Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Hivyo huyu nape nani kampa huwezo wa kuzungumza upumbavu kama huu.kasomea shule gani huyu?mbona anaongea pumba ?sidhani hata kama alifahuru somo la mahalifa ,maana-ake anaongea pumba sana.naona kama vile ana uwendawazimu au ukichaa fulani wa dkk 2 mbele .naomba atueleze hizo pesa kwenda kwa chadema ametoa nani sio ataje wazungu tu .hao niwatu nanitaasisi aitaje? ,huyu jamaa kweli ni kenge .ebu ccm muangalieni huyu jamaa yenu ,mnaelekea kubaya sana ,viongozi wenu wengi wa chama chenu wanaongea pumbasana ,jamani angalieni nyakati.mshaona kifo cha mendenyie ? Miguu juu.
 
Mara nyingi fikra za mtu aliyemo kwenye box ,hutegemea ukubwa wa box alilomo. hayo ndiyo mawazo ya box alilomo Nape na msimlaum kwa lololte huo ndio uwezo wake ktk kuingamiza ccm na vilevile mjue madhara ya kitu cha kupewa bure bila jasho hakisaminiki na mpokeaji cku zote na ndiyo maana ataendelea kuharisha kwenye vyombo vya habari bila kukarishwa na chama chake.

Tatizo na jambo linalotisha ni kwamba hao wananchi ambao anawaeleza huo uharo WANAAMINI anachowaeleza. Mtaona kwamba anatumia propaganda ile ile ya Mhe Dikteta Robert Mugabe ya kuwaaminisha wananchi wake (tena wasomi) kuwa adui yao mkubwa ni WAZUNGU. Nepi anatumia neno WAZUNGU sio kwa bahati mbaya, bali anajua akiishawaambia wananchi wenye welewa mdogo wataamini kuwa adui ni Wazungu. Kwa bahati mbaya watu wenye welewa mdogo ambao ndio wengi hawawezi kumhoji kuwa mbona Mhe Rais wetu mpendwa Daktari JK huwa siku zote anatamba kuwa husafiri sana kwa WAZUNGU hao hao ili kutuhemelea vibaba tusije tukafa njaa🙁 Huu ni ushahidi kuwa mchakato wa Katiba Mpya umefikia ukingoni. Tuanze kuhamasishana kuanza upya baada ya Katiba ya CCM kupitishwa.
 
Bandari ya Tanga imetajwa katika ripoti ya umoja wa mataifa kua ndo njia ya Mihadarati kubwa Kwa Africa mashariki! Leo Nape na yeye anatusaidi kutoa Ripoti Yake ya kuingizwa Fedha kwa minajili ya kufadhiliwa Cdm! Ikumbukwe kua aliwahi kuja na tuhuma za Cdm kuingiza silaha nchini na alipobanwa sana na kutaka kufunguliwa mashitaka na Cdm akawa kimya! Swali ni kwa hapo badae atakuja na Habari gani tena mpya?

CDM wamesha mstukia Nape, sii sii eem hawana tena kile kitengo cha propaganda, wamebaki na kuzua mambo tuu. Nape anajua akisema huenda na ninyi mkazua yenu ili mshitakiwe. M/kiti Mbowe ana makesi zaidi ya 10 mahakamani. Yoote ya kuzuliwa, kama CCM wataweza kumfanya akasirike atamke uongo unaoweza kuthibitishwa, watapata mwanya wa kumfunga.
Aendelee kuzua mambo tu, ulimwengu ndo watamhukumu sio sisi. Uongo hujitenga ukakaa wenyewe. Hizo pembe na bangi zinazo kamatwa huko nje na zinawahusisha wakuu huko ccm hazioni ila anaona ati Dr. Slaa kapewa hela za kuchafua mchakato wa katiba. Poleni.
Akumbuke kampuni ya kujenga barabara ya mabasi yaendayo kasi, kimewalipukia hicho nacho. Angekuwa na data, hili lingefunikwa sawia. Sasa baasiii.
 
Huyu mropokaji na mada zisizo na vielelezo ni sawa kichwa cha wendawazimu. Nasema kukichafua cdm si jambo jepesi hata kidogo. Namshauri aacha kunya humu jamvini.
 
mfa maji huishia kutapatapa... Nape ni janga la taifa, ccm kimeushiwa sera wanabaki kuropoka tu.. Tanzania ya sasa sii ile ya zamani wasome alama za nyakati kuwa watanzania hawaitaki ccm tena...

Nape majanga
 
ni kweli nauliza kutokana na hizo tuhuma za nape.lakini hata hivyo siyo wewe tu bali hakuna kasuku yoyote anaeweza kujibu.

Usiwe na haraka majibu utayapata 2015..Sio mbali sana tuombe uzima..
 
Nape ni jembe la ukweli maana anaizika CCM kwa kishindo.
 
