Kuna video clips zinatembea zikionesha gari ya serikali iliyo na plate namba ya waziri wa habari na mawasilno ikidondoka muda mfupi tu baada ya taarifa za kutumbuliwa kwa Nape kuwekwa mitandaoni. Wakati huo Nape ndiyo alikuwa meza kuu akigawa tuzo kama mgeni rasmi, na hata hotuba alikuwa bado hajatoa.
Hii si sawa. Hata kama alikuwa na mapungufu ktk uongozi wake ama kuna kosa kalifanya basi hakustahili kulipwa udhalilishaji huu. Huu siyo utamaduni wetu watanzania na hii si tu inamdhalilisha mhusika, bali inajenga chuki kwa ndugu, jamaa, marafiki, wananchi wa Jimbo lake na watanzania kwa ujumla dhidi ya mamlaka ya uteuzi.
Kama mtu aliteuliwa kwa heshima, akapewa majukumu fulani, basi hata siku ya kumuondoa aondolewe bila kudhalilishwa.
Uovu kama huu aliwahi kufanyiwa pia Dr. Mwigulu Nchemba kipindi cha rais kichaa. Dr. Mwigulu Nchemba alishushwa njiani akiwa safarini kuelekea Mwanza.
Tusiibomoe nchi yetu kwa tabia zetu mbaya na chuki zetu binafsi. Uongozi ni hekima