Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Kufuatia taarifa mfulululizo za wanasiasa wanaoenda kuomba msamaha kwa rais nini kinatafutwa? Alianza Ngereja na January Makamba leo Nape, Hivi ni nani anatafutwa?
 
Mbona ameshukia mbali na makaz ya Rais akaanza kutembea kwa miguu? Uku tunaonaga wageni wengine wanashushwa mbaka karibia na ngazi za kuingia ndani ikulu.

Inawezekana ipo Sababu kwa walio andaa hili Tukio.
 
Kijasusi nimekuelewa sana japo na Mzee Baba nae hajalala Usingizi ,labda apitiwe .
Membe ni mwepesi kama karatasi!
Nchi kama zetu ili mtu atoke madarakani ni mpaka system nzima iwe iwe imaamua hivyo, siyo tu kwa ushawishi wa ka mtu kamoja kama Membe.
 
Membe, ila si wote wanafanya hivyo kutoka moyoni bali tatizo ni katiba inayompa mtu mmoja madaraka makubwa bila kusahau aliyonayo ndani ya chama pia.

Subiri muda wake uishe ndio utajua rangi halisi za wanaodaiwa kwenda kuomba msamaha huku wakiwa na majeraha katika nafsi zao.
 
Katiba aliotuachia Nyerere ndio inasababisha yote haya. Ndio maana sometimes sikumbali yule mzee. Alikua na kaubinafsi flani hivi

Sio yeye tu ,hata Marehemu Mzee Sitta (R.I.P.) kwa Maelekezo ya wana CCM na mfumo mzima wa Chama chini ya mwamvuli wa Taifa.
 
[emoji123][emoji123][emoji123]
Magu anamuhitaji Nape kwasababu anahitaji kura za watu wa kusini, na Nape nae anamuhitaji Magu ili ajiweke katika nafasi nzuri ya jina lake kupita kama mgombea 2020.

In short,kila mtu hapo anamuhitaji mwingine kuelekea 2020.

Ni kweli tunajua CCM hawategemei sanduku la kura kushinda, ila ni ukweli pia wangependa zaidi washinde kupitia sanduku la kura.
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] Najua leo lazima ulale na viatu,!
Vipi jasusi wenu mbobevu Membe watu wake wanasarenda kirahisi namna hii

Usilo lijua litakusumbua sana ,wewe endelea kushangilia tu kwa Sababu Mtazamo wako unaangalia tukio lilo Usoni kwako kwa wakati huo.
 
Unafiki na ubinafsi vimetawala sana mkuu!!
Kwa hiyo kwa akili zenu mlikuwa mmewekeza kwa akina Nape kwamba ndio watawasaidia kujitoa ccm?

Kwanza ninyi sasa hivi mnapambana na Magufuli na siyo ccm, hapo ndio ujinga wenu ulipo
 
Back
Top Bottom