Napenda kufahamu juu ya hawa mbuzi

Joined
Nov 13, 2018
Posts
20
Reaction score
5
Habari wakuu.

Katika harakati za kupata maarifa mapya mtandaoni nilikutana na hawa mbuzi (picha chini) maelezo niliyosoma kuwahusu ni kuwa;

hawa ni mbizi wa nyama wanao uwezo mkubwa wa kupata uzito hadi kufikia kg 150 kwa dume. Pia jike lake hufika hadi kg 120 na huzaa mapacha.

Maelezo yanasema kuwa hawa mbuzi licha ya kuwa na miili mikubwa na pembe ni wapole. Na ni mbuzi wanaofaa sana kwa ufigaji wa mbuzi wa nyama.

Kwa bahati mbaya niliposoma habari ya kuwahusu mbuzi hawa hapakuwa na taarifa nilizoitaji kuzifahamu kuwahusu, sasa naleta kwenu wandugu kwa anayewafahamu anijuze haya yafuatayo:-

1. Wanapatikana wapi kwa hapa Tz

2. Wanachukua muda gani kuwakuza

3. Gharama za matunzo yao kwa wastani wa mbuzi 3. (Dume 1, jike 2)

4. Changamoto na ufugaji wake kwa jumla

Nimeambatanisha na picha zao

Natanguliza shukrani wakuu.
 
Niliwaona kwa wingi nane nane ya mwaka huu arusha
 
Ndio walishazaliana na sasa wanauzwa bei ni 150,000 kwa mtoto na wakubwa ni kuanzia 450,000. Wapo sana siha, mwanga, karatu. Wanazaa mapacha (guaranteed). Nitakutumia mawasiliano ya washiriki /wafugaji
Duh!.kuzaa mapacha ni guarantee? Au ni mbuzi wa gmo?
 
Ndio walishazaliana na sasa wanauzwa bei ni 150,000 kwa mtoto na wakubwa ni kuanzia 450,000. Wapo sana siha, mwanga, karatu. Wanazaa mapacha (guaranteed). Nitakutumia mawasiliano ya washiriki /wafugaji
Yale yale bei za sungura. Mfugaji anauziwa bei mara 10 ya bei yenyewe ya sungura kisa anamanyoya mengi
 
Ndio walishazaliana na sasa wanauzwa bei ni 150,000 kwa mtoto na wakubwa ni kuanzia 450,000. Wapo sana siha, mwanga, karatu. Wanazaa mapacha (guaranteed). Nitakutumia mawasiliano ya washiriki /wafugaji

Shukrani sana ndugu. Nitafurahi nikipata mawasiliano yao.
 
Kuna jamaa alileta picha na watu wakanunua picha, shauri yako
 
Hao mbuzi si WANGU niliwakuta maonesho ya 8-8 kaskazini 2018.
wenye mbuzi sifahamiani nao niliweza tu kuchukua mawasiliano yao
Nimekuelewa sana, ila kuna mtu alikuwa anawatangaza kitambo kuwa anao na anauza, lakini alikuwa tapeli tu

Hawa mbuzi wanaitwa Boer means farmer
Na walipandikizwa miaka ya nyuma huko South Africa na sasa wanapatikana duniani kote hata Pakistan mpaka India na USA wapo.

Ni mbuzi wakubwa haswa na ni kwa ajili ya nyama.
Nilitamani kupata mbegu hiyo lakini nikagonga mwamba.
Tuwekee mawasiliano yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…