mwananyaso
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 2,995
- 3,401
"Kuludi"ndio nini?,swine!Naona uwanja wa vita umekuwa mgumu kiasi kwamba Battalion Commander anaanza kuludisha Comrades aliowastaafisha kwa kusema kuwa wamezeeka, hawana msaada nk!,aliwastaafisha na majukumu yao akawapa watoto aliodhani watamfaa sasa uwanja umekuwa mgumu imebidi aludishe wanaojua vita lakin ili kuficha ukweli anatuambia kuwa comrades ndio wanaomba kuludi........
Sawa yeye kaogopa kuwafukuza, na wao pamoja na mizizi hiyo waliyonayo wameshindwa kujiondoa?
Kitendo cha Nape kuomba msamaha hakuna mslahi kwa taifa zaidi ya chama chake Na yeye binafsi.wanasiasa muda mwingi wanaongozwa Na maslahi binafsi...
Islamic fundamentalist your here.Anawafikishia uongo mabeberu halafu kibeberu kinampiga chenga.
Uongo mtupu.
Premature imbecile at work.Acha upotoshaji sio jambo zuri kujifungia chumbani na kupotosha kwenye Mitandao kwa kutomboka tomboka hovyo bila hata advance.
AlhamduliLlah you have noticed that I follow the fundamentals of Islam.Islamic fundamentalist your here.
Mbona unatoka nje ya mada na kuanza personal attack? jikite kwenye mada,hii ni JF na sio Fesibuku.Islamic fundamentalist your here.
Kabisa mkuu hawawezi ku surviveAna safar ndefu kama kijana, ana malengo mengi mbeleNje ya ccm, kuna watu c lolote wala s chchte
Isipotangazwa hadharani wakati matusi yametolewa hadharani inakua haileti maana na vilevile husaidia kuzuia propaganda.Kww nini misamaha ya mh inatangazwa hadharani? navyofaham msamaha ni siri kati ya muomba msamaha na mtoa msamaha
Ni muda mwafaka kwa Tindu Lissu naye kuomba msamaha kwa yote aliyowahi kutamka dhidi ya Mh. Raisi na serikali yake kwa faida na maslahi mapana ya nchi yetu; kufanya hivyo kutamuwezesha Mh. Raisi kufanya kazi na vyama vyote kwa masikilizano kwa faida ya Taifa la Tanzania.Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amefika Ikulu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuomba msamaha. Ameomba msamaha na kusamehewa kosa aliliofanya miezi michache iliyopita.
Akizungumza akiwa nje ya Ikulu baada ya kuzungumza na Rais Magufuli, Nape Nnauye amesema "Kwanza nimekuja kumuona baba yangu lakini Mwenyekiti wa Chama changu, Rais wangu kwasababu wote mnajua mambo yaliyopita au kutokea hapo katikati na mimi kama mtoto wa CCM, kama mwanae, nimeona ni vizuri nije niongee na Baba yangu.
Nashukuru kwamba amenipa fursa ya kuja kumuona na ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri na kwakweli kwa dhati ya moyo wangu nishukuru sana amenipa fursa kubwa sana."
Mbunge Nape anaendelea kusema "Kwa kweli Muheshimiwa Rais kama Baba yangu, kama mzazi wangu nashukuru sana kwa fursa uliyonipa kwa kunisikiliza, kwa kunisamehe, kunishauri, kunielekeza nifanye nini huko mbele ninapokenda."
Rais Magufuli amesma "Mimi nimeshamsamehe kwa dhati Nape, amekuwa akiandika 'message' nyingi sana za kuomba msamaha hata saa nane za usiku nimemuona huyu mtu akiomba msamaha'"
"Leo ameniomba hapa aje anione na kabla, amejaribu sana, ameenda kwa Mzee Mangula amefika hadi kwa Mzee Opson na Mama Nyerere, amehangaika kweli. Na kwamba sisi tumeumbwa kusamehe, na wewe umemuona asubuhi amekuja hapa nikasema siwezi kumzuia kumuona ngoja nimuone kwanza japo nilikuwa na kikao kingine na kikubwa" ameongeza Rais Magufuli
"Anachozungumza ni kwamba naomba Baba unisamehe, najua kusamehe kunaumiza lakini nasema kwa dhati kabisa nimemsamehe kabisa na anaeleza yaliyokuwa yanamsibu na baadhi ya watu waliokuwa wanamrubuni. Wengine wapo kwenye chama lakini nasema yote tumesamehe kwa sababu bado ni kijana mdogo na ana 'future' nzuri kwenye maisha yake."
"Nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu, kwanza ni dhambi kubwa kwa mwenyezi Mungu na imeandikwa tusamehe saba mara sabini na Mungu amtangulie katika shughuli zake, akalee mke wake na familia yake, akakitumikie chama na akawatumikie wananchi wa jimbo lake." Amemalizia Rais Magufuli
Wakimalizia katika maongezi yao nje ya Ikulu, Rais Magufuli alimuuliza Nape "Kwa hiyo ulikuwa huna amani?"
Nape: Sana
Rais Magufuli: Uwe na amani na Mungu akusaidie
Pia soma;
Imevuja sauti inayodaiwa ni Maongezi ya Simu ya Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana kuhusu njama za kuichafua CCM
Ni kuhusu barua iliyotolewa na Makamba na Kinana kuhusu kuchafuliwa na Musiba. Ni Maelekezo ya Kinana Kumtaka Nape aisambaza barua kwenye vyombo vya habari. Kinana: Mwambie bwana hawa jamaa wanatoa statement leo, Unafikiri tumpe nakala? [Nape: Hapana] Mwambie wanaiandaa Mzee wataitoa leo...www.jamiiforums.com
..unataka mtu kama Mzee Makamba aondoke na kumuachia chama Magufuli?
...Mzee Makamba ametumikia Tanu na Ccm ktk kila ngazi kuanzia shina mpaka Taifa.
..waliosema Jpm hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa shina wa ccm walikuwa na maana yao.
..kwa kifupi Waraka wa Wazee ulikuwa na mbaya kwa Jpm kuliko kwa kina Kinana na Makamba.
..Kitendo cha kuwadukua kilikuwa ni UHALIFU na Mwenyekiti asingeweza kuwabana kwa kutumia taarifa zilizopatikana kwa njia za kuhalifu.
..Lakini pamoja na yote haya waTz wameweza kujua wakina Kinana na Makamba wana mtizamo gani kuhusu Jpm.
..Huku kuombana msamaha hakufuti mtizamo wao kuwa wanamuona Jpm kuwa ni mshamba na kwa hiyo hafai ktk kuongoza ccm.
..Na Jpm asingekuwa na nguvu za DOLA nyuma yake asingeombwa msamaha. Lakini huo ni mjadala wa siku nyingine.
Hana chochote. Akitemwa 2020 itabidi awe marioo kwa mkewe.Usikariri anaweza kuajiri vile vile...
Akili hizi January, Ngereja na Nape ndio wanapiga kura?Hahaha
Kwa hizi dalili Magufuli anaenda kushinda 95%
Kwanza inavyoonekana alishtushwa na kusikia January kaenda kuomba msamaha. Ikabidi na yeye akaombe. Kila mtu anakufa kivyake.Nafikiri hili ndio wengine tulishindwa kuliona
Use rational procedure critically, you will understand the content of the thread.AlhamduliLlah you have noticed that I follow the fundamentals of Islam.
Thanks for the praise.
Nawaonea huruma wakulima wa korosho sasa, maana nape sioni kama atawapigania tena.Magu anamuhitaji Nape kwasababu anahitaji kura za watu wa kusini, na Nape nae anamuhitaji Magu ili ajiweke katika nafasi nzuri ya jina lake kupita kama mgombea 2020.
In short,kila mtu hapo anamuhitaji mwingine kuelekea 2020.
Ni kweli tunajua CCM hawategemei sanduku la kura kushinda, ila ni ukweli pia wangependa zaidi washinde kupitia sanduku la kura.
HUYUUUU INAONEKANA NDIE ALIKUWA KIONGOZI WA HILI GENGE NDIO MAANA NA MA CAMERA.TUMEMWEKEA KABISAA ASIJE TULETEA DHARAU ....ALLAHMbunge wa Mtama Nape Nnauye amefika Ikulu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuomba msamaha. Ameomba msamaha na kusamehewa kosa aliliofanya miezi michache iliyopita.