Powder
JF-Expert Member
- Jan 6, 2016
- 4,977
- 6,635
Mkuu!Wakuu habari za majukumu ya kutwa mzima.
Mimi ni kijana wa kiume (31) nina ham ya kutaka kufanya biashara lakini kila ninae muamini na kumuachia mtaji anakula mazima yaani mpaka nashindwa kumuamini tena mtu yeyote hata kama hana nia mbaya na mimi.
* Wa kwanza tulikubaliana biashara fulani nikampa mtaji wa laki 4 lakini hadi leo sikuona mtaji wala faida.
* Wa pili na yeye nilimpa laki 5 na yeye hadi leo sikuona faida wala mtaji.
* Wa tatu na yeye nilimpa laki 3 lakini alijiongezea yeye kwenye biashara zake yeye nilimbana akarudisha pesa zangu.
Sasa hapa nilipo nimekaa nawaza tena nianzishe biashara lakini kuna mdau mmoja alinambia ni bora utoe vitenge Kigoma na kuleta Dar aidha kwa cash au mkopo.
Iwapo kama wateja watakua waaminifu ( wa mkopo).
Ila changamoto iliyopo ni kukosa mtu mwaminifu wa kutoa kule na kuleta sehemu husika.
Napenda kusaidia mtu kwa njia kama kama hiyo ili na yeye apate chochote lakini watu wa sasa hawafadhiliki.
Hapa nilikua nataka nitoe fursa ya shilingi laki 5 ya kuanzia lakini ndo mpaka sasa naumiza kichwa nani nimpe afanye hiyo biashara.
Kazi yake aende akavichukuwe na kuja navyo Dar.
Kama hana wenyeji atakua analala guest gharama juu yangu ilimradi vyuma vilegee.
Sasa wakuu nimeona nije hapa nipate ushauri wowote kwenu maana hapa pana watu wana maoni ya mbali kuliko hata mitaani.
Na pia najua kuna watu watabeza ila mnaruhusiwa ila siruhusu matusi tu......karibuni.
Achana na hizo habari za kumpa mtu 500,000 sijui 1,000,000....
Weeki ijayo Mwishoni nashusha Vitenge vya Wax Original kama Piece 300 hapo Dar!
Vitenge ni kutoka Congo, Burundi na Nigeria...
Bei ya jumla ni 25,000, ukichukua zaidi ya 10 pieces bei 20,000, sitaki faida kubwa coz navitoa jikoni!
Jumla naanza kuuza kuanzia 10 Pieces....
Kama upo serious njoo PM!