KERO Nape Nnauye afungia mtandao wa Clubhouse, haupatikani Tanzania bila VPN

KERO Nape Nnauye afungia mtandao wa Clubhouse, haupatikani Tanzania bila VPN

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ni wenyewe wanaoumiliki ndio wameufunga, wanafunga kwa baadhi ya nchi, hasa za kiafrika, wameona hauna faida, na mwaka Jana wamepata hasara sana, nasikia Wana mpango wa kuuza, lakini hawajapata mteja.

Imekuwa ngumu kupata matangazo au faida, na kwamba muda mwingi watu wanapigizana kelele tu, na wengine wakiwa wamelewa
Sijaelewa, mfano twitter waamue kuifungia Tanzania kisa kuna hasara. Hii ngumu kumeza, wanatafuta wateja mtandao uwe na mpana harafu waje wabane sehemu ndogo. Kwa nn wasifungie Malawi wafungie Tz.
Ni nape kafunga usitetee
 
Ni wenyewe wanaoumiliki ndio wameufunga, wanafunga kwa baadhi ya nchi, hasa za kiafrika, wameona hauna faida, na mwaka Jana wamepata hasara sana, nasikia Wana mpango wa kuuza, lakini hawajapata mteja.

Imekuwa ngumu kupata matangazo au faida, na kwamba muda mwingi watu wanapigizana kelele tu, na wengine wakiwa wamelewa

Kama watu wanapigazana kelele wakiwa wamelewa ni hasara, bar zote si zingefungwq? Acha utoto dogo.
 
Nape strikes again.

Ukishaonja kula nyama za watu, kamwe hutoacha.

Yuleyule aliyetuondolea bunge live wakati huo akiwa waziri wa habari kipindi cha utawala wa Magufuli, Leo tena akiwa na dhamana hiyohiyo ya Waziri wa habari ameufungia kimyakimya mtandao maarufu wa Clubhouse.

Mtandao wa Clubhouse, ni mtandao ambapo watu popote pale walipo duniani huingia kujadiliana vitu mbalimbali kwa Sauti. Kupitia mtandao huu watu hujadili mada mbalimbali za maisha yao, ikiwemo uchumi, mambo ya kijamii, siasa n.k Nape mwenyewe ashaalikwa katika mada mojawapo kujadili ishu za anwani makazi.

Kutokana na elimu ya kuwaamsha watu na maarifa makubwa ambayo watanzania wamekuwa wakipata kupitia mtandao huo, serikali ya CCM imeona ni tishio kwao. Sasa Nape kama kawaida yake kaufungia mtandao huu ili Watanzania waendelee kuwa gizani.

Nape alipofungia bunge live wananchi walimlaani sana, baadae alipowekwa nje ya madaraka na JPM alikiri kuwa anajuta kushiriki maamuzi yale ya kufungia bunge Live. Leo Nape karudi madarakani kafungia tena mtandao wa Clubhouse ili Watanzania wasiweze kucongregate na kujadili mambo muhimu ya nchi yao.

Tukumbuke Nape huyuhuyu ndo alikuwa kinara wa kutetea sheria kandamizi ya vyombo vya habari wakati alipokuwa waziri wa habari kipindi cha JPM.

Tunamtaka Nape na TCRA, wafungulie mara moja mtandao wa clubhouse. Haiwezekani Rais Samia anasema kuwa anataka kuifungua nchi, na uhuru wa maoni uwepo, na kukosoa utawala wake ruksa, halafu anakuja Waziri kimyakimya bila kuutarifu Umma anafungia mitandao.

Kwa hivi sasa bila kuwasha VPN huwezi kuupata mtandao huu kwa sababu Nape Nnauye kaufungia.

Huyu Nape anajisahau sana, hii mitandao anayoiona ni mibaya ndiyo hiyohiyo iliyokuwa sauti ya pekee kumtetea kipindi kile katolewa bunduki njenje. Hivi huwa hawajifunzi kitu hawa?
Mbona maudhui ya kishoga katika mitandao wanayafumbia macho?
 
Sijaelewa, mfano twitter waamue kuifungia Tanzania kisa kuna hasara. Hii ngumu kumeza, wanatafuta wsteja mtandao uwe na mpana harafu waje wabane sehemu ndogo. Kwa nn wasifungie Malawi wafungie Tz.
Ni nape kafunga usitetee
Mjumbe wa ajabu. Kwanza umesema huelewi halafu unazidi kueleza, huoni kuna tatizo hapo? Ila kwa kweli huelewi, ngoja nikusaidie. Chukua mfano wa TANU au tusema YANGA, ina Malawi duniani kote. Ukidikia tawi la YANGA la Denmark linatoa uongo, au linavunja sheria za huko, ni sawa YANGA Makao Makuu kulichukulia hatua za kinidhamu, ikiwamo kulifunga.
 
WaTz hawana cha maana wanachojadili huko , wacha Nape afungie tu wanajadili upupu mtupu.
 
Mjumbe wa ajabu. Kwanza umesema huelewi halafu unazidi kueleza, huoni kuna tatizo hapo? Ila kwa kweli huelewi, ngoja nikusaidie. Chukua mfano wa TANU au tusema YANGA, ina Malawi duniani kote. Ukidikia tawi la YANGA la Denmark linatoa uongo, au linavunja sheria za huko, ni sawa YANGA Makao Makuu kulichukulia hatua za kinidhamu, ikiwamo kulifunga.
Ndio italichukulia hizo hatua kimya kimya ?? Kwa hiyo wa Tz ndio tunawaingizia hasara sio.
Nakwambia
nape kafunga, kajamaa kaoga, si umeona hata hizi tv za local wamebana tena. Wanataka tbc ndio isikike. mmefungulia mikutano mkabana local tv.
Siwaelewi nyinyi chawa na nitaelezea....
 
Zile websites pendwa zimekosa watetezi kabisa ilhali ndiyo zinatembelewa zaidi kuliko hata hiyo "discohouse".
 
Nape strikes again.

Ukishaonja kula nyama za watu, kamwe hutoacha...
Hawa huwa ni watu wabinafsi sana kwani wanajali matumbo yao tu, kama kuifungia club house hiyo ni kwa ajili ya kulinda cheo chake tu sio vinginevyo, hata alipofungia Bunge live sababu ilikuwa hiyo hiyo na ndio maana alipoondolewa madarakani akajifanya kujutia kitendo kile, unafiki mtupu.
 
Screenshot_20230215-233806.jpg
 
Huyo jamaa Ana laana ya makamba senior kuwa umelahaniwa mbinguni na duniani

Sasa Kuna mtu Happ

Yule aliyemtolea bastola angemalizana nae tu tupunguze wanafiki Kama yeye

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hili jambo ni muhimu likatekelezwa ili kusaidia Wananchi kuifikia Internet kwa urahisi .

Ifahamike kwamba bila kuingia mitandaoni ni sawa na kuzikwa kaburini ukiwa hai , maana sasa imejulikana kwamba Watawala bado wana vimelea vile vile vya awamu ya kikatili

Rejea ya Club House
 
Nape alituambia kwamba Mungu aliamua ugomvi, kwa maana Magifuli kuna watu alikuwa na ugomvi nao ila Mungu akaingilia na kuondoa uhai wa Magufulu na hivyo hao maadui zale wakawa washindi.

Muhimu hapa wale waliyojipa kazi ya kueleza maovu tu ya Magufuli ili wengine wajifunze basi wanatakiwa waongeze kueleza hayo maovu ya Magufuli ili hao wakina Nape wajifunze.
 
Back
Top Bottom