Akiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM leo May 15, Waziri wa teknolojia na habari, Nape Nnauye ameongelea changamoto ya Internet nchini na mipango ya kuliepuka janga kama hili siku za baadae. Kuhusu mkongo uliokatika amesema bado una siku si chini ya saba mbele ili kutengemaa.
Nape Nnauye: Bajeti iliyopita tulitangaza bungeni na mchakato ulianza wa Tanzania kuwa na Sattelite yetu kama sehemu ya backup.
Baharini mikongo iko mingi, Serikali ya Rais Samia imeongeza mikongo mfano Rais Samia alilaunch tulitegemea uanze mwezi wa sita lakini kwa hali iliyotokea tunakimbizana kuuwasha sasa hivi.
Mpaka leo saa 10 usiku tulikuwa tumerejesha 78% ya internet, mpaka leo mchana tunatarajia kurejesha asilimia 90+ kama sio mia wakati mikongo iliyopata matatizo baharini wakiendelea kuhangaika nayo kwasababu yenyewe bado hali inaonekana inaweza kuchukua siku nyingi kama saba mpaka tisa.