Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

"Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote,na huo utakatifu,ambao hapana atakayemuona BWANA asipokuwa nao"- waebrania 12:14
 
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amefika Ikulu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuomba msamaha. Ameomba msamaha na kusamehewa kosa aliliofanya miezi michache iliyopita.


Akizungumza akiwa nje ya Ikulu baada ya kuzungumza na Rais Magufuli, Nape Nnauye amesema "Kwanza nimekuja kumuona baba yangu lakini Mwenyekiti wa Chama changu, Rais wangu kwasababu wote mnajua mambo yaliyopita au kutokea hapo katikati na mimi kama mtoto wa CCM, kama mwanae, nimeona ni vizuri nije niongee na Baba yangu.

Nashukuru kwamba amenipa fursa ya kuja kumuona na ameniambia amenisamehe na amenipa ushauri na kwakweli kwa dhati ya moyo wangu nishukuru sana amenipa fursa kubwa sana."



Mbunge Nape anaendelea kusema "Kwa kweli Muheshimiwa Rais kama Baba yangu, kama mzazi wangu nashukuru sana kwa fursa uliyonipa kwa kunisikiliza, kwa kunisamehe, kunishauri, kunielekeza nifanye nini huko mbele ninapokenda."

Rais Magufuli amesma "Mimi nimeshamsamehe kwa dhati Nape, amekuwa akiandika 'message' nyingi sana za kuomba msamaha hata saa nane za usiku nimemuona huyu mtu akiomba msamaha'"

"Leo ameniomba hapa aje anione na kabla, amejaribu sana, ameenda kwa Mzee Mangula amefika hadi kwa Mzee Opson na Mama Nyerere, amehangaika kweli. Na kwamba sisi tumeumbwa kusamehe, na wewe umemuona asubuhi amekuja hapa nikasema siwezi kumzuia kumuona ngoja nimuone kwanza japo nilikuwa na kikao kingine na kikubwa"
ameongeza Rais Magufuli

"Anachozungumza ni kwamba naomba Baba unisamehe, najua kusamehe kunaumiza lakini nasema kwa dhati kabisa nimemsamehe kabisa na anaeleza yaliyokuwa yanamsibu na baadhi ya watu waliokuwa wanamrubuni. Wengine wapo kwenye chama lakini nasema yote tumesamehe kwa sababu bado ni kijana mdogo na ana 'future' nzuri kwenye maisha yake."

"Nikiendelea kumshikilia kwenye moyo wangu, kwanza ni dhambi kubwa kwa mwenyezi Mungu na imeandikwa tusamehe saba mara sabini na Mungu amtangulie katika shughuli zake, akalee mke wake na familia yake, akakitumikie chama na akawatumikie wananchi wa jimbo lake."
Amemalizia Rais Magufuli

Wakimalizia katika maongezi yao nje ya Ikulu, Rais Magufuli alimuuliza Nape "Kwa hiyo ulikuwa huna amani?"

Nape: Sana

Rais Magufuli: Uwe na amani na Mungu akusaidie

Pia soma;
Awamu hii kwa mungu wa chato kila goti litapigwa
 
watu mbona povu, ya ccm waachieni ccm wenyewe, tatizo cdm mnapenda sana kuyaingilia hadi ya ccm kwa ccm na hiyo ni hadi kwa viongozi wenu cjui mkoje
 
Musiba akatafute kazi nyingine

Waraka wa Wazee ule ulikuwa na Barka za Wenye Chama na sasa umekuwa neema kwa watu kuombana samahani na kuyamaliza

Kidumu chama cha Mapinduzi
Kupambana na Rais lazima ukubali kupoteza kila kitu,,Nan yupo tayar kupoteza mkate wa fàmilia?Hakuna labda Lissu
 
Kww nini misamaha ya mh inatangazwa hadharani? navyofaham msamaha ni siri kati ya muomba msamaha na mtoa msamaha
 
Tissue paper hutafutwa saa mtu anataka kujisaidia, huyu bao la mkono tafakuri hiyo.
 
Aliyemuita mzee baba mshamba ameshaomba msamaha bado yule Msomali mzee Mali Mali.

Ndio uzuri wa Ccm

Huwa inamaliza mambo yake katika mazingira msiyotarajia

Mzee Kinana na Makamba nae kamalizana nao kwa heshma yao na umri wao kina Mzee Msekwa wameona sio busara waombe radhi hadharan

Ule Waraka ulikuwa wa kuomba Wazee wastaaf waingilie kati na wameingilia kati kweli

Hata Membe kamalizana nae
 
Bado tuna safari ndefu sana ya kulikomboa Taifa letu kutoka mikononi mwa wahuni, majizi, mafisadi na WAUAJI.

Wanachojali ni MATUMBO YAO tu bali si maslahi ya nchi.

Magu anamuhitaji Nape kwasababu anahitaji kura za watu wa kusini, na Nape nae anamuhitaji Magu ili ajiweke katika nafasi nzuri ya jina lake kupita kama mgombea 2020.

In short,kila mtu hapo anamuhitaji mwingine kuelekea 2020.

Ni kweli tunajua CCM hawategemei sanduku la kura kushinda, ila ni ukweli pia wangependa zaidi washinde kupitia sanduku la kura.
 
Nimetazama sana kwa jicho la tatu nimegundua yafuatayo
1. Nape amesoma siasa na ameelewa nyakati hizi ni pambio gani linafaa kuimbwa . Nape halisi tutanwona 2025 panapo majaliwa

2.Nape ameelewa kitakachofuata kwake ikiwa hatajishusha ni kufutwa katika historia ya siasa kwasababu utawala wa sasa hautaki mchezo mchezo maana yake amesoma nyakati

3.tumtazamie Nape akiwa mpole sana Bungeni na yawezekana akarudi kwenye baraza la mawaziri maana ametambua alichokuwa anakitenda na anaye mtendea sio wa kawaida na hataki utani.

4. Ni vema Nape abadilike kabisa isiwe season break tu



Je wewe umeona nini

Wako baadhi ya wanasiasa wanacheza mchezo wa kisiasa kama unaangalia zile seasons za kikorea....Huwa naziangalia sana zile movie za kikorea...zinafundisha mambo mengi sana kwenye maisha ya kisiasa kuhusu Uaminifu, fitina, unafiki, uzalendo, mikakati, majungu, ushujaa/ujasiri, ubinafsi, uonevu, ubabe, ulimbukeni, ukabila, ufisadi, wizi, ukweli halisi, utaifa na kadhalika.
 
Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko, ni msemo maarufu wenye umri mkubwa.

Kilichofanyika mpaka udukuzi ukaweza kuanikwa hadharani ni kitendo cha kuiua fitina ambayo imekuwa na nguvu ndani ya CCM tangu Mwalimu Nyerere alipoachia nafasi ya uenyekiti.

Fitina imekuwa ikichangia kuwadhoofisha nguvu wenyeviti na ndio maana hata wale wanaodhani kwamba wanafaa kuwa warithi wao wanashindwa kuja kuwa marais, fitina ndio kikwazo kikuu.

Fitina huenda sambamba na unafiki, na unafiki ni hali mbaya sana kwani hakuna tena anayefaa kuaminiwa kati ya wanaokuwa wamekuzunguka.
 
Ndio uzuri wa Ccm

Huwa inamaliza mambo yake katika mazingira msiyotarajia

Mzee Kinana na Makamba nae kamalizana nao kwa heshma yao na umri wao kina Mzee Msekwa wameona sio busara waombe radhi hadharan

Ule Waraka ulikuwa wa kuomba Wazee wastaaf waingilie kati na wameingilia kati kweli

Hata Membe kamalizana nae
Kwani hili la Nape kuomba msamaha unadhani limenishtua?

Kama yule RC PHD mzima aliyetumbuliwa kule Moro kipindi Magu ameingia tu aliandika huko Mitandaoni oooh Baba nimekosa mimi nimekosa sana kama samaki alivyommeza petro sijui nini baba nisamehe 7 mara 70 mimi mkosefu sijui nini,so sishangazwi na style zenu za kuombana msamaha kwa kujinyenyekeza.

No wonder kwa style hii ya kuombana msamaha huku mkisema baba yangu nisamehe baba sijui nini ilimfanya mpk Mwanri akasema itabidi 'mungu' amshukuru Magufuli kwa utendaji kazi wake,hahah.
 
Back
Top Bottom