Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge Nape Nnauye amesema; "Tulikodi uwanja wiki nzima ili Chadema wasifanye kampeni, Kikwete akatuzuia" kupitia mahojiano yake na M&SPodcast inayongozwa na Omar Kashera pamoja na Salma Dacotha
“Nakumbuka siku moja tumezindua Kampeni pale jangwani, Tumeanza sisi kuzindua tumejaza uwanja vizuri alafu siku chache baadae wanakuja kuzindua Chadema wakiongozwa na Lowasa kama Mgombea wao.
Mimi, January Makamba, Ruge Mutahaba tukakodi uwanja ili Chadema wasizindulie pale waende sehemu nyingine, tukasema tutapiga mziki wiki nzima ili tu wasizindulie pale. Tulisema hawa wakija watatengeneza utaratibu wajaze kuliko sisi na ili tuzuie kipimo hicho tukakodi uwanja.
Mkuu wa Mkoa alikuwa anaitwa Mecky Sadick, Chadema walipitapita huko wakalalmika Mzee Kikwete akasema achieni uwanja, tukasema Mzee sisi tumelipia kila kitu hatuwezi kuachia uwanja. Tukaanza kubishana, Mzee akasema hapana Achieni Uwanja.
Ulikuwa ugomvi mbaya kidogo nakumbuka alimwambia mzee Kinana akatuita mpaka nikasema maneno nikamwambia “Mzee kama vile Mnataka kumuachia Nchi Rafiki yenu” akasema hapana nape waachieni wafanye Mkutano.
Mzee Kikwete akasema kama kuna Cost zozote mlizoingia mimi nitawarudishieni waachieni Chadema wafanye mkutano. Kama kuna ustaarabu wa ajabu this was Maximum.
Mkutano ulikuwa mkubwa sana, kilichosumbua ni kwamba Mgombea wao akaongea chini ya Dakika Tano kwahiyo usiku mzee akaniambia Nape mmeona sasa mlitaka kuzuia watu wasijue uwezo wa mgombea.”