Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Huu msemo ni kwa Tanzania tu au unapply Duniani kote. Na huo urafiki au uadui ni kwa maslahi ya nini?
Msemo huu kuwa " hakuna adui wala rafiki wa kudumu kwenye siasa " ni wadunia nzima , urafiki na uadui unategemea tofauti na uungwaji mkono katika sera husika
 
*Nape Amerudi Kwenye* *Reli Sasa* .
Nijambo amabalo wana CCM wengi hawajalifurahia kuona *Nape Moses Nauye* Mbegu iliyo Kufa na kuoza sasa imeanza kuchipua.
Kifo chake kilisababishwa na kusema ukweli palipohitajika kusema ukweli wakati sio utamaduni wa chama cha *CCM* kusema ukweli kwa wanachama wa kawaida kazi yao ni kuisifu serikali na kukisifia chama tu.


Nape ameomba kwa kuikosoa serikali iliposhindwa kununua korosho. *Nape* kaomba msamaha kwa kushinikiza uchunguzi wa Makonda kuvamia kituo redio cha *Clouds* .


*Nape* kaomba msamaha kwa sauti iliyotengenezwa na *Makonda* kuwa naongea na Membe anamuita Mheshimiwa Rais Mshamba.


*Nape* anameomba msamaha kwakuwa alipotolewa bastola na MTU asiejulikana alisema hadharani kwamba aliipigania CCM ili ishinde mwaka 2015 .


Nape kaomba msamaha kwakuwa huonekana yupo karibu na Zito Kabwe na *Membe* hasa kwenye Picha.


Hivyo ndivo vilivyo muuwa Nape.
Mbegu inachupua sasa


Msamaha wa kinafiki wa *Nape* ni kuionyesha dunia kuwa ukisema ukweli *CCM* nikosa sasa ameomba msamaha kwa kuusimamia ukweli.Yeye na Rais wamemaliza kwakuwa Rais *Magufuli* sio MTU wa visasi na anafahamu kabisa *Nape* hajafanya kosa lolote na hajawahi kumkosea na kisiasa hawezi kupambana na hawa vijana ambao wao kesho yao inaweza kuwa nikubwa kuliko yake ya Leo ya kisiasa,ieleweke kuwa Rais amebakiza Miaka Sita yakuongoza kama atashinda 2020 *Nape* au *Makamba* , *Mwigulu* vijana hawa bado wao wana miaka 10 yakuja kuongoza nchi wakijaaliwa kupata Urais.


*Msamaha wa Nape* umemrudishia heshima yake ndani ya CCM ambayo wengi walitamani apotee wakiamini kupotea kwa Nape na Kina *Kinana* ndo kuipoteza CCM ya Zamani.


Wana *CCM* Siku zote huwa wanaombeana Mabaya wakiamini wenye vyeo hawastahili Siku wakitumbuliwa waio na vyeo na wao watapata nafasi na wenye vyeo wanawatumia wasio na *vyeo kama jukwaa la wao kuimbiwa nyimbo za sifa kusifiwa hata wanapo boronga.*


*Namuona *Nape* kesho* Akiwa kiongozi mkubwa mwenye ushawishi ndani ya chama na serikali maana anajua kusifia zaidi kuliko kukosoa sasa baada ya msamaha ni kusifia kwa kwenda mbele nani atamzuia tena. Mbegu itamea 2025 *Nape* hata kuwa Mbegu tena Atakua ni Mti kamili wenye Matunda.
*Hongera Nape umefanya* *maamuzi sahihi* kwa umri ulio nao haijalishi utaanguka Mara ngapi nilazima uamke maana nguvu na sababu unazo.
*Na
MwanafalsafaMweusi* .
 
Hii inaonesha Tanzania tuna watu wa wanamna gani! Jinsi gani watu walivyo vigeugeu wasiyo jua wanacho simamamia na hao ndiyo viongozi wetu, dah! Nawaonea huruma sana mnao panga foleni kwenda kuwachagua hao wanao itwa viongozi.
Hii pointi ya msingi sana japo inachoma
 
HUYU NAPE KUNA KIPI CHA ZIADA ANATAFUTA? KAMA NI MAISHA ASHAYAPATIA
 
Wanaume wa Dar hawa hata misimamo hawana.

Msimamo tu huna utaweza kusimamisha?
 
Pumbavu mwingine. Nape amruka kaka yake (Membe) kipumbavu kabisa. Hovyoo.
Usikute huyo kaka yake mwenyewe nae ameshawekwa kati kitambo tu anasubiri siku ya kutangazwa aende ikulu akapige picha akiomba msamaha kwa unyenyekevu huku akimuita Magu Baba,hahah.
 
Back
Top Bottom