Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Zile tweet na picha za kimafumbo ndio mwisho wake...

Ujumbe ulisha fika Mkuu ,Sababu ya ile Nia na Dhamira ya kukerwa na jambo flani ilitimia baada ya kutapika Nyongo kwa mhusika.
 
Ni vizuri,hamna sababu kuleta ujuaji wakati unajua mwisho wa siku Rais ndio kashika mpini,angempotezea mbali kwenye jimbo lake 2020,bora hao kina Makamba baba mtu,na mwenzie Kinana wameshazeeka hawana cha kupoteza.
 
Magu anamuhitaji Nape kwasababu anahitaji kura za watu wa kusini, na Nape nae anamuhitaji Magu ili ajiweke katika nafasi nzuri ya jina lake kupita kama mgombea 2020.

In short,kila mtu hapo anamuhitaji mwingine kuelekea 2020.

Ni kweli tunajua CCM hawategemei sanduku la kura kushinda, ila ni ukweli pia wangependa zaidi washinde kupitia sanduku la kura.
Magufuli anahitaji kura? Nape ndo anamhitaji Magufuli siyo Magufuli kumhitaji Nape
 
Achaneni na siasa ndugu zangu....
Njooni jukwaa la mapenzi na mahusiano... Tunakula rahaaaa... Wenzenu wako kazini, nyie mko Kama watazamaji wa TV kuangalia wakiwa kazini..
NB: Kuomba msamaha sio ujinga, na kusamehe sio Ujinga as well.. Kila mtu analia "Mama yangu"
Hakuna anaelia "mama yetu"
Kwa kumalizia, kama una mtu una ugomvi nae kaombe msamaha...Kasemehe rais mwenye kila kitu, sasa wewe mwenye bajaji ukatae kwann.
 
Kale Ndimu!
Ona ujinga wenu eti mlikuwa mnawategemea Nape, Membe na kina Kinana na Makamba wawasaidie kujitoa ccm?
Mlivyowajinga zaidi nyie mnapambana na Magufuli badala ya kupambana na ccm iliyomweka hapo alipo, ndio maana mnaramba Mata. Ko ya kila mtu anayeonesha kumkosoa Magufuli.

Mtu akiwauliza sasa hivi kwamba chadema au upinzani kwa ujumla una mikakati gani kuelekea 2020 kupambana na ccm, jibu lenu utasikia Membe kiboko ya Magufuli!
Pumbavu kabisa.
Bado tuna safari ndefu sana ya kulikomboa Taifa letu kutoka mikononi mwa wahuni, majizi, mafisadi na WAUAJI.

Wanachojali ni MATUMBO YAO tu bali si maslahi ya nchi.
 
Siku Kinana na Membe wakija kuomba msamaha mzee baba lazima awatembeze kwa magoti kuanzia getini mpaka ikulu na Waandishi habari wa kutosha kwa ajili ya coverage
 
Membe, ila si wote wanafanya hivyo kutoka moyoni bali tatizo ni katiba inayompa mtu mmoja madaraka makubwa bila kusahau aliyonayo ndani ya chama pia.

Subiri muda wake uishe ndio utajua rangi halisi za wanaodaiwa kwenda kuomba msamaha huku wakiwa na majeraha katika nafsi zao.
Mkuu upo sahihi kabisa yaani anayetafutwa hapo ni Membe, ngoja tuone karata za Jiwe nani atalamba garasa kati yake na mahasimu wake?
 
Hili jukwaa sijui siku hizi vipi, yaani tunaletewa taarifa za kipuuzi sana.
 
Ujumbe ulisha fika Mkuu ,Sababu ya ile Nia na Dhamira ya kukerwa na jambo flani ilitimia baada ya kutapika Nyongo kwa mhusika.
Sasa kile kilicho kuwa kina fanya atapike vile kimeshaondoka?
 
Moods nisaidieni heading hapo juu neno la mwisho nani anatafutwa sio nani anatanua please.
 
Umaskini na ukesefu wa demokrasia ndio unao unatughalimu, fikiria mtu ni dependant toka tumbuni mpka leo unadhani anaweza kusimamia anachokiamini?
 
Ila tatizo ni hao TISS sijui kama watatafsiri ...neno samahani.
 
Watu ambao hawafaham how politician works ndio watashangaa Nape kuomba msamaha. Political is a Science.
 
Back
Top Bottom