Nape: Wema ametupa heshima kubwa, tutamuweka kwenye rekodi zetu

Nape: Wema ametupa heshima kubwa, tutamuweka kwenye rekodi zetu

WAZIRI NAPE AZINDUA MFUMO WA KISASA WA WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari, katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.Picha na Geofrey Adroph(Pamoja Blog)


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akizungumza kabla ya kuzindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.


Msanii wa Bongo Movie na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Maadam Wema Sepetu akizunguma mbele ya waandishi wa habari katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar kabla ya kuzindua huduma yake WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION,ambayo itakuwa ikijumuisa matukio yake yote sambamba na video mbalimbali yatakayowekwa kwenye mfumo wa teknolojia ya kisasa kupitia simu za mikononi.

Mtaalamu wa huduma za mitandao kutoka Push Mobile, Haji Yussuph akifafanua jambo kuhusiana na huduma hiyo ya WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION

Meneja wa Biashara wa Hartmann Trader ambao ndio watoa huduma ya Wema Sepetu Mobile Application,Cecil Mhina akifafanua namna huduma hiyo inavyoweza kutumika na pia maelezo kadhaa namna ya kujinga na kupata taarifa mbalimbali na video kupitia huduma hiyo

Munalove(kushoto) akimwelekeza mama mzazi wa Wema Sepetu jinsi ya kujiunga na WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mara bada ya kufanyika kwa uzinduzi huo

Msaniii wa Bongo Movie, Wema Sepetu akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye baada ya uzinduzi wa huduma hiyo kufanyika mbele ya waandishi wa habari, katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini

Msanii wa Bongo Movie na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Maadam Wema Sepetu akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wake wa huduma ya WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION

Wema Sepetu akiwa amemkumbatia mama yake mzazi mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.

Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi
Mfumo wa kisasa kabisa??? U must be joking
 
Nyota inang'aa sana huyo Dada.wenye wivu mtapata shida sana
 
Inabidi huyu waziri aende Kenya aone vijana wanavyo develop app zenye kuleta faida kwenye jamii si huu ujinga.
 
Mi naona wema mwenyewe Kafanya juhudi binafsi za kuandaa hilo tukio na pia katumia ubunifu kumualika waziri.Hao vijana unaosema je wameshafanya hivyo na waziri akakataa kuhudhuria huo uzinduzi?
Watu wanaodevelop app za maana hawaitaji hizo show za kijinga they know what they are doing.
 
Watanzani tuacheni wivu wa kijinga mwenzenu keshafanya yake anategemea kupiga hela nyie mnabaki kulialia tu fanyeni ubunifu umizeni vichwa muone kama hamtatusua,mwenzenu kila kukicha anawaza jinsi ya kubaki kuwa madam wema asiechuja aweze kuyamudu maisha ya mujini nyie ni kuponda tu shauri yenu muda haumngoji mtu.Wema nakupa big up sana kwa juhudi zako pamoja na ubunifu wako songa mbele mama.
Ubunifu gani?? Kuuza sura tu.
 
Hii nchi ina vituko sana.

Waziri anakataa kuhudhuria VIKAO VYA BUNGE, anaenda KUHUDHURIA halfa ya WEMA SEPETU kuzindua application yake ya kupost ishu zake za UDAKU kwa mashabiki wake.

Halafu anatoa PUBLIC ANNOUNCEMENT, eti nimeahirisha kuhudhuria kikao BUNGENI ili nije KUZINDUA application yenu.

MAGUFULI kweli UNA KAZI mwaka huu.
 
Swali la kujiuliza...ni eneo lipi nikikaa nitajulikana na kuonekana?
 
PHD hebu tabiri basi kuhusu huyu mbunge wa mtama anaondolewa lini mjengoni ? Au Kama Vipi namimi ngoja nijaribu....atafuta huyu kuwa evicted maana hajui asemalo wala atendalo uelekeo wake kuwa out Ni mkubwa Sana
 
Mtabaki kusema sijui Kenya sijui huku ulaya aah wapi mwenzenu keshatusua anabaki kua expensive wkt nyie hata mtaa hamjulikani shame on you
 
[emoji23][emoji23][emoji23] hii nchi unaweza ukajuta kuwa MTanzania mana duh
 
Huyu waziri anaweza kutumbuliwa kwa mambo kama haya anaacha Bunge anakuja kuzindua mambo binafsi ya Mtu? Magu atavifungia vitu kama hivi soon... Watanzania tunataka maendeleo na sio kuchezea simu kusoma Wema amefanya nini leo kesho blah blah tele... Siamini kama waziri amechagua wema badala ya kikao cha Bunge...
 
Back
Top Bottom