Nape Nnauye: Kiroboto ulishindwa akiwepo godfather, utaweza leo?

Wacha punda arushe mateke, nimependa huu msamiati dadadeki hahaha Sasa apa patamu
Kumbe jamaa nikiroboto tu 😂😂
Nape naye aanze kutoka hadharani kuonyesha wazi kwa umma kwamba yeye anatetea vile ambavyo Mhe. Humphrey Polepole anavipinga.
Mhe. Polepole anapinga vikali ufisadi, uhuni, wizi, rushwa, upigaji, unyonyaji, ukupe, unyang'anyi na mengine yanayofanana na hayo.
 
Na kama CCM wakimuona Polepole tofauti na huo msimamo wake maanake ni kwamba CCM ya sasa inaiambia umma wa Watanzania kwa uwazi kabisa hadhrani kwamba inaunga mkono rushwa, ufisadi, upigaji, unyonyaji, ukupe, wizi na kuuza rasilimali za Taifa kama vile mwambao mwa bahari kwa mabeberu au wanaofanana na mabeberu.
 
siamini kama kiroboto alishindwa maana kuna alieenda kuomba msamaha ikulu. kitendo cha kuomba msamaha na suluhu na yale maneno tuliyoyasikia yamtoa msamahaa yatosha kujua wakati huo kiroboto alikuwa na uwezo na hakushidwa kwenye hiyo game yao
 
Anapinga now????hali ya kuwa nae alikuwa muhuni
 
Kwa hiyo siasa ndo zilikofika huku............nape si ndo yule alietembea kwa magoti kwenda kumwomba Magu msamaha, leo tayari kawa kambale.
 
Kiroboto tena?

Muda siyo mrefu kigogo atajulikana.

Ajilikane Mara ngapi Kigogo ni January , Nape na zito Kabwe

January Makamba ni kiongozi wao , na Hilo ndio kundi lao

Mzee wa Msoga msimuingize muacheni apumzike wala hawakingii kifua hao wahuni
 
Mkuu hii ya kurudi nyuma miaka 30 ndicho nakitafurahia zaidi kuliko yote endapo katiba mpya itapatikana.
Kama sheria ya bodi ya mikopo ilirudi nyuma zaidi ya miaka 10, hakuna namna mafisadi ya nchi hii hata ya miaka 40 iliyopita yasiwajibishwe na katiba mpya, ndo maana yanaiona chungu na yanafanya kila hila mchakato usifike mwisho.
 
Polepole hajawahi kuwa mtetezi kumbuka alipokuwa Ikulu hayo mambo ya wizi, uhuni, unyonyaji na unyanganyi na utekaji hayo mambo yalitaradadi sana hakuwahi kuinua mdomo wake., wafanyabiashara wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni walinyanganywa hela zao mchana pale kariakoo lakini na utekaji na ufisadi leo ndio ivyo anarusha mateke
 
Yah hii demokrasia ya kurithishana mikoba kama waganga wa jadi haitufai😅
Katiba mpya ituletee kaimu rais wa mpito wa miezi sita tu baasi, rais kama rais apigiwe kura bhana, mambo ya kuletewa rais wa ngekewa yanatugharimu pakubwa....
 
Kwa nini watoto wa viongozi wastaafu wapewe ubalozi ?

Na wewe ndio wale wale wenye mentality za kina Nape

Waafrika tujivue mindset za u-chifu na utoto na ujukuu wa uchifu
 
Polepole alikuwa Ikulu? Kwa hiyo tunaweza kufungamanisha matendo ya serikali au mamlaka za serikali ya SSH na Hamidu Shaka? Au serikali ya JK na Nape? Kama ndivyo basi tutamhusisha Nape na ESCROW na Uchafu mwingine wote uliofanywa na watendaji wa serikali ya JK.
 
Sasa Huyu Nnape baba yake kuuimbia muungano wetu anaona ndo mwenye nchi hii cycle itatupa shida sana kwa ufupi ni kundi la futungo .mbona hatuwasikii watoto wa mwalimu Nyerere wakidai nchi ni yao .watoto wa hawa vigogo watatu wapigwe chini wa hustle kama watanzania wengine .ni watu tu kujivua oblongata ila Pole Pole mantiki yake itasimama Daima
 
Kama sheria ya bodi ya mikopo ilirudi nyuma zaidi ya miaka 10, hakuna namna mafisadi ya nchi hii hata ya miaka 40 iliyopita yasiwajibishwe na katiba mpya, ndo maana yanaiona chungu na yanafanya kila hila mchakato usifike mwisho.
Ila kila jambo lina mwisho wake mkuu
 
Kwanini wakati yanafanyika hayo hakuachia ngazi ili kuonyesha kuchukia angalau au kuitisha wanahabari? sasa anarusha mateke kwa sababu anajua ubunge ukiisha atarudi kuungana na warioba kudai katiba mpya, polepole hakuwa mwana ccm alipandikizwa tu na akina waitara na wenzake mwache arushe mateke halafu atatulia.,
 
Lakini ni mtanzania. Unaweza kuondoa UCCM wake lkn huwezi kuondoa Utanzania wake na UCCM ndani mwake.
 
Anaeongoza Nchi kwa saa ni Mama na wazanzibari wenzie , Mzee wa msoga mnamuonea
Uzoefu umeonyesha Waislamu wakiongoza nchi kunakuwa na uponyaji wa kitaifa, upendo, neema ya mtu mmoja mmoja. Hawana chuki wala kisasi na wanapenda kutafuta hela/ riziki wao wenyewe na hawana hiana na wengine walipata

Mimi ni Mkristu Mkatoliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…