Pre GE2025 Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!

Pre GE2025 Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Teknolojia ya Habari Nape Moses Nnauye amewatoa wasiwasi wakazi wa Bukoba na wanachama wa CCM kuwa Mbunge wao Stephen Byabato atashinda uchaguzi ujao na hakuna mwingine.

"Matokeo ya kura siyo lazima yawe yale ya kwenye box, inategemea nani anahesabu na nani anatangaza. Unajua kuna mbinu nyingi za uchaguzi, Kuna halali, nusu halali na haramu na zote zinaweza kutumika ilimradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe" alisema Nape.

Aliyesema hayo katika Soko la Kashai jana Julai 15 usiku alipoalikwa na Mbunge Byabato kushuhudia ramani na michoro ya Soko jipya la Kashai linalotarajiwa kujengwa.

Kauli ya Chama ~ CCM yakataa maneno aliyosema Nape kuhusu ushindi wa kura unategemea na anayehesabu kura

Pia, utetezi wake: Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani

PIA SOMA
 
Majizi yameanza kuanika siri zao hadharani.

Angeongeza kwenye list hapo sio tu anayehesabu , na kutangaza tu.

Aongeze na msaada wa POLICCM na UsalamaCCM
IMG_20201028_173703.jpg
IMG_20201027_222808.jpg
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Teknolojia ya Habari Nape Moses Nnauye amewatoa wasiwasi wakazi wa Bukoba na wanachama wa CCM kuwa Mbunge wao Stephen Byabato atashinda uchaguzi ujao na hakuna mwingine.

"Matokeo ya kura siyo lazima yawe yale ya kwenye box, inategemea nani anahesabu na nani anatangaza. Unajua kuna mbinu nyingi za uchaguzi, Kuna halali, nusu halali na haramu na zote zinaweza kutumika ilimradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe" alisema Nape.

Aliyesema hayo katika Soko la Kashai jana Julai 15 usiku alipoalikwa na Mbunge Byabato kushuhudia ramani na michoro ya Soko jipya la Kashai linalotarajiwa kujengwa.
Wallah hawa watu wamevimbia na ulevi wa madaraka. Yani mtu anakiri hadharani kitu kama hiki na ni kiburi kuwa nitafanywa nini.
 
Haya ni maneno ya kusema ukiwa na hawara yako au kimoyo moyo au ukiwa na washikaji zako mnavuta Bangi..., ila sio waziri mwenye dhamana tena kwenye kadamnasi
Ni kiburi na jeuri. Washajua kuwa wanaongoza wafu ndio maana wana guts za kusema chochote maana hakuna tutakachofanya zaidi ya kulalamika mtandaoni.
 
Back
Top Bottom