Nape effect: Kosa la Nape ni kuzungumza ukweli kuhusu chaguzi za Tanzania. Hajawakosea wananchi, amewakosea wenye mamlaka

Nape effect: Kosa la Nape ni kuzungumza ukweli kuhusu chaguzi za Tanzania. Hajawakosea wananchi, amewakosea wenye mamlaka

Sasa moja ya hatua hizo ambazo mamlaka imechukua ni kumvua uwaziri wake. we ulitaka ichukue hatua gani?
 
Hakuna rais anayedanganywa kama Samia, hata waliomshauri awatimue wakurugenzi wa makampuni jana wamemdanganya tena. Tatizo kubwa la Nape ni kusema ukweli mchungu kwa viongozi wa CCM.
Unaonesha una akili nyingi sana lakini za kushikwa.

Ukimwaga mboga watu wanamwaga ugali.
 
Ametukejeli wananchi kwamba nyie sio wafanya maamuzi huo muda mnaojisumbua kusimama na kupanga foleni kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kushiriki zoezi la kupiga kura NI KAZI BURE
 
Nape alitukanwa, akaandamwa na pengine ikawa sababu ya kupoteza Uwaziri lakini kwa kinachoendelea kwa sasa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa; Nape alikuwa sahihi kabisa.

Amekosa Uwaziri lakini kauli yake ya ukweli imemsogeza karibu na Muumba.
 
Nape alitukanwa,akaandamwa na pengine ikawa sababu ya kupoteza U waziri lakini kwa kinachoendelea kwa sasa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa;Nape alikuwa sahihi kabisa.

Amekosa U waziri lakini kauli yake ya ukweli imemsogeza karibu na Muumba.
Kwani yupo wapi atupe neno tafadhali.
 
Ccm wanaamini nchi n ya kwao peke yao ....lets wait for Armageddon..
 
Kusema ukweli hakumsafishi dhidi ya maovu yake aliyotenda, na wala hayamtenganishi na wadhalimu wenzake, Once a snake, always a snake.
 
Nape kwa asili ni mtu mwenye mizaha, tabia hii imemsaidia kwingi lakini pia imemuumiza katika mambo mengi. Sio mara ya kwanza kwa Nape kutoa kauli zenye utata kuhusu ushindi wa CCM dhidi ya Upinzani Tanzania. Mwaka 2015 aliwahi kutamka kuwa CCM itashinda hata kwa bao la mkono. Mwaka 2020 katika uchaguzi mkuu tulishuhudia waziwazi bao la mkono maana yake ni nini.

Wiki iliyopita Nape akiwa mkoani Kagera alisikika na kunukuliwa vizuri na media akisema; ushindi katika uchaguzi hutegemea nani anahesabu kura na pia nani anatangaza matokeo. Kumbe mpinzani anaweza kushinda lakini kura zake za ushindi zisihesabiwe akashinda mwingine asiyechaguliwa na wananchi. Au mpinzani akapata kura za ushindi lakini akatangazwa mtu mwingine kuwa ni mshindi.

Mpaka sasa maneno ya Nape yamesababisha viongozi wengine hata wasio wa kisiasa kuondolewa madarakani kutokana na kuonekana kumshukuru Nape kwa utendaji wake wakati akiwa waziri wa Habari na Mawasiliano.

Kosa la Nape ni kuusema ukweli wa chaguzi za Tanzania. Nape ameweka wazi kabisa yanayotendeka nyuma ya pazia katika chaguzi zetu. Mamlaka zilipaswa kuchunguza hoja za Nape na kujirekebisha kuliko kumwondoa tu katika nafasi yake.

Nape amewakosea wenye mamlaka (CCM) na serikali yake lakini amesema ukweli ambao Wananchi tunapenda kuujua.

Pia soma
  1. Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani
  2. Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!
Nape amepoa sana.
Utadhani sio nape yule tumjuaye.
 
Fedheha
 

Attachments

  • b3a34e7e631270a9e73fdd13db687369.mp4
    3.6 MB
  • watermark-51a3cc01acd06eefe8d1d23a20c76918_0.jpeg
    watermark-51a3cc01acd06eefe8d1d23a20c76918_0.jpeg
    516.2 KB · Views: 5
Back
Top Bottom