Nape: Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge haupo kwenye ilani, sie tulinadi mradi wa gesi. Huu tumedandia tu

Nape: Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge haupo kwenye ilani, sie tulinadi mradi wa gesi. Huu tumedandia tu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Waziri wa zamani na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) ameishangaa Serikali kuweka nguvu nyingi kwenye mradi wa umeme wa Stigler’s George ambao haupo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 na kuachana na umeme wa gesi ambao waliunadi wakati wa kampeni.

 
Na moja ya maamuzi mabovu kabisa ya JPM ni kutotoa kipaumbele kwenye sekta ya gas.

Gas ni uchumi

Gas ni viwanda

Gas ni ajira

Gas ni bakora ya siasa za kimataifa....

Too much energy in minerals but madini means nothing but only money!
 
Jamani huyu mtoto ana nini huyu ?

Nape sasa huna maana,Ni kipi ukitakacho ?
Jiulize kwa mapana,na utizame kwa macho
Gesi bado tunavuna,hutaki kiongezwacho?
Stigler ni nyongeza,Umeme kwetu lazima.
 
Naona ameanza kubishana na huyo mwenyekiti wake dikteta ambaye anawasomesha namba mpaka wao
Dikteta ni yule ambae amebadili katiba ya Chadema na kufanya nafasi ya mwenyekiti wa chama haina ukomo wa uongozi. Dikteta niyule ambae pesa za ruzuku za chadema anajilipa madeni ambayo hayaeleweki na hayana mwisho.Dikteta ni yule nafasi za Viti maalumu anazigawa kwa rushwa ya ngono.
 
Mimi nimeshasema kwa sasa hakuna cha ilani, bunge, katiba wala sheria rais ndiye amekuwa mpangaji na mwamuzi wa kila kitu yeye ndiye bunge wa kupanga na kupangua bajeti, ndiye chief procuament and supplies officer, ndiye mwanasheria mkuu, ndiye katiba anacho kisema na kutaka yeye ndicho kinachamualiwa na kufanyika hata kama sheria na katiba vinasema tofauti aliapa kulinda katiba kama kitabu lakini sio kutekeleza yaliyomo
 
Nape mbona unatumia akili ndogo sana ! mlipokuwa mnaahidi Tz ya viwanda mlijua viwanda mtaviendesha kwa nguvu ya soda? kwani huko mnakoandaa ilani yenu huwa hamna strategies za kutimiza ilani hizo ? kama huwa mnazo hizo strategies za kutimiza ilani yenu, huwezi kuikwepa hii ya stieglers gorge ili kutimiza hiyo ahadi yenu ya TANZANIA ya viwanda inawezekana.

Kwa suala la maendeleo ya TZ weka pempeni tofauti zako na mteuzi wako,tunataka nchi isonge mbele doesn't matter who concerned kuleta maendeleo, huu mradi usipofanyika msitegemee kufanikisha hiyo ilani yenu ya tanzania ya viwanda.

Tunataka uhuru wa kiuchumi ,nishati ya umeme ina mchango mkubwa sana ktk kufanikisha hilo, nape acha kuwa kigeu geu,kama unaona mkuu wako kakurupuka huku kwenye stieglers gorge basi team nzima ya kIJANI mlikurupuka maana hamkujua namna ya kufikia lengo lenu. Naunga mkono maendeleo ya TZ yangu
 
Back
Top Bottom