Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Mkuu kuna error imetokea sikuaandika mtandaoni
 
Akili matope ndo hizi...mtu akimtukana Magufuli anakuwa 'mhujumu wa uchumi'?
Ndio rais ni mtu Mkubwa Sana kumtusi ni sawa na kuhujumu uchumi, au wewe hujui? Au unajitoa ufaham? Unadani kumtukana rais wa nchi ni Jambo Dogo Kama unavyoweza kumtus jirani yako, kumtusi rais ni kuitus nchi mkuuu ndio maaana unaona kiongoz yoyote wa nchi nyingne akitusi nchi nyingne au kuikashfu anaambiwa aombe msamaha kwa nchi husika
 
Wewe ndiyo atakaye tuma kama choo kwa buku saba.majority wa supporter wa opposition angalau wana life lakini % kubwa ya washsbiki wa Magu hawajielewi isipokuwa wale wachache sana wanaonufaika
Umesema kweli kabisa. Ila mimi kwa taarifa yako siyo mshabiki wa Magufuli ila ni mwananchi wa Magufuli anayeridhishwa na sehemu ya juhudi zake za uongozi.
 
Ule waraka wazee wa ccm haufai kujadiliwa kwenye vikao; haujadiliki. Lakini kwa maslahi ya chama chao nadhani wazee wenye busara wameona njia bora ni kuwashawishi baadhi ya wahusika kujishusha chini na kuombana msamaha mbele ya camera. Mzee Mangula ametajwatajwa kwenye clip; bila shaka ndiye aliyeratibu haya mambo. Hata misahafu inatufundisha kujisbusha chini ili upate kunyanyuliwa.
 
CCM ni Chama makini sana chini ya uongozi makini wa Mh. Rais wetu mpendwa, JPM..

Chadema haiwezi samehe mtu hata siku moja, ila CCM ni chama cha kujifunza kwa wengine.. Sisi tunaonyesha mfano wa uongozi bora ukoje.

Hongera Mh. Rais na hongera Nape, sasa ni kazi tu
 
Sidhani kama hili ( Nape kuomba msamaha) litamzuia JPM kumkata jina lake kwe uchaguzi ujao. Hii ilikuwa ni justification tu ya kuwa wakina Nape na wenzie walikosea, na mzee baba yeye always yupo right. Na alichotaka JPM, ni hiki kilichotokea.

Kwasababu tayari Nape ameshaonekana ni "kirusi" tangu siku nyingi kwa chama na utawala huu ujumla, basi sina hakika sana kama jina lake litapita tena Mtama 2020.

Duh Magufuli ameishika nchi, bado Membe.

Nappe alikuwa anaenda kukatwa 2020

Njaa haina baunsa.
 
Ndo siasa hizi
unafiki mwanzo mwisho

Baada ya uchaguzi mwakani tutajua rangi halisi za wanasiasa
Kwenye ligi za kabumbu lazima wawepo watu wa kufanya faulo hili ushindi upatikane. Hivyo mzee wa faulo lazima ajisalimishe mapema.
 
Gerson msigwa is typing now, kesho, nape, January kuwa makatibu tawala au wakuu wa mikoa... I bet.
 
huyu anayeombwa msamaha kwa kweli will need his head examined kama anaamini kweli hawa wanaomwomba msamaha wao tayari wamemsamehe in the first place.

2020 ina giza kubwa sana ndani ya hichi chama changu!!
 
Dah! Yani Victoire una mwenyekiti wa chama wa ajabu sana. Umungu upo ndani yake na anauonyesha waziwazi.. Sijawahi kuona hivi vituko aisee!
 
Inategemea na bidii ya kusifia, akiendelea na mafumbo yake atatupiliwa mbali.
 
Quran inasema sifa za mnafiki ni tatu, kwanza akisema hasemi ukweli, akihahidi hatekelezi na akiaminiwa haminiki.
 


Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Mhe. Nape Nnauye amekutana na kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia kuhusika kwake katika mazungumzo yasiyofaa dhidi ya Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Nape Nnauye amekutana na Mhe. Rais Magufuli leo tarehe 10 Septemba, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo, Mhe. Nape amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kukubali ombi lake la kukutana nae na kumsikiliza, na pia kumsamehe kwa makosa aliyoyafanya kufuatia taharuki iliyoibuka baada ya kuvuja kwa sauti za mawasiliano yake na wanasiasa wengine wakimsema Mhe. Rais Magufuli.

“Kwa hiyo baada ya kupata fursa nimekuja nimemuona, na mle ambamo nilimkosea kama Baba yangu nimeongea nae na Baba amenielewa, ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri ambao nitaufanyia kazi na naamini baada ya hapa mambo yatakwenda vizuri, na kwa kweli kwa dhati ya moyo wangu nimshukuru sana sana, amenipa fursa kubwa, ndefu na ameongea maneno mengi kwangu na ushauri wake nimeuchukua” amesema Mhe. Nape Nnauye.

Kuhusu maendeleo, Mhe. Nape Nnauye amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa inayofanywa na Serikali na amesema ana matumaini kuwa CCM itapata ushindi katika chaguzi kutokana na kazi hiyo.

Kwa upande wake, Mhe. Rais Magufuli amesema Mhe. Nape amekuwa akiomba kukutana nae mara nyingi na tangu siku nyingi kupitia kwa watu mbalimbali wakiwemo wasaidizi wake, viongozi wastaafu na viongozi wa CCM, na kwamba baada ya kukutana nae na kumuomba radhi ameamua kumsahehe.

Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mhe. Nape Nnauye kwenda kufanya kazi za kuhudumia wananchi wa Jimbo lake la Mtama na kukitumikia vyema chama chake cha CCM.

“Yote nimesamehe, huyu bado ni kijana mdogo, ana matarajio makubwa katika maisha yake, mimi nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu kwanza ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu na tumefundishwa katika maandiko yote tusamehe saba mara sabini, kwa hiyo nimemsamehe na Mungu amsaidie katika shughuli zake akafanye kazi zake vizuri, akalee Mke wake na familia yake, akakitumikie chama, akawatumikie wananchi wa Jimbo lake vizuri, mimi nimemsamehe, labda kama yeye atakengeuka hiyo itakuwa ni juu yake, lakini mimi kutoka moyoni mwangu nimeshamsamehe na nimemsaheme kweli. Nape nenda ukafanye kazi, Mungu akujaalie” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…