Nape: Ukusanyaji wa kodi ni taaluma ila Serikali imeacha kutumia wenye taaluma inatumia task force ambao kazi yao ni kuua biashara tu

Nape: Ukusanyaji wa kodi ni taaluma ila Serikali imeacha kutumia wenye taaluma inatumia task force ambao kazi yao ni kuua biashara tu

Bwana yule hajali pesa imepatikanaje, yeye anataka tu kusikia Kapu limejaa afurahie.
 
Kodi inatakiwa ukusanye kwa Nguvu wabongo hawaendi kwa barua utamaliza Rimu ya barua na hakuna kodi kubwa kodi nyingi ni adhabu watu wana default sheria za kodi
Kama walivyofanyiwa Ramadhan Ntuzwe, St Jude.....kwako hiyo ni sawa kabisa, kwako bora pesa ipatikane tu.
 
Vichekesho sana.....wanalalama lakini mwishoni kabisa...'naunga mkono hoja kwa asimia miyaa"

Kichefuchefu tu
 
Jamani msisikie mtaani kuna njaa kali..machinga anakaa hadi siku tano hajauza hata pair moja ya soksi au kiwembe

Je unaweza kuvuna mahindi kwenye mabua? Hii serikali inafikiri inaweza kukusanya kodi hata wafanya biashara wakifunga biashara zao! Huo ni ujinga.
 
Swali la kujiuliza hivi wakusanya kodi wanakusanya kwa kutumia nini si sheria ndiyo wanayotumia na wanaotunga hizo sheria ni kina nani?Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Ukisoma sheria zinazosimamiwa na watoza kodi kila kitu kipo wazi wao kazi yao ni kufata sheria ilivyosema ndiyo maana wakienda nje ya utaratibu au matakwa ya sheria wanashitakiwa.
Sheria ambayo haiendani na matakwa ya biashara ndugu yangu,

yaani inauwa biashara, acha kutetea mambo kwenye angle ndogo hivyo....
Hivi mtu ana duka lenye thamani let say ya mil 12, akijisahau kwa lolote asipotoa risit ya 500 unampiga fine ya 4.5M... na ni kwa lazima..
Mfano mwingine, unakuta mfanyabiashara umeweka hela bank, changanya na mkopo, bank wanakwambia mamlaka inataka kuelewa mapato yako.... yani mradi tu usumbufu mwanzo mwisho...
Kumbe analosema Kosomea ni pamoja na kuelewa money flow, just follow the money, mtu wanatoa hela bank anarudisha kwenye biashara au anajenga au anafungua biashara nyingine shida ipo wap, na yupo registered kama business man..
Usumbufu unaosababishwa na short sighted operator unakwamisha mambo mengi sana mzee wa kaz
 
Nape ana akili nzuri, suala la kodi ni very sensitive kwa uhai wa serikali na wafanya biashara.. So task force itaua biashara na wafanya biashara wakifilisika serikali itakosa mapato mengi
 
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema kuna changamoto kubwa ya biashara nyingi kufungwa na hili ni kutokana na Serikali kutotumia Wanataaluma katika kukusanya kodi.

Mafanikio yanayofurahiwa sasa kwenye mapato ni ya muda mfupi lakini itafika wakati hakutakuwa na cha kukusanya. Asema baadhi ya Wafanyabiashara wanatishwa kwa mashtaka ya Uhujumu #Uchumi hivyo huamua kufunga biashara.

Kinachofanyika sasa ni ujambazi wa kidola na huenda viongozi wana historia ya ujambazi
 
Haya tusubiri kuona kama bwana atafurahishwa na haya. TAL alishasema haya kitambo na watu hawahawa wakamubishia. Sasa wanakiri kuwa TRA inatafuna biashara.
Kwani task force ndio TRA... Kwa sasa kodi inakusanywa na taasisi nyingi, nafikiri ndizo zilizomaanishwa hapo
 
Kodi inatakiwa ukusanye kwa Nguvu wabongo hawaendi kwa barua utamaliza Rimu ya barua na hakuna kodi kubwa kodi nyingi ni adhabu watu wana default sheria za kodi
Saa nyingine muwe mnakaa kimya mkiona watu wanaongea mambo ya msingi
 
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema kuna changamoto kubwa ya biashara nyingi kufungwa na hili ni kutokana na Serikali kutotumia Wanataaluma katika kukusanya kodi.

Mafanikio yanayofurahiwa sasa kwenye mapato ni ya muda mfupi lakini itafika wakati hakutakuwa na cha kukusanya. Asema baadhi ya Wafanyabiashara wanatishwa kwa mashtaka ya Uhujumu #Uchumi hivyo huamua kufunga biashara.

Safi.Tuambie aliyekutolea bastola alitumwa na nani?
 
Ila nasikia hii Task Force ndiyo imewaweka madarakani nyinyi wabunge na serikali.
Hivyo usiache mbachao kwa msala upitao.
 
Back
Top Bottom