Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Naona uwanja wa vita umekuwa mgumu kiasi kwamba Battalion Commander anaanza kuludisha Comrades aliowastaafisha kwa kusema kuwa wamezeeka, hawana msaada nk!,aliwastaafisha na majukumu yao akawapa watoto aliodhani watamfaa sasa uwanja umekuwa mgumu imebidi aludishe wanaojua vita lakin ili kuficha ukweli anatuambia kuwa comrades ndio wanaomba kuludi........
"Kuludi"ndio nini?,swine!
 
Kitendo cha Nape kuomba msamaha hakuna mslahi kwa taifa zaidi ya chama chake Na yeye binafsi.wanasiasa muda mwingi wanaongozwa Na maslahi binafsi...

Ndio kazi yao na kula yao ilipo so wafanyeje sasa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ukiwaendekeza Hawa utapata tabu sana wewe fanya yako ya kutafuta pesa tu
 
Kww nini misamaha ya mh inatangazwa hadharani? navyofaham msamaha ni siri kati ya muomba msamaha na mtoa msamaha
Isipotangazwa hadharani wakati matusi yametolewa hadharani inakua haileti maana na vilevile husaidia kuzuia propaganda.
 
Rais kama kawaida awasamehe, lakn awe makini na wala asiwaamini tena, kinga ni bora kuliko tiba, once a traitor will always be. Hawa vijana kuna jambo wanatafuta na hapa duniani RAIS haheshimiwi tu pale unapoona unahitaji kitu ama umepoteza kitu. Hence lazima kuwa nao mbali kama jua na ardhi. I have spoken
 
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amefika Ikulu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuomba msamaha. Ameomba msamaha na kusamehewa kosa aliliofanya miezi michache iliyopita.

Akizungumza akiwa nje ya Ikulu baada ya kuzungumza na Rais Magufuli, Nape Nnauye amesema "Kwanza nimekuja kumuona baba yangu lakini Mwenyekiti wa Chama changu, Rais wangu kwasababu wote mnajua mambo yaliyopita au kutokea hapo katikati na mimi kama mtoto wa CCM, kama mwanae, nimeona ni vizuri nije niongee na Baba yangu.

Nashukuru kwamba amenipa fursa ya kuja kumuona na ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri na kwakweli kwa dhati ya moyo wangu nishukuru sana amenipa fursa kubwa sana."

Mbunge Nape anaendelea kusema "Kwa kweli Muheshimiwa Rais kama Baba yangu, kama mzazi wangu nashukuru sana kwa fursa uliyonipa kwa kunisikiliza, kwa kunisamehe, kunishauri, kunielekeza nifanye nini huko mbele ninapokenda."

Rais Magufuli amesma "Mimi nimeshamsamehe kwa dhati Nape, amekuwa akiandika 'message' nyingi sana za kuomba msamaha hata saa nane za usiku nimemuona huyu mtu akiomba msamaha'"

"Leo ameniomba hapa aje anione na kabla, amejaribu sana, ameenda kwa Mzee Mangula amefika hadi kwa Mzee Opson na Mama Nyerere, amehangaika kweli. Na kwamba sisi tumeumbwa kusamehe, na wewe umemuona asubuhi amekuja hapa nikasema siwezi kumzuia kumuona ngoja nimuone kwanza japo nilikuwa na kikao kingine na kikubwa"
ameongeza Rais Magufuli

"Anachozungumza ni kwamba naomba Baba unisamehe, najua kusamehe kunaumiza lakini nasema kwa dhati kabisa nimemsamehe kabisa na anaeleza yaliyokuwa yanamsibu na baadhi ya watu waliokuwa wanamrubuni. Wengine wapo kwenye chama lakini nasema yote tumesamehe kwa sababu bado ni kijana mdogo na ana 'future' nzuri kwenye maisha yake."

"Nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu, kwanza ni dhambi kubwa kwa mwenyezi Mungu na imeandikwa tusamehe saba mara sabini na Mungu amtangulie katika shughuli zake, akalee mke wake na familia yake, akakitumikie chama na akawatumikie wananchi wa jimbo lake."
Amemalizia Rais Magufuli

Wakimalizia katika maongezi yao nje ya Ikulu, Rais Magufuli alimuuliza Nape "Kwa hiyo ulikuwa huna amani?"

Nape: Sana

Rais Magufuli: Uwe na amani na Mungu akusaidie

Pia soma;
Ni muda mwafaka kwa Tindu Lissu naye kuomba msamaha kwa yote aliyowahi kutamka dhidi ya Mh. Raisi na serikali yake kwa faida na maslahi mapana ya nchi yetu; kufanya hivyo kutamuwezesha Mh. Raisi kufanya kazi na vyama vyote kwa masikilizano kwa faida ya Taifa la Tanzania.
 
Huo msamaha unahusu kitu gani hasa, wale walogawa nyumba za serikali kama njugu wao walishaomba msamaha?
 
..unataka mtu kama Mzee Makamba aondoke na kumuachia chama Magufuli?

