Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaonesha una akili nyingi sana lakini za kushikwa.Hakuna rais anayedanganywa kama Samia, hata waliomshauri awatimue wakurugenzi wa makampuni jana wamemdanganya tena. Tatizo kubwa la Nape ni kusema ukweli mchungu kwa viongozi wa CCM.
Kwani mlikuwa hamjui kuwa uchaguzi unaibwa siku zote?
Kwamba ulikuwa hujui?
Kufanyaje?Haikuwa rasmi.
Nape na CCM ni Pipaa na mfuniko..yaani hakuna afadhali hapo au angalau🤪🤪Nape alikuwa sahihi kabisa.
Kwani yupo wapi atupe neno tafadhali.Nape alitukanwa,akaandamwa na pengine ikawa sababu ya kupoteza U waziri lakini kwa kinachoendelea kwa sasa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa;Nape alikuwa sahihi kabisa.
Amekosa U waziri lakini kauli yake ya ukweli imemsogeza karibu na Muumba.
Nape amepoa sana.Nape kwa asili ni mtu mwenye mizaha, tabia hii imemsaidia kwingi lakini pia imemuumiza katika mambo mengi. Sio mara ya kwanza kwa Nape kutoa kauli zenye utata kuhusu ushindi wa CCM dhidi ya Upinzani Tanzania. Mwaka 2015 aliwahi kutamka kuwa CCM itashinda hata kwa bao la mkono. Mwaka 2020 katika uchaguzi mkuu tulishuhudia waziwazi bao la mkono maana yake ni nini.
Wiki iliyopita Nape akiwa mkoani Kagera alisikika na kunukuliwa vizuri na media akisema; ushindi katika uchaguzi hutegemea nani anahesabu kura na pia nani anatangaza matokeo. Kumbe mpinzani anaweza kushinda lakini kura zake za ushindi zisihesabiwe akashinda mwingine asiyechaguliwa na wananchi. Au mpinzani akapata kura za ushindi lakini akatangazwa mtu mwingine kuwa ni mshindi.
Mpaka sasa maneno ya Nape yamesababisha viongozi wengine hata wasio wa kisiasa kuondolewa madarakani kutokana na kuonekana kumshukuru Nape kwa utendaji wake wakati akiwa waziri wa Habari na Mawasiliano.
Kosa la Nape ni kuusema ukweli wa chaguzi za Tanzania. Nape ameweka wazi kabisa yanayotendeka nyuma ya pazia katika chaguzi zetu. Mamlaka zilipaswa kuchunguza hoja za Nape na kujirekebisha kuliko kumwondoa tu katika nafasi yake.
Nape amewakosea wenye mamlaka (CCM) na serikali yake lakini amesema ukweli ambao Wananchi tunapenda kuujua.
Pia soma
Viva Nape historia itakulinda