Hiyo ndo kazi yake nape, lazima aongee ili aingize siku haijalishi anaongea utumbo au uhalo
 
Nimeshangazwa sana na uchochezi unaofanywa na kuwadi wa ccm, Nape !hivi vyombo vya ulinzi na usalama vipo wapi kumuacha mtu kama Nape kuendelea kufanya uchochezi?lakini pia nimeshangazwa na uwezo hafifu alionao kiongozi wa ngazi za juu ndani ya ccm kama Nape, hivi Nape anashidwa kusoma alama za nyakati?bado anawafananisha watanzania wa leo na watanzania wa enzi zile? je baada ya wabunge wa upinzani kutoka nje, wabunge wake wa ccm walijadili hoja ya katiba au waligeuza bunge kuwa ukumbi wa mipasho iliyojaa kejeli na majigambo? je wabunge gani ambao wanatumia kodi zetu vibaya, binafsi naona wabunge wa ccm ndio wanaotufilisi pesa zetu za kodi! Je hoja ya kumlundika raisi madaraka ya kuteua wabunge wa bunge maalumu ni sahihi?nadhani ccm ndio mnaotaka kuharibu mchakato wa katiba na sio People's power! namshauri Nape uchochezi kama huo hauna nafasi katika watanzania wa leo

 
Nape umeanza uvuvuzela tena? Bahati mbaya una uwezo mdogo sana wa kujenga hoja na hakuna Mtanzania atakayekusikiliza! Kajipange upya!
~ Adai ndio chanzo cha kupigana bungeni
~ Asema ndizo walizotumia kuzunguka na helkopta nchini.
~ Aeleza yaliyotokea sio bahati mbaya, Chadema waliyapanga
~ Ashukuru bunge kuendelea kuonyeshwa "live" ili wananchi waone ujinga wao.
~ Awatuhumu kuweka masilahi yao mbele badala ya nchi.
~ Asisitiza CCM kuendelea kuheshimu uamuzi wa wananchi juu ya katiba.
~ Aonyesha madai ya Chadema kitakwimu yasivyojali wakulima na wafanyakazi.


Katibu wa NEC ya CCM itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kinachowasumbua Chadema mpaka wanafanya yote waliyoyafanya hasa ngumi na vurugu bungeni ni namna watakavyoeleza kwa waliowapa pesa za kuvuruga mchakato wa katiba nchini kwani wanatakiwa kupeleka mrejesho jinsi walivyofanikiwa na jinsi walivyotumia mabilioni hayo.

Nape ameyasema hayo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kahama kwenye ikiwa ni sehemu ya ziara ya wilaya zote za mikoa ya kanda ya ziwa ya Shinyanga, Simiyu na Mara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abralhaman Kinana.

"Wenzetu hawa nasikia wamepewa mabilioni toka nje kwa kisingizio cha kushiriki mchakato wa katiba, na kama ilivyo kwa vibaraka wengine katika bara la Afrika lengo la mapesa hayo sio kuwawezesha kushiriki bali kuanzisha fujo na vurugu ili mchakato usimalizike salama iwe ajenda 2015 kwani kimsingi hawana ajenda mpya" alisisitiza Nape.

Akifafanua juu ya suala la pesa kutoka nje Nape alisema mara tu baada ya rasimu ya kwanza kutoka Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa alikwenda nje ya nchi na akakaa kwa muda na aliporudi tu, ndio Chadema wakapanga kuanza kuzunguka na helkopta.

"Babu atwambie alifuata nini nje? Na pesa za kuzunguka na misafara miwili tofauti ya helkopta walitoa wapi? Na watwambie kama walisharudisha mrejesho kwa wafadhili wao" alisema Nape

Nape alisisiza kuwa yote yaliyotokea bungeni si mambo yaliyotokea kwa bahati mbaya isipokuwa ni mambo yaliyopangwa na Chadema katika mkakati wa kutimiza moja ya malengo yao.Alisema ilikua ni lazima watafute mahali pa kufanya kituko bungeni ili iwe mjadala na ili wapate sababu na picha za kuonyesha kwa waliowapa pesa kuwa wanapambana.

"Hili walilofanya Chadema bungeni ni jambo walilopanga katika mkakati wao wa 'civil disobidiency' ...machafuko ya umma dhidi ya dola, mkakati ambao unaratibiwa kutoka nje na baadhi ya wale waliokuwa wakoloni katika nchi zetu za Afrika. Lengo ni kusababisha machafuko na nchi kutotawalika" alisema Nape.

Nape alisema ndio maana CCM ilisisitiza lazima bunge liendelee kuonyeshwa na televisheni ili kuonyesha yanayoendelea bungeni kuwawezesha wananchi kuona kinachofanywa na wawakilishi wao.
"bila shaka wananchi mmeona kilichotokea bungeni kwa macho yenu, sina haja ya kuwaeleza. Mmeona wabunge wa upinzani walichofanya,uchaguzi ujao tupunguze idadi ya wau wasio na maadili bungeni ili kodi zetu zitumike vizuri,kwani tuliwatuma wakajadili maendeleo yetu wao wamegeuza bunge uwanja wa masumbwi.

