KERO Nape Nnauye afungia mtandao wa Clubhouse, haupatikani Tanzania bila VPN

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Nape strikes again.

Ukishaonja kula nyama za watu, kamwe hutoacha.

Yuleyule aliyetuondolea bunge live wakati huo akiwa waziri wa habari kipindi cha utawala wa Magufuli, Leo tena akiwa na dhamana hiyohiyo ya Waziri wa habari ameufungia kimyakimya mtandao maarufu wa Clubhouse.

Mtandao wa Clubhouse, ni mtandao ambapo watu popote pale walipo duniani huingia kujadiliana vitu mbalimbali kwa Sauti. Kupitia mtandao huu watu hujadili mada mbalimbali za maisha yao, ikiwemo uchumi, mambo ya kijamii, siasa n.k Nape mwenyewe ashaalikwa katika mada mojawapo kujadili ishu za anwani makazi.

Kutokana na elimu ya kuwaamsha watu na maarifa makubwa ambayo watanzania wamekuwa wakipata kupitia mtandao huo, serikali ya CCM imeona ni tishio kwao. Sasa Nape kama kawaida yake kaufungia mtandao huu ili Watanzania waendelee kuwa gizani.

Nape alipofungia bunge live wananchi walimlaani sana, baadae alipowekwa nje ya madaraka na JPM alikiri kuwa anajuta kushiriki maamuzi yale ya kufungia bunge Live. Leo Nape karudi madarakani kafungia tena mtandao wa Clubhouse ili Watanzania wasiweze kucongregate na kujadili mambo muhimu ya nchi yao.

Soma: TCRA yadai Clubhouse ilipotea kwasababu ya Kiufundi, sasa ipo hewani

Tukumbuke Nape huyuhuyu ndo alikuwa kinara wa kutetea sheria kandamizi ya vyombo vya habari wakati alipokuwa waziri wa habari kipindi cha JPM.

Tunamtaka Nape na TCRA, wafungulie mara moja mtandao wa clubhouse. Haiwezekani Rais Samia anasema kuwa anataka kuifungua nchi, na uhuru wa maoni uwepo, na kukosoa utawala wake ruksa, halafu anakuja Waziri kimyakimya bila kuutarifu Umma anafungia mitandao.

Kwa hivi sasa bila kuwasha VPN huwezi kuupata mtandao huu kwa sababu Nape Nnauye kaufungia.

Huyu Nape anajisahau sana, hii mitandao anayoiona ni mibaya ndiyo hiyohiyo iliyokuwa sauti ya pekee kumtetea kipindi kile katolewa bunduki njenje. Hivi huwa hawajifunzi kitu hawa?
 
Ni wenyewe wanaoumiliki ndio wameufunga, wanafunga kwa baadhi ya nchi, hasa za kiafrika, wameona hauna faida, na mwaka Jana wamepata hasara sana, nasikia Wana mpango wa kuuza, lakini hawajapata mteja.

Imekuwa ngumu kupata matangazo au faida, na kwamba muda mwingi watu wanapigizana kelele tu, na wengine wakiwa wamelewa
 
Umeandika kama vile kuna tofauti kati ya Nape wa Magufuli, na Nape wa Samia.

Nape ni huyo huyo wa Magufuli, wakati ule Samia akiwa msaidizi wa Magufuli, hivyo sishangai tabia za Nape kuendelea kama sasa yule msaidizi wa Magufuli yupo ikulu.
 
Kauli yangu ni moja kila siku, Nape ashukuru Mungu kuwa ni uzao wa baba yake. Kinyume na hapo, huyu jamaa angekuwa kama kina Mwijaku na Baba Levo anatembea barabarani tumbo nje akifanya uchawa.

Nape ana upeo mdogo mno wa fikra,hakupaswa kuwa hata mjumbe wa shina.
 
Sasa kama hadi uwashe vpn ndio unapata sasa nape kafungia kitu gani? Ingekua ni mimi ningefungia popote watu kama Lissu fatma karume na maria sarungi wanapata fursa kusema uongo na kupotosha hali halisi ya siasa na haki za binadami Tanzania.
 
Kuna taarifa yoyote toka twitter inayozungumzia hili? kama unayo tuwekee hapa.

Isijekuwa kwasababu ulikuwa unakerwa na nondo za kule Space, umeona utafute sababu kutetea uamuzi wa kidikteta uliofanywa na serikali uipendayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…