Nape: Ukusanyaji wa kodi ni taaluma ila Serikali imeacha kutumia wenye taaluma inatumia task force ambao kazi yao ni kuua biashara tu

Nape: Ukusanyaji wa kodi ni taaluma ila Serikali imeacha kutumia wenye taaluma inatumia task force ambao kazi yao ni kuua biashara tu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema kuna changamoto kubwa ya biashara nyingi kufungwa na hili ni kutokana na Serikali kutotumia Wanataaluma katika kukusanya kodi.

Mafanikio yanayofurahiwa sasa kwenye mapato ni ya muda mfupi lakini itafika wakati hakutakuwa na cha kukusanya. Asema baadhi ya Wafanyabiashara wanatishwa kwa mashtaka ya Uhujumu #Uchumi hivyo huamua kufunga biashara.

 
Ukishaharibu mfumo kwa jumla namna bora ya kutoka salama ni kutoongeza muda ili athari ya makosa yako akutane nayo mwenzie

Nyerere alipogundua kila kitu kinakufa akaona hakuna tena Mwanga kama hadi sabuni huwezi kupata mpaka ukimbizane na magari ya 'ugawaji' wiki nzima 'akang'atuka' akijua Gari linaenda halijojo,

Mzee Mwinyi akaingia na kufanya yasiyotegemewa, miaka ya mwanzo Nyerere akapiga Kimya akidhan mikakati ile isingefanikiwa…gari lilipochomolewa kwny tope likarudi kwny lami akaanza kelele zake z kusema Rushwa imetamalaki mara sijui Rais anashauriwa na Mkewe wakati maamuzi yote ya Nchi yanapitishwa kwny Cabinet na Minutes zilikuwepo

Athari ya kiuchumi na kikodi na lawama zake atabebeshwa Rais ajae kwa kuwa ndio ule ugumu na athari zitakuwa wazi mno
 
Kodi inatakiwa ukusanye kwa Nguvu wabongo hawaendi kwa barua utamaliza Rimu ya barua na hakuna kodi kubwa kodi nyingi ni adhabu watu wana default sheria za kodi
 
Back
Top Bottom