Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Nape Nnauye kama January Makamba, maji ya shingo yamfika. Amuangukia Rais Magufuli baada ya kumnanga

Hahah nimeanza kukubali kauli yako,hivi Nape alishawahi kuajiriwa sehemu nyingine yoyote ile ukiachana na UVCCM/CCM.
Yeye na Bashite hawawezi ajiriwa wala kujiajiri. Siasa ndo inayowaweka mjini.
 
Both had fake smiles! Aliyeomba msamaha hakumaanisha na aliyesamehe pia hakumaanisha. Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Afrika.
 
Kundi la shetani Luciferi
Kweli shetani lucifa hufurahia mafanikio ya muda mfupi,

Lucifa alipowatumia wayahudi kumuua Yesu alifurahi sana,

kimbembe ni pale Yesu kufa na kwenda kuzimu akamyanganya funguo lucifa, Siku ya tatu akapaa mbinguni, furaha ya Lucifer ilikoma ikabaki majuto, alinyongonyea mpaka kesho
 
Nape usisahau pia kwenda kumuomba msamaha Edward Ngoyai Lowassa [emoji41]
 
*Nape Amerudi Kwenye* *Reli Sasa* .
Nijambo amabalo wana CCM wengi hawajalifurahia kuona *Nape Moses Nauye* Mbegu iliyo Kufa na kuoza sasa imeanza kuchipua.
Kifo chake kilisababishwa na kusema ukweli palipohitajika kusema ukweli wakati sio utamaduni wa chama cha *CCM* kusema ukweli kwa wanachama wa kawaida kazi yao ni kuisifu serikali na kukisifia chama tu.


Nape ameomba kwa kuikosoa serikali iliposhindwa kununua korosho. *Nape* kaomba msamaha kwa kushinikiza uchunguzi wa Makonda kuvamia kituo redio cha *Clouds* .


*Nape* kaomba msamaha kwa sauti iliyotengenezwa na *Makonda* kuwa naongea na Membe anamuita Mheshimiwa Rais Mshamba.


*Nape* anameomba msamaha kwakuwa alipotolewa bastola na MTU asiejulikana alisema hadharani kwamba aliipigania CCM ili ishinde mwaka 2015 .


Nape kaomba msamaha kwakuwa huonekana yupo karibu na Zito Kabwe na *Membe* hasa kwenye Picha.


Hivyo ndivo vilivyo muuwa Nape.
Mbegu inachupua sasa


Msamaha wa kinafiki wa *Nape* ni kuionyesha dunia kuwa ukisema ukweli *CCM* nikosa sasa ameomba msamaha kwa kuusimamia ukweli.Yeye na Rais wamemaliza kwakuwa Rais *Magufuli* sio MTU wa visasi na anafahamu kabisa *Nape* hajafanya kosa lolote na hajawahi kumkosea na kisiasa hawezi kupambana na hawa vijana ambao wao kesho yao inaweza kuwa nikubwa kuliko yake ya Leo ya kisiasa,ieleweke kuwa Rais amebakiza Miaka Sita yakuongoza kama atashinda 2020 *Nape* au *Makamba* , *Mwigulu* vijana hawa bado wao wana miaka 10 yakuja kuongoza nchi wakijaaliwa kupata Urais.


*Msamaha wa Nape* umemrudishia heshima yake ndani ya CCM ambayo wengi walitamani apotee wakiamini kupotea kwa Nape na Kina *Kinana* ndo kuipoteza CCM ya Zamani.


Wana *CCM* Siku zote huwa wanaombeana Mabaya wakiamini wenye vyeo hawastahili Siku wakitumbuliwa waio na vyeo na wao watapata nafasi na wenye vyeo wanawatumia wasio na *vyeo kama jukwaa la wao kuimbiwa nyimbo za sifa kusifiwa hata wanapo boronga.*


*Namuona *Nape* kesho* Akiwa kiongozi mkubwa mwenye ushawishi ndani ya chama na serikali maana anajua kusifia zaidi kuliko kukosoa sasa baada ya msamaha ni kusifia kwa kwenda mbele nani atamzuia tena. Mbegu itamea 2025 *Nape* hata kuwa Mbegu tena Atakua ni Mti kamili wenye Matunda.
*Hongera Nape umefanya* *maamuzi sahihi* kwa umri ulio nao haijalishi utaanguka Mara ngapi nilazima uamke maana nguvu na sababu unazo.
*Na
MwanafalsafaMweusi* .
RIP Ruge Mutahaba, hili bandiko limenitia simanzi sana.

Nimekumbuka kuvamiwa kwa clouds Tv. Mpaka kifo cha Ruge,

Hakika watawala ni mawkala wa lucifer
 
Siyo siri,upinzani inabidi kujipanga sana kuiondoa Ccm madarakani. Hawa jamaa wako very well organized. Wanajua kumaliza tofauti zao wenyewe kwa wenyewe. Ingekuwa ni upinzani hapa watu wameshafukuzana siku nyingi kwenye Chama. Kitu kingine nilichojifunza kwenye hili sakata,wazee ni watu muhimu sana ndani ya chama. Busara zote hizi nina uhakika ni za wazee ndani ya Ccm.
Hakuna cha well organized wala nini kwa mwanasiasa yeyote ambaye anategemea siasa Kama ajira lazima atafanya alichofanya nappe
 
UTOKA KUWA MPIGA ZUMARI MKUU NA MPIGA NGOMA WAKATI WA KAMPENI MPAKA KUWA KAMA "MYATIMA"we mean politics.
 
Watu hawajui baada ya ile clip ya audio kutoka nape alikamatwa na watu wasiojulikana wakaminya kimya kimya wakaaa naye chimbo kimya kimya alichofanywa uko hatujui ukitaka amini tafuta siku ile audio imepandishwa hapa JF alafu nenda Twitter tafuta tweet za nape wiki mbili baad ya ile clip nape hakutweet chochote na siyo kawaida yake wazee wakazi walikuwa naye alikuwa chimbo wanaume wamekaa naye uko wanamfanya nini hatujui

Wamemuachia kawa mpole [emoji3][emoji3][emoji3] alifanywa nini siri yake [emoji3][emoji3][emoji3]
Chezea ngosha wewe, mmoja mmoja ananyooka.
Alisikika mlevi mmoja toka mbagala
 
Back
Top Bottom