Napenda kufanya biashara ila sijapata muuzaji mwaminifu

Ww kama mkubwa wake yakupasa umfundishe adabu. Timua huko aliko kwa baba mwambie atafute kazi afanye sio anakaa tu anabweteka. Kumbuka saizi anadeka kwa baba akitoka hapo atakuja kudeka kwako. Shauri yako mtakuja nuniana kwa mbeleni msipo ziba ufa.
Mungu ni mkubwa siku baba akiaga dunia atateseka kama hajapata kazi.
Itabidi mzigo niubebe mimi.
 
Mkuu hayo mawazo tayari nilishawahi kufikiria, nipo na mdogo wangu wa kuzaliwa ila hataki kabisa shida ye anataka akae kwenye kiti azunguke kama boss.
Baba aliwahi kumpatia nafasi ya kwenda JKT aliamua kurudi hata mafunzo hayajaanza.
Kwa ufupi ni mvivu wa kutupwa lakini angefaidi matunda yangu.
Tafuta kijana saini nae mkataba maana watu mkielewana kwa mdomo hakuna mbaya aisee ila ukikaza kabisa utafanikiwa
 
Sina uwezo wa kumfukuza maana anakaa baba sio kwangu Ba istoshe kitu kibaya zaidi kaowa juzi hana hata kazi za kufanya analishwa nyumbani huku nikitegemewa na mimi nnachotuma ndo aunganishie hapo hapo.
Ila kuna siku nilishakataa tangia siku aliyotafuta sababu ya kurudi JKT hadi leo sina ham nae.
Namsaidia kwasababu dam ni mzito kuliko maji lakini yamenifika shingoni maana anajua kunipangia matumizi ya pesa zangu ila yeye kazi hataki.
Aisee pole sana una mtihani mzito sana mbeleni. Yaani mtu ameoa alafu hana kazi kisha anategemea kupewa hela ya matumizi kama yy ndio ameolewa.!!! Fanya hiv muite kaa nae uongea nae kwa upole na upendo kisha mshirikishe hiyo ishu muelekeze kwa upole mpaka aelewe. Mkuu msaidie ndugu yako acha kulemaa wakati ndunguyo anapotea. Kaa nae mfunze kazi mwambie maisha ni hiv wala sio hivyo utakavyo ww.
 
nimependa spirit yako, ushauri wangu anzisha biashara usimame nayo mwenyewe peke yako kwanza ikishakuwa stable ajiri kijana.
 
Kwahiyo na ww umetulia tu na umelidhika badala ya kumsaidia ndugu yako.
Mkuu wewe mzazi wako akisema hapana wewe unasema ndio?
Mimi nilishamsaidia ila hakuna msaada wangu.
Nilimbembeleza abakie JKT wenzake tayari wameshaajiriwa kwa mfano ungekua wewe ungemsaidiaje wakati njia rahisi ya kupata kazi alikua nayo.
Kwa ufupi mkuu anaringia uwepo wa baba.
Ungekua unamfaham hata wewe ungesema baba ndo anamuharibu.
Mimi sikulelewa hivyo, nilijua mapema sina bahati kwa mzee zaidi yake ndo maana nikang'ang'ana kuumia mpaka nimeona matunda.
 
Hiyo biashara ya kukopesha na vyuma hivi mzee ni kutafuta lawama tu ..ushauri wangu tafuta likizo ndefu ya siku 28 ufungue biashara na uisimamie mwenyewe japo kwa mwezi mmoja uone mwelekeo wake.. muda huo utakua karibu na kijana na kumsimamia na kumpa maelekezo.. ktk kipindi hicho utapata hata picha ya faida ya biashara yako! note: hii ni applicable kwa biashara ndogo kama ya chakula e.g. chips.. ukipata eneo ambalo itakua rahisi kwako kupita kila siku urudipo kazini itakusaidia sana maana kijana wa kazi ataongeza umakini.. ila all in all biashara inahitaji kusimamiwa na mwenyewe otherwise changamoto haziepukiki
 
Ila biashara ya vitenge mmmh
Labda kama una network ya watu maofisini siyo huku mtaani.
 
Kwanza nikupongeze kwa jitihadazako na kwa moyo wako wakusaidiana, mkuu niruhusu nikufuate pm.
 
Huko ukichukua vile vya elfu 24 Moro wanakopesha 45 kwa mwezi.
Vingine vya bei ya juu sijajua maana nataka nianzie hapo kwanza.
Wazo lako ni zuri lakini kiuhalisia utapata hasara!...kwa mtaji wa laki5 huwezi kufanya biashara ya vitenge kutoka kigoma kwa kumtuma mtu asiyekuwa na uzoefu,tena umgharamie chakula na malazi aende kufuata pea 10 za vitenge then ukopeshe uanze kudai!!!!...utaishia kujuta kumbe tatizo ni mipango!

Kwa bei ulizozitaja unaoneka hujafanya utafiti wowote kuhusu biashara ya vitenge kwenye mikoa ya karibu...mfano Dar...Dom..vitenge vya wax pc3 bei za jumla ni 20000-22000,sasa kwann uende kigoma kwa mtaji wa laki5!?tena unatuma mtu badae ukopeshe!

