Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Huo ni ujumbe wa Mheshimiwa Nape Moses Nnauye Katibu Mwenezi wa CCM Mstaafu aliyeongoza Kampeni maarufu ya kujivua Gamba Ndani ya CCM ili Wale walioitwa Mafisadi na waliokichafua chama na kujipunguzia imani na kuaminika kwa watanzania hususan vijana waweze kuwajibishwa na kuwajibika.
Ni katibu Mwenezi ambaye alipita maeneo mbalimbali ya Tanzania Hususani vijijini katika kukijenga chama chetu cha Mapinduzi. Ndio Maana huwa anasema kuwa alilala Maporini kukipigania chama.
Mheshimiwa Nape Moses Nnauye ambaye pia ni Waziri wa habari mstaafu na mtoto wa Brigedia Moses Nnauye amesema ya kuwa siyo kila sehemu akili yako Itakusaidia Bali kuna wakati Hata ujinga unaweza kuwa Msaada.
Je wanajukwaa mnafikiri nini amemaanisha Mheshimiwa Mbunge ambaye alikuwa Machachari kwelikweli Enzi za Uenezi wake katika kilele cha upinzani Mkubwa hapa Nchini uliokuwa umechagizwa na vuguvugu na harakati za vijana wengi wa vyuo Vikuu Hususani chuo kikuu cha Dar es salaam Maarufu Kama UdSM.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.