Nape, muda mwingi unaotumia kumsema vibaya Hayati Magufuli ungeutumia kupigania Tozo za Intaneti na Miamala

Shetani hajawahi kuwa binadamu mpaka hapo anakucheka sana
1. Shetani alikuwa malaika wa nuru ila akatamani utukufu wa Mungu ili autwae
2. JPM alikuwa binadamu mwenye asili ya uzao wa 'Adamu na Eva' waliofinyangwa kwa kutumia udongo wa ardhi kisha wakahuishwa pumzi ya Mungu kuwa hai

Je, kama JPM alikuwa shetani alishawahi kuwa malaika?
 
Nape anaongea ukweli kadri anavoujua.
Lakini kiukweli jamaa hapendezwi na kushuka kwa bei za bando!
WaMarekani wenyewe wanashangaa, mbona mabando ghali bila sababu za msingi?
Ukiongea kitu ambacho huweiz kukithibitisha kwa namna yoyote ile hiyo ni kama porojo tu kuwafurahisha baadhi ya watu
 
Unamwambia mnufaika wa hizo Tozo Serikali aimarishe hizo Tozo ?

Tatizo wala sio Makampuni ya Simu Tatizo ni TCRA na Serikali yao amini nakwambia wasingekuwepo watu tungeendelea kupata hata offer za internet bure let alone sasa hivi bundle za bei elekezi isiyoshikika

 
Rekodi ya Matusi ya Nape kwa Lowassa haitavunjwa milele
 
Yeye amesema alienda kufanya uchunguzi 🤷🏻‍♀️ Hatujamlisha maneno, amesema mwenyewe. Swali: Toka lini waziri anafanya uchunguzi?
1. Huyo waziri kachanganyikiwa yaani mwanasiasa anaenda kumchunguza mtu mwenye nafasi sawa na ya kwake? 2. Amekuwa polisi achunguze? Nani alimtuma achunguze?
3. Kwanini hakwenda kwanza polisi kusajili lalamiko lililofika ofisini kwake kisha alikabidhi jeshi la polisi kuchunguza kwa niaba ya Jamhuri?
4. Alikuwa na maslahi gani wakati clouds walisema hawakuomba kuchunguzwa kwa tukio hilo wala hawakwenda kulalamika polisi?
5. Kwanini hakwenda kwenye mamlaka ya uteuzi kushitaki kutokana na kile alichodai uvamizi wa chombo cha habari?
6. Kwanini aliogopa kusajili lalamiko hilo kwa niaba ya chombo cha habari husika kama mtu aliyeathirik kutokana na kitendo cha kiongozi mmojawapo kuvamia chombo hicho?
7. Kwanini amekuwa sehemu ya kulipiza kisasi kwa watu waliomzuia kwenda kuchunguza kile anachodai uvamizi wa chombo cha habari?
 
Sasa mtu baba yake alikua anaimbisha mapambio jeshini akili atatoa wapi??
 
Ukiongea kitu ambacho huweiz kukithibitisha kwa namna yoyote ile hiyo ni kama porojo tu kuwafurahisha baadhi ya watu
Mbona unasahau haraka. Au tatizo lugha??
Uthibitisho: Wamarekani kuleta internet ya gharama nafuu Tanzania.
Wamegundua wanaibiwa!
 
Nape ni aina ya mwanasiasa ambaye mimi binafsi hunivutia mara chache sana; akiwa na madaraka hujisahau kirahisi na kuwa jeuri. Akiwa nje ya madaraka hujitambua na kuwa mnyenyekevu. Pamoja na huo udhaifu kwa hili analolalamikiwa kuwa anamsema vibaya marehemu namuelewa; anayo sababu ya kutosha kufanya hivyo. Anayesemwa na Nape pamoja na raia wengine wengi siyo marehemu wa kawaida tu; huyu ni marehemu aliyeaminiwa na kukabidhiwa mamlaka ya umma. Nape alindwe na aachwe atumie uhuru wake kwa kuyasema yote ambayo hakuyapenda; wenye mazuri ya kuyasema nao wafanye hivyo hivyo! Hii ndiyo njia pekee ya yeye Nape kujifaraji nafsi yake na kujipunguzia machungu ya ule udhalilishaji wa kutembezwa kwa miguu mbele ya kamera kwenda mbele ya "mtukufu" kufanya toba na kuomba msahamaha wa dhambi.

Akiwa kiongozi wa kuchaguliwa na watu, kibinadamu siyo jambo rahisi yeye Nape binafsi pamoja na wananchi waliomwamini na kumchagua kusahau na kusamehe huo udhalilishaji aliofanyiwa. Mambo mengine ni ya kishetani na hayasahauliki wala kusameheka; kutaka kufanya hivyo kirahisi ni sawa sawa na kufungamana na shetani na kazi zake zote na mambo yake. Nchi hii inahitaji kuweka utaratibu wa kitaifa wa kutafakari, kutubu na kuomba msamaha kwa uovu wote wa kipindi kile cha giza. Hili siyo jambo la kuwataka watu mmoja mmoja wanaotoa hisia zao za maumivu hadharani kunyamaza kwa sababu tu aliyewaumiza kwa kutumia mamlaka ya umma amefariki. Isitoshe, mamlaka hayo yaliyotumika kuumiza raia sasa yamekabidhiwa mtu mwingine! Kwani kuna tatizo gani kama mamlaka hayo yakitumika sasa kwa hekima kuwaomba radhi raia ambao wameumizwa kwa matumizu mabaya ya hayo mamlaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…