Nape Nnauye: Tanzania kuwa na Satelaiti yake kama backup ya internet, Mkongo uliokatika kuchukua siku 7 zaidi kutengamaa

Nadhani hadi kufikia sasa, saa kumi na nusu wamesharejesha asilimia 99.99 ya internet. Hongereni sana.
 
Ainisha uhovyo wake,acheni chuki zisizo na msingi
Kama unajua utendaji wake then ulikuwa hauna ulazima wa kuhoji na kama haujui why unasema ni chuki, kwan mimi namfahamu personally hadi nimchukie?

Yule ni public figure na ana vitu vingi mtandaoni ambavyo ameweka huko mtandaoni ndivyo tunavyotumia kumhukumu wala sio chuki binafsi.
 
Huyu ni kati ya mawaziri wasiokuwa na sifa ya u waziri na taswira halisi ya serikali ya Mzanzibari mtawala wa Tanganyika
 
Vitu gani,utendaji upi umeona wa hovyo?
 
Kuna watu wanaamini hizi porojo za kina Nape?
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Tanzania, Nape Nnauye amesema Serikali inaona umuhimu wa kuwa na satellite na kwamba suala la ununuzi wake si kama kununua nyanya ni mchakato wa muda mrefu.

“Tulianzisha hili kwenye bajeti iliyopita, tumeanzisha kamati, tupo hatua za mbele sana kufikia kuwa na satellite yetu,” amesema Nape.

Waziri Nape amesema hayo leo Jumatano, Mei 22, 2024 wakati akichangia mjadala wa X Space, unaoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kila Jumatano na mjadala huu una mada: “Tufanye nini tatizo la kukosekana kwa Intaneti lisijirudie.”

Msingi wa mjadala huo ni kilichotokea Mei 12, 2024 kwa kukosekana na huduma ya intaneti kwa siku takribani mbili iliyotokana na huduma wa nyaya za baharini Seacom na EASSy kupata hitilafu kwenye nyaya hizo zilizoko kati ya Msumbiji na Afrika Kusini.

Katika maelezo yake, Waziri Nape amesema: “Hata nchi zilizoathirika na intaneti zilikuwa na satellite, ndio maana nasema satellite inategemea hali ya hewa ina changamoto nyingi sana ambazo nasema si njia nzuri ya kuwasiliana ndio maana dunia iliweka kebo kuwasiliana.”

“Hii huduma tunayotumia ni huduma mbadala, kuna mtu anasema tuwe na kebo yetu wenyewe niseme kuwa hakuna gharama ya kupitisha kebo baharini na usalama wake lazima iwe ni mshikamano wa nchi,” amesema.

Waziri huyo amesema, “kwa jiogorafia tuliyonayo tutaongeza idadi ya kebo ili inapokatika moja tuunganishe nyingine.”

“Kama Serikali hatuwezi kusema tatizo hili haliwezi kutokea tena, unajua janga lolote linaweza kutokea ikaleta shida, jambo la msingi ikitokea tunaondoka vipi kurejesha huduma kwa muda mfupi madhara yasiye makubwa,” amesema.

Pia soma
- Nape Nnauye: Tanzania kuwa na Satelaiti yake kama backup ya internet, Mkongo uliokatika kuchukua siku 7 zaidi kutengamaa
 
Kama kuna wapuuzi wa kubwa ndani ya serikali ni huyu jamaa, huyu ilibidi abaki kama team ya propaganda tu katika chama, hakupaswa kuwa ndani ya serikali.
MNACHOMLAUMIA BADO SIKIONI, MBONA AMETOA MWELEKEO MZURI SANA KWA KILE TUNACHOKWENDA KUFANYA KAMA TAIFA, KUWA NA FIXED ALTERNATIVE!, PINGAPINGA ZA CHADOMO BANA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…