Nape hastahili kusimama kukemea tabia za kutukana watu

Nape hastahili kusimama kukemea tabia za kutukana watu

olimpio

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2023
Posts
418
Reaction score
866
Nimewaza sana maneno ya Nape leo ya kumshambulia Lissu kuwa amemtukana Rais Samia.

Yes , ni kweli ametumia maneno mabaya sana kwa Rais , lakini of all people Nape huwezi kusimama kukemea tabia za kutukana watu.

Wewe ulimtukana Edward Lowassa kuwa ni Oil Chafu, mara mgonjwa, wewe huyu huyu uliwahi kurekediwa ukimtukana Rais aliyepita Hayati Magufuli kuwa ni Mshamba na maneno mengi ya kihaini, huwezi leo kusimama na kujipa uadilifu wa kukemea wengine , ungemuacha Naibu wako Eng Kundo aje akemee uchafu wa matusi ya Lissu lakini sio wewe.

Nakuheshimu sana kama moja ya viongozi vijana wazuri lakini unashida kwenye maadili, kausha kuni kabisa usiongee tena.
 
Kutoa katika kinywa maneno ya kuudhi / kera/ tusi mtu mwingine ni JINAI.

SHERIA IFUATE MKONDO!
 
Nape hajawahi kuwa na akili mtake radhi, kama sio jina la babake ungekuta ni dereva bodaboda tu huko Lindi.
Kuna vijana kwa maelfu wenye uwezo sawa nayeye lakini ni nobody hapa bongo.
Nampa benefit of the doubt , amewahi kuwa katibu mwenezi wa CCM kwa mafanikio makubwa tu , hilo hatuwez kuliondoa , lakini ana kauli chafu sana , yeye kuwa mkuu wa usimamizi wa maudhui hasa ya mitandaoni sio sahihi
 
Sasa kama unamheshimu Nape kama kiongozi kijana mzuri unalalamika nini tena? Hujielewi. Hii mada tupa kule.
shida ya vijana wenye ubongo mgando , hamuelewi
 
Wewe umekubaliana na Nape kuwa Tundu Lissu katukana...
Halafu tena unakuja kumshambulia Nape?

Umewahi sikia msemo unasema
Two wrongs do not make a right?
 
Stahaa👇🤡🤡🤡
ZPSd.jpeg
 
Nimewaza sana maneno ya Nape leo ya kumshambulia Lissu kuwa amemtukana Rais Samia.

Yes , ni kweli ametumia maneno mabaya sana kwa Rais , lakini of all people Nape huwezi kusimama kukemea tabia za kutukana watu.

Wewe ulimtukana Edward Lowassa kuwa ni Oil Chafu, mara mgonjwa, wewe huyu huyu uliwahi kurekediwa ukimtukana Rais aliyepita Hayati Magufuli kuwa ni Mshamba na maneno mengi ya kihaini, huwezi leo kusimama na kujipa uadilifu wa kukemea wengine , ungemuacha Naibu wako Eng Kundo aje akemee uchafu wa matusi ya Lissu lakini sio wewe.

Nakuheshimu sana kama moja ya viongozi vijana wazuri lakini unashida kwenye maadili, kausha kuni kabisa usiongee tena.
Wewe ulimtukana Edward Lowassa kuwa ni Oil Chafu, mara mgonjwa, wewe huyu huyu uliwahi kurekediwa ukimtukana Rais aliyepita Hayati Magufuli kuwa ni Mshamba na maneno mengi ya kihaini, huwezi leo kusimama na kujipa uadilifu wa kukemea wengine[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom