Nape Nnauye: "Tunakamilisha mchakato wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi"

Nape Nnauye: "Tunakamilisha mchakato wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi"

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia amethibitisha kuwa Serikali inakamilisha mchakato wa utungwaji wa Sheria hiyo itakayolinda taarifa binafsi za watu.

Kauli ya Nape inakuja wakati kukiwa na madai mengi ya sheria hiyo kutoka kwa watu binafsi na taasisi ikiwemo JamiiForums ambayo imekuwa ikisisitiza umuhimu wa Sheria hiyo kutokana na ukusanyaji, uchakataji na utumiaji holela wa taarifa binafsi bila kuwa na ulinzi.

Amesema "Tumeshuhudia hapa nchini mtu anaingilia privacy ya mtu anachukua taarifa anaziweka hadharani, ndani ya miezi michache tutatunga sheria ambayo itaeleza nani anakusanya taarifa gani, anaziweka wapi, anazichakata vipi anazitumiaje na nani anawajibika".

Mkurugenzi wa JamiiForums akiongea na East Africa Radio alithibitisha kuwa wamepeleka pendekezo la Muswada ambao unaishauri Serikali juu ya umuhimu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
 
Hizi ni habari njema sana siku hizi information zenu zinauzwa kwa third party bila ya ninyi kujua zimekuwa big bussines.
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia amethibitisha kuwa Serikali inakamilisha mchakato wa utungwaji wa Sheria hiyo itakayolinda taarifa binafsi za watu...
Hatari iko hapa, nani anazikisanya anazihifadhi wapi na anazipeleka wapi?? Na nani anastahili kuzipata akiziitaji, hapo ndo jamii forum inakwenda kupigwa na kitu kizito kichwani, kwa nchi hii usije omba na kushangilia kuwa kuna manufaa ya sheria kama hizo kwa mtu mmojammoja zaidi ya faida kwa serikali
 
Hio sheria ita deal na wanaosema waziri fulani ameingiza mabasi 60 😂😂😂
 
Hii sheria kama itakuja isitumike kijanja kuweka exception kwa serikali.

Serikali wasije wakasema kwenye hiyo sheria mpya wana haki ya kutafuta/kuomba taarifa za yeyote "anayehatarisha amani ya nchi", kumbe wanamuwinda yule anayewakosoa mitandaoni ili wamfunge mdomo.

Nawataka hao wadau wanaoshauri uwepo wa hiyo sheria, JF ikiwemo, wawe makini sana na vifungu vya hiyo sheria. Inaweza ikaja sheria ya kuwabana watu binafsi pekee lakini isiwabane serikali.

Wadau hasa JF wasipokuwa makini kwenye hili, wanaweza kujikuta zile safari za kwenda mahakamani zinaendelea kuwepo licha ya hiyo sheria kutungwa na kutufanya wanachama tuendelee kuishi kwa hofu mitandaoni.

Muhimu wahakikishe hiyo sheria inakuwa active kwa pande zote mbili, serikali na watu binafsi, hapo ndipo itakamilika ile maana ya ule msemo wa sheria ni msumeno.
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema Tanzania imepewa kibali cha kutunga sheria ya kulinda taarifa binafsi za watumiaji mitandao na usalama wake.
 
Back
Top Bottom