Aidha Nape akifafanua hoja ya upinzani bungeni juu ya idadi ya wabunge wa bunge maalum la katiba alisema upinzani hawana hoja ya msingi bali wanasukumwa na ubinafsi na ulafi wa madaraka.

"Hoja iliyowafanya wapigane bungeni haina mashiko, wanataka idadi iongezwe ya wabunge wa bunge la katiba kutoka 357 mpaka 792. Hivi nani anabeba mzigo huu wa kuwalipa hawa wabunge kama sio mwananchi wa kawaida? Halafu mnajiita watetezi wa wanyonge? Hawaoni aibu?" alihoji Nape.

Akiendelea kufafanua Nape anasema,"Katika hali ya kawaida tungetegemea wajenge hoja ya kundi kubwa katika jamii ya kitanzania ambao ni wakulima na wafanyakazi ndio wawe na uwakilishi mkubwa kwenye hilo bunge kama tunataka katiba kweli ya wananchi lakini badala yake wao wanapendekeza wawakilishi kutoka vyama vya siasa ukiacha wabunge waliopo sasa wawe 72 na wakulima wawe 10 tu! Wanataka katiba ya vyama vya siasa badala ya katiba ya nchi kwa ajili ya wananchi. Wanataka wafugaji wawe 10 tu na wafanyakazi 40. Kwa uwiano wa kawaida asilimia 80% wa wananchi wa nchi hii ni wakulima, tungetegemea wangependekeza idadi yao kuwa kubwa lakini wao wanawapuuza wakulima na wafugaji kwa kudai wawe kumi tu"!

Nape alimalizia kuwa siku za vyama kama Chadema zinahesabika maana hii ya katiba ndio ilikuwa karata yao ya mwisho.

Amevitahadharisha vyama vingine vya siasa kama CUF, NCCR mageuzi na wengine kuwa wenzao wamepewa mapesa wao wanawaunga mkono kwa ajenda iliyojificha. Na kwa kuwa hili la kuvuruga katiba ndio karata yao ya mwisho basi tutarajie anguko baya sana kwa Chadema na huo ndio utakuwa mwisho wao!
 
Nape again........!!!!!! Bomu la Arusha CDM walijilipua (ushahidi, kapuni), haya sasa fujo bungeni, mabilioni kutoka kwa wazungu (kiasi gani, kimeingia kwa njia zipi,.....)?? Na kwa njia yoyote serikali mnayo nyinyi, jeshi mnalo nyinyi, usalama wa taifa mnao nyinyi, mnataka nini tena? Kamata watu wanaoingiza pesa nchini na ushahidi wake peleka mahakamani watanzania wenye akili wajionee na kufanya maamuzi magumu lakini sahihi....

Unalalama tu hii ni dalili mbaya sana kwa CCM na inathibitisha kukosa weledi katika siasa kwa vijana wachache waliopo ndani ya CCM au ni mamluki nini???
 
...Unamdanganya nani Nape?Hivi huwa huna aibu au unashinikizwa kusema hayo unayoyasema?We endelea kuwadanganya watz ilhali tunajua wazi kuwa CCM haijawahi kuwahurumia watz na kamwe haitakaa ifanye hivyo....CDM inataka wajumbe wa bunge la katiba waongezwe ilha Magamba mshije mkatumia wingi wenu wa sasa bungeni kupitisha maamuzi mabovu ya kujipendelea.Iwapo wajumbe watakuwa zaidi ya 700 hata magamba zaidi ya 300 mkipiga kura bado hamtakuwa mmefikisha robo tatu...POLE NAPE TUMEKUSHTUKIA,Upendo wa Simba kupiga magoti kusali si kumhurumia anayeliwa bali kushukuru kwa kupata kitoweo...
 
Kwa jinsi dunia inavyochukulia suala la 'money laundering' sidhani kama fedha hizo zinzotajwa zingeingia bila kugundulika na wahusika kukamatwa mara moja! Hawa vijana wanasiasa wanawafanya Watanzania ni wa jana hawajui yanayoendelewa na wanaweza kuaminishwa watakacho wanasiasa. Mbaya zaidi hoja inajengwa kwa kuweka uafrika wetu kwamba wapinzani wanaandaa mazingira ya kuleta machafuko. Bahati mbaya historia inaonyesha kuwa machafuko mengi Afrika yanatokea kwa watawala kung'ang'ania madarakani hata pale wananchi wanapowakataa - Mh Kaguta Museveni aliwahi kusema haya siku zake za mwanzo kutawala.
 
Back
Top Bottom