Nape Nnauye: Tanzania kuwa na Satelaiti yake kama backup ya internet, Mkongo uliokatika kuchukua siku 7 zaidi kutengamaa

Nape Nnauye: Tanzania kuwa na Satelaiti yake kama backup ya internet, Mkongo uliokatika kuchukua siku 7 zaidi kutengamaa

Wewe unadhani satelite au hizo fibre cable za Baharini ni kama taa za kuongoza barabarani,
Suala la satellite mbona ni la muda mrefu,ni vile tu hamfuatilii mambo ya maana,tutarusha satellite kupitia dit,mipango ya muda na nadhani imekaribia
 
Akiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM leo May 15, Waziri wa teknolojia na habari, Nape Nnauye ameongelea changamoto ya Internet nchini na mipango ya kuliepuka janga kama hili siku za baadae. Kuhusu mkongo uliokatika amesema bado una siku si chini ya saba mbele ili kutengemaa lakini mpaka leo zaidi ya 70% ya internet imerejea kwa vyanzo mbadala.

=====

Nape Nnauye: Bajeti iliyopita tulitangaza bungeni na mchakato ulianza wa Tanzania kuwa na Sattelite yetu kama sehemu ya backup.

Baharini mikongo iko mingi, Serikali ya Rais Samia imeongeza mikongo mfano Rais Samia alilaunch tulitegemea uanze mwezi wa sita lakini kwa hali iliyotokea tunakimbizana kuuwasha sasa hivi.

Mpaka leo saa 10 usiku tulikuwa tumerejesha 78% ya internet, mpaka leo mchana tunatarajia kurejesha asilimia 90+ kama sio mia wakati mikongo iliyopata matatizo baharini wakiendelea kuhangaika nayo kwasababu yenyewe bado hali inaonekana inaweza kuchukua siku nyingi kama saba mpaka tisa.
Unaambiwa tangu juzi Nape alikua baharini anaangaika
 
Eti form four failure ndo anakuwa waziri wa teknologia hivi CCM wahisi China ipo pale kwa bahati?
Vipi Kuhusu form six division zero Mbowe kuwa mwenyekiti wa Chadema taifa akiongoza wasomi akina Tundu Lisu na akina Profesa Rwaitama hapo vipi?
 
Hiyo Satellite 🛰 ya Chama itarushwa kutokea Dodoma wakati Wagogo hawana Maji.
Screenshot_20240508-102147.png

Huyu jamaa angeacha bata atage tungekuwa tumisahau kitambo
 
Back
Top Bottom