...Mzee Makamba ametumikia Tanu na Ccm ktk kila ngazi kuanzia shina mpaka Taifa.

..waliosema Jpm hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa shina wa ccm walikuwa na maana yao.

..kwa kifupi Waraka wa Wazee ulikuwa na mbaya kwa Jpm kuliko kwa kina Kinana na Makamba.

..Kitendo cha kuwadukua kilikuwa ni UHALIFU na Mwenyekiti asingeweza kuwabana kwa kutumia taarifa zilizopatikana kwa njia za kuhalifu.

..Lakini pamoja na yote haya waTz wameweza kujua wakina Kinana na Makamba wana mtizamo gani kuhusu Jpm.

..Huku kuombana msamaha hakufuti mtizamo wao kuwa wanamuona Jpm kuwa ni mshamba na kwa hiyo hafai ktk kuongoza ccm.

..Na Jpm asingekuwa na nguvu za DOLA nyuma yake asingeombwa msamaha. Lakini huo ni mjadala wa siku nyingine.

Huwa nawashangaa sana watu kama nyie. Mnawaza sana kuhusu half empty cup of coffee than half full cup of coffee. This attitude reflects your own frustrations in your personal lives. It’s better that you develop the art of positive thinking. Dunia imebadilika sana. Hizo Systems ndizo watu huzilinda kwa manufaa yao binafsi.
 
Magu anamuhitaji Nape kwasababu anahitaji kura za watu wa kusini, na Nape nae anamuhitaji Magu ili ajiweke katika nafasi nzuri ya jina lake kupita kama mgombea 2020.

In short,kila mtu hapo anamuhitaji mwingine kuelekea 2020.

Ni kweli tunajua CCM hawategemei sanduku la kura kushinda, ila ni ukweli pia wangependa zaidi washinde kupitia sanduku la kura.
Nawaonea huruma wakulima wa korosho sasa, maana nape sioni kama atawapigania tena.
 
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amefika Ikulu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuomba msamaha. Ameomba msamaha na kusamehewa kosa aliliofanya miezi michache iliyopita.

Akizungumza akiwa nje ya Ikulu baada ya kuzungumza na Rais Magufuli, Nape Nnauye amesema "Kwanza nimekuja kumuona baba yangu lakini Mwenyekiti wa Chama changu, Rais wangu kwasababu wote mnajua mambo yaliyopita au kutokea hapo katikati na mimi kama mtoto wa CCM, kama mwanae, nimeona ni vizuri nije niongee na Baba yangu.

Nashukuru kwamba amenipa fursa ya kuja kumuona na ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri na kwakweli kwa dhati ya moyo wangu nishukuru sana amenipa fursa kubwa sana."

Mbunge Nape anaendelea kusema "Kwa kweli Muheshimiwa Rais kama Baba yangu, kama mzazi wangu nashukuru sana kwa fursa uliyonipa kwa kunisikiliza, kwa kunisamehe, kunishauri, kunielekeza nifanye nini huko mbele ninapokenda."

Rais Magufuli amesma "Mimi nimeshamsamehe kwa dhati Nape, amekuwa akiandika 'message' nyingi sana za kuomba msamaha hata saa nane za usiku nimemuona huyu mtu akiomba msamaha'"

"Leo ameniomba hapa aje anione na kabla, amejaribu sana, ameenda kwa Mzee Mangula amefika hadi kwa Mzee Opson na Mama Nyerere, amehangaika kweli. Na kwamba sisi tumeumbwa kusamehe, na wewe umemuona asubuhi amekuja hapa nikasema siwezi kumzuia kumuona ngoja nimuone kwanza japo nilikuwa na kikao kingine na kikubwa"
ameongeza Rais Magufuli

"Anachozungumza ni kwamba naomba Baba unisamehe, najua kusamehe kunaumiza lakini nasema kwa dhati kabisa nimemsamehe kabisa na anaeleza yaliyokuwa yanamsibu na baadhi ya watu waliokuwa wanamrubuni. Wengine wapo kwenye chama lakini nasema yote tumesamehe kwa sababu bado ni kijana mdogo na ana 'future' nzuri kwenye maisha yake."

"Nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu, kwanza ni dhambi kubwa kwa mwenyezi Mungu na imeandikwa tusamehe saba mara sabini na Mungu amtangulie katika shughuli zake, akalee mke wake na familia yake, akakitumikie chama na akawatumikie wananchi wa jimbo lake."
Amemalizia Rais Magufuli

Wakimalizia katika maongezi yao nje ya Ikulu, Rais Magufuli alimuuliza Nape "Kwa hiyo ulikuwa huna amani?"

Nape: Sana

Rais Magufuli: Uwe na amani na Mungu akusaidie

Pia soma;
HUYUUUU INAONEKANA NDIE ALIKUWA KIONGOZI WA HILI GENGE NDIO MAANA NA MA CAMERA.TUMEMWEKEA KABISAA ASIJE TULETEA DHARAU ....ALLAH
 
Back
Top Bottom