Nape: Ukusanyaji wa kodi ni taaluma ila Serikali imeacha kutumia wenye taaluma inatumia task force ambao kazi yao ni kuua biashara tu

Nape: Ukusanyaji wa kodi ni taaluma ila Serikali imeacha kutumia wenye taaluma inatumia task force ambao kazi yao ni kuua biashara tu

Nape hana wasiwasi anajua mwenye mamlaka anaelekea mwishoni
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema kuna changamoto kubwa ya biashara nyingi kufungwa na hili ni kutokana na Serikali kutotumia Wanataaluma katika kukusanya kodi.

Mafanikio yanayofurahiwa sasa kwenye mapato ni ya muda mfupi lakini itafika wakati hakutakuwa na cha kukusanya. Asema baadhi ya Wafanyabiashara wanatishwa kwa mashtaka ya Uhujumu #Uchumi hivyo huamua kufunga biashara.

 
Kodi inatakiwa ukusanye kwa Nguvu wabongo hawaendi kwa barua utamaliza Rimu ya barua na hakuna kodi kubwa kodi nyingi ni adhabu watu wana default sheria za kodi

Hapa hatuongelei kukusanya kodi kwa mujibu wa sheria, bali tunazungumzia kukusanya kodi kwa kukomoa.
 
N
Nape Bado anadukuduku hata msamaha alioomba ni kupisha shari
Nape sio ndege wala sio mnyama, huku ataka na kule ataka hivyo anauma na kupuliza hivyo mpaka siku watakapogundua itakuwa too late....Anazar Malema?
 
Kadri siku zinavyoenda hawaogopi tena maana wanajua ni muhula wake wa mwisho tena huenda bunge kwa sasa likambadilikia hamuwezi amini itafika kipindi watu wataanza kusifia bunge

Tusifie bunge la wezi wa kura, maisha yao hilo wasahau.
 
Kaa kimyaa utumie hizo barabara na Dawa hospitalini usiulize zinakotoka

Dawa zipi, au unadhani kwakuwa watu wamekaa kimya kwa kuogopa kutekwa ama kuuwawa ndio hawajui kuwa hospitali hazina dawa?
 
Hata guta hatujapata, tumepata baskel ya miti
Nibora hata hiyo baskeli ya miti tungejua tumepata chichote kitu! Zikeishia saundi tu ukijifanya unahoji sana wanakutafutia janga la kukupa
 
Malalamiko mengi yametokana na utendaji uliojaa extremism.
Moderation inahitajika katika utendaji wa siku kwa siku serikalini.
Ni makosa makubwa kuchagua au kuteua watu wenye msimamo mkali kuongoza.
Vitabu vitakatifu na hata busara tu ya kawaida vinatuelekeza tuwe na kiasi.
 
Nape bado ana hasira ila ngoja watampetipeti mpaka asahau
 
Mtasema yote awamu hii,maana wapinzani hawapo, maccm yanatengeneza kiki.
 
Back
Top Bottom