Napenda kufanya biashara ila sijapata muuzaji mwaminifu

Napenda kufanya biashara ila sijapata muuzaji mwaminifu

Ingia mkataba na mtu au tumia ndugu zako kabisa tena wa ndani kabisa eg mke na hata mdogo wako nawe utafanikiwa, nje ya hapo utateseka sana

Walinifanya hivyo vijana wawili nikamweka mke wangu sasa mambo ni murua japo waliniliza karibu 2.3 milions
Nashukuru moyo umetulia
Ila wadogo wengine nao balaa, utakuta ana vimichepuko kibao siku asipokuwepo sehemu ya biashara vinapanga foleni kuja kumuulizia natamani nitandike makofi.
 
Mkuu hayo mawazo tayari nilishawahi kufikiria, nipo na mdogo wangu wa kuzaliwa ila hataki kabisa shida ye anataka akae kwenye kiti azunguke kama boss.
Baba aliwahi kumpatia nafasi ya kwenda JKT aliamua kurudi hata mafunzo hayajaanza.
Kwa ufupi ni mvivu wa kutupwa lakini angefaidi matunda yangu.
Bora huyo mimi nilikuwa naye alikuwa anajituma sana lakini faida siioni, alikuwa na videