Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Awamu hii kwa mungu wa chato kila goti litapigwaMbunge wa Mtama Nape Nnauye amefika Ikulu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuomba msamaha. Ameomba msamaha na kusamehewa kosa aliliofanya miezi michache iliyopita.
Akizungumza akiwa nje ya Ikulu baada ya kuzungumza na Rais Magufuli, Nape Nnauye amesema "Kwanza nimekuja kumuona baba yangu lakini Mwenyekiti wa Chama changu, Rais wangu kwasababu wote mnajua mambo yaliyopita au kutokea hapo katikati na mimi kama mtoto wa CCM, kama mwanae, nimeona ni vizuri nije niongee na Baba yangu.
Nashukuru kwamba amenipa fursa ya kuja kumuona na ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri na kwakweli kwa dhati ya moyo wangu nishukuru sana amenipa fursa kubwa sana."
Mbunge Nape anaendelea kusema "Kwa kweli Muheshimiwa Rais kama Baba yangu, kama mzazi wangu nashukuru sana kwa fursa uliyonipa kwa kunisikiliza, kwa kunisamehe, kunishauri, kunielekeza nifanye nini huko mbele ninapokenda."
Rais Magufuli amesma "Mimi nimeshamsamehe kwa dhati Nape, amekuwa akiandika 'message' nyingi sana za kuomba msamaha hata saa nane za usiku nimemuona huyu mtu akiomba msamaha'"
"Leo ameniomba hapa aje anione na kabla, amejaribu sana, ameenda kwa Mzee Mangula amefika hadi kwa Mzee Opson na Mama Nyerere, amehangaika kweli. Na kwamba sisi tumeumbwa kusamehe, na wewe umemuona asubuhi amekuja hapa nikasema siwezi kumzuia kumuona ngoja nimuone kwanza japo nilikuwa na kikao kingine na kikubwa" ameongeza Rais Magufuli
"Anachozungumza ni kwamba naomba Baba unisamehe, najua kusamehe kunaumiza lakini nasema kwa dhati kabisa nimemsamehe kabisa na anaeleza yaliyokuwa yanamsibu na baadhi ya watu waliokuwa wanamrubuni. Wengine wapo kwenye chama lakini nasema yote tumesamehe kwa sababu bado ni kijana mdogo na ana 'future' nzuri kwenye maisha yake."
"Nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu, kwanza ni dhambi kubwa kwa mwenyezi Mungu na imeandikwa tusamehe saba mara sabini na Mungu amtangulie katika shughuli zake, akalee mke wake na familia yake, akakitumikie chama na akawatumikie wananchi wa jimbo lake." Amemalizia Rais Magufuli
Wakimalizia katika maongezi yao nje ya Ikulu, Rais Magufuli alimuuliza Nape "Kwa hiyo ulikuwa huna amani?"
Nape: Sana
Rais Magufuli: Uwe na amani na Mungu akusaidie
Pia soma;
Imevuja sauti inayodaiwa ni Maongezi ya Simu ya Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana kuhusu njama za kuichafua CCM
Ni kuhusu barua iliyotolewa na Makamba na Kinana kuhusu kuchafuliwa na Musiba. Ni Maelekezo ya Kinana Kumtaka Nape aisambaza barua kwenye vyombo vya habari. Kinana: Mwambie bwana hawa jamaa wanatoa statement leo, Unafikiri tumpe nakala? [Nape: Hapana] Mwambie wanaiandaa Mzee wataitoa leo...www.jamiiforums.com
Nili-pledge kura milioni kumi na saba kwenye uchaguzi Mkuu ujao. Kuna uwezekano kura zaweza kuvuka pledge yangu kwa mwendo huu.Hahaha
Kwa hizi dalili Magufuli anaenda kushinda 95%
Kupambana na Rais lazima ukubali kupoteza kila kitu,,Nan yupo tayar kupoteza mkate wa fàmilia?Hakuna labda LissuMusiba akatafute kazi nyingine
Waraka wa Wazee ule ulikuwa na Barka za Wenye Chama na sasa umekuwa neema kwa watu kuombana samahani na kuyamaliza
Kidumu chama cha Mapinduzi
Aliyemuita mzee baba mshamba ameshaomba msamaha bado yule Msomali mzee Mali Mali.Musiba akatafute kazi nyingine
Waraka wa Wazee ule ulikuwa na Barka za Wenye Chama na sasa umekuwa neema kwa watu kuombana samahani na kuyamaliza
Kidumu chama cha Mapinduzi
[emoji3] [emoji3]Aliyemuita mzee baba mshamba ameshaomba msamaha bado yule Msomali mzee Mali Mali.
Aliyemuita mzee baba mshamba ameshaomba msamaha bado yule Msomali mzee Mali Mali.
Musiba bado anao wale jamaa waliopeleka kesi kule kwa Ramaphosa, kumbuka ni watanzania wenzetu, ule mchezo bado haujaisha.Musiba akatafute kazi nyingine
Waraka wa Wazee ule ulikuwa na Barka za Wenye Chama na sasa umekuwa neema kwa watu kuombana samahani na kuyamaliza
Kidumu chama cha Mapinduzi
Kumbuka kinana amekimbia uhamishon CanadaMusiba bado anao wale jamaa waliopeleka kesi kule kwa Ramaphosa, kumbuka ni watanzania wenzetu, ule mchezo bado haujaisha.
Magu anamuhitaji Nape kwasababu anahitaji kura za watu wa kusini, na Nape nae anamuhitaji Magu ili ajiweke katika nafasi nzuri ya jina lake kupita kama mgombea 2020.
In short,kila mtu hapo anamuhitaji mwingine kuelekea 2020.
Ni kweli tunajua CCM hawategemei sanduku la kura kushinda, ila ni ukweli pia wangependa zaidi washinde kupitia sanduku la kura.
Walifanyaje hao watu kwaniAkumbuke kufanya kama Akina Ngeleja na Makamba
Nimetazama sana kwa jicho la tatu nimegundua yafuatayo
1. Nape amesoma siasa na ameelewa nyakati hizi ni pambio gani linafaa kuimbwa . Nape halisi tutanwona 2025 panapo majaliwa
2.Nape ameelewa kitakachofuata kwake ikiwa hatajishusha ni kufutwa katika historia ya siasa kwasababu utawala wa sasa hautaki mchezo mchezo maana yake amesoma nyakati
3.tumtazamie Nape akiwa mpole sana Bungeni na yawezekana akarudi kwenye baraza la mawaziri maana ametambua alichokuwa anakitenda na anaye mtendea sio wa kawaida na hataki utani.
4. Ni vema Nape abadilike kabisa isiwe season break tu
Je wewe umeona nini
Kwani hili la Nape kuomba msamaha unadhani limenishtua?Ndio uzuri wa Ccm
Huwa inamaliza mambo yake katika mazingira msiyotarajia
Mzee Kinana na Makamba nae kamalizana nao kwa heshma yao na umri wao kina Mzee Msekwa wameona sio busara waombe radhi hadharan
Ule Waraka ulikuwa wa kuomba Wazee wastaaf waingilie kati na wameingilia kati kweli
Hata Membe kamalizana nae