa!
Huyo Bwana maslahi ya Taifa kwake ni kuona dini yake inawekwa kuwa ni kundi maalum kwenye Katiba ya nchi, hayo ndiyo maslahi ya taifa kwakeMakubwa! Tunaongelea Maslahi ya Taifa- ambayo ni....sasa hukumalizia, maana umeanza na ...amedharau maoni ya waislamu..." ungeendelea ukaeleza maoni ya kina nani amezingatia, na ndipo uje useme kwa ajili hii - rasimu haina maslahi ya taifa....Lakini nadhani una hekima zaidi ya hapo- usije ukasema maoni ya waislamu yakizingatiwa basi rasimu inaongelea maslahi ya taifa!
Inashangaza kweli mkuuHuenda wanafikiri watakaa madarakani milele