Hujasema unafanya kazi gani lakini
Ushauri wangu:
Kwa mtaji ulionao unafaa ufanye biashara ya nafaka:uza mchele bei za jumla maeneo ya uswahilini,tafuta watu wawili committed wenye maduka au vibanda vya mtaani msaini mkataba uwe supplier wao, laki5 unaeza kuanza na gunia 2(kg200)ukipata Faida ya 150-200 kwenye kg1 si chini ya 30000kwa wiki×4=120,000.
Ukitoa gharama za bodaboda wa kupeleka mzigo madukani na dharura hata ukipata elfu80 kwa mwezi, hii ni sawa na mifuko mitano ya cement!!

Au vinginevyo tafta eneo dogo la wazi isiwe mbali sana na makazi yako..(unaeza ukakodi) lima mbogamboga za fasta (mchicha,chinese,pilipili)anzisha kilimo cha umwagiliaji then mweke kijana (cheap labor)asimamie uzalishaji alafu mwingine asimamie mauzo nyakati za asubuhi na jion(hakikisha ni mtu wa karibu na mwaminifu)usipotoka Nenda katubu!
 
Doh hela ya mikono mingi sio yako...biashara ni ya alie golini sio yako. Mara 100 ufanye biashara ya kukppesha uletewe chako na riba
 
Mkuu hayo mawazo tayari nilishawahi kufikiria, nipo na mdogo wangu wa kuzaliwa ila hataki kabisa shida ye anataka akae kwenye kiti azunguke kama boss.
Baba aliwahi kumpatia nafasi ya kwenda JKT aliamua kurudi hata mafunzo hayajaanza.
Kwa ufupi ni mvivu wa kutupwa lakini angefaidi matunda yangu.
[emoji121]
HUYO MDOGO WAKO MVIVU
KAMA NI WA KIKE NI_PM NAMBA YAKE YA SIMU FASTA ILI NIZUNGUMZE NAYE VEMA NA KUMJENGEA ARI YA KUJITUMA KATIKA MAISHA!!!

FASTA MKUU.
 
Chakukushauri, tafuta muda uende kigoma pale mwanga sokoni ukatengeneze connection na mfanyabiasha wa vitenge, watu wa pale ni waaminifu sana mie niliwahi kumsaidia sister kufanya biashara hii au kama vp Njoo inbox nikusaidie kupata mtu mwaminifu kigoma atakusaidia
 
Wakuu habari za majukumu ya kutwa mzima.

Mimi ni kijana wa kiume (31) nina ham ya kutaka kufanya biashara lakini kila ninae muamini na kumuachia mtaji anakula mazima yaani mpaka nashindwa kumuamini tena mtu yeyote hata kama hana nia mbaya na mimi.

* Wa kwanza tulikubaliana biashara fulani nikampa mtaji wa laki 4 lakini hadi leo sikuona mtaji wala faida.

* Wa pili na yeye nilimpa laki 5 na yeye hadi leo sikuona faida wala mtaji.

* Wa tatu na yeye nilimpa laki 3 lakini alijiongezea yeye kwenye biashara zake yeye nilimbana akarudisha pesa zangu.

Sasa hapa nilipo nimekaa nawaza tena nianzishe biashara lakini kuna mdau mmoja alinambia ni bora utoe vitenge Kigoma na kuleta Dar aidha kwa cash au mkopo.
Iwapo kama wateja watakua waaminifu ( wa mkopo).

Ila changamoto iliyopo ni kukosa mtu mwaminifu wa kutoa kule na kuleta sehemu husika.
Napenda kusaidia mtu kwa njia kama kama hiyo ili na yeye apate chochote lakini watu wa sasa hawafadhiliki.

Hapa nilikua nataka nitoe fursa ya shilingi laki 5 ya kuanzia lakini ndo mpaka sasa naumiza kichwa nani nimpe afanye hiyo biashara.
Kazi yake aende akavichukuwe na kuja navyo Dar.
Kama hana wenyeji atakua analala guest gharama juu yangu ilimradi vyuma vilegee.

Sasa wakuu nimeona nije hapa nipate ushauri wowote kwenu maana hapa pana watu wana maoni ya mbali kuliko hata mitaani.
Na pia najua kuna watu watabeza ila mnaruhusiwa ila siruhusu matusi tu......karibuni.
nimekuchek pm
 
kama hutojali mkuu nipm tuongee vizur
 
Mkuu hapa umetangaza kazi kwa vijana sipati picha huko PM , ,
 
Habari za muda huu.
Nipende kukupa hongera na pia nikusifu kuwa hiyo ndio njia sahihi ya kufanya biashara na kutoa ajira kihalali.
Nikuombe usikate tamaa hata humu wapo wenye uhitaji na waaminifu na unaweza kumpata.
Niwaombe watanzania wenzangu tuwe waaminifu na wenye kujituma ndio njia pekee ya kufanikiwa.
 
Back
Top Bottom