Nape Nnauye samehe na kusahau, mwache Hayati Magufuli apumzike

Nape Nnauye samehe na kusahau, mwache Hayati Magufuli apumzike

Mtoa hoja ngoja tuwe sober hapa,wewe inafikiria mh. Nape hakua mkweli alipotamka kuwa bei ya korosho imeshuka kutokana na serikali ya President Magufuri kutokusema ukweli na kuwa na mwelekeo wa bei ya korosho?its not a rocket science bei ya korosho iliathirika mno na awamu ya tano ya kuingiza siasa mno kwenye jambo hili
Sio korosho tu!kule dodoma mbaazi ilishuka bei hadi waziri akasema Tule eti zina protein nyingi!!!Nape hajakosea!!Jpm ni janga!!
 
Mimba ya Magufuli itawatesa wengi na siyo Nape tu, wapo pia akina Lema na Lisu

Muulizeni kwenye huo mfumo anaouita mbovu Korosho ilikuwa bei gani na sasa mfumo ukiwa mzuri korosho ni shs ngapi?
Fools are fools never argue with them people will Neve rknow who is a fool.

Kabla ya magufuli kuwa rais korosho ilikuwa Bei gani? Na Sasa Nini kimewafanya washindwe kupandisha Bei ya korosho? Je Bei ya vitu vingine Kama fuel, gas na mahitaji mengine nchini yanayopanda Sasa kapandisha magufuli?
 
Mtoa mada ndio umemtaja magu ila Nape alisema "mfumo mbovu wa ununuzi wa korosho"
 
Ila JPM alitaka kufuta "madili" katika chama. Basi kwa mantiki hiyo wanaomchukia waliokuwa wapigaji madili.
 
Jana nilikuwa jimboni Mtama, sehemu ambayo mwakilishi wake kwenye bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nape Moses Nnauye mwanasiasa kijana aliyewahi kuwa Mwenezi wa CCM na Waziri wakati fulani.

Akiwa kwenye mikutano yake kwa wapiga kura wa Mtama, jioni ya jana ilikuwa zamu ya Nyangao sehemu ambayo ipo kilomita chache toka makao makuu ya halmashauri ya Mtama.

Katika hali ambayo iliniacha na maswali ni namna Nape alivyokuwa anajibu maswali ya wananchi wake kwa kupeleka lawama kwa Hayati JPM.

Mfano alipotakiwa atolee maelezo kwanini zao la korosho msimu huu bei yake ghalani imekuwa ndogo Nape akaaminisha umma hayo ni matokeo ya mfumo mbovu uliotumika wakati uliopita wa Serikali kununua Korosho.

Sipo hapa kusadiki ama kutosadiki aliyozungumza Nape bali ni kuishangaa chuki ya wazi kwa Hayati JPM mwenyewe. Ningemwelewa Nape kama angesema haya ni matokeo mabovu ya serikali ya chama cha Mapinduzi badala ya kum'attack mtu ambaye hawezi kujitetea tena.

Serikali ya CCM ingali madarakani bado inao wajibu wa kueleza haya kwa wananchi wake kuliko kujificha kwenye kivuli cha hayati.

Msafiri.
Safarini Mtama.
HUYO NAE KAISHIWA SERA AJIANDAEE KUSHINDWA 2025
 
Back
Top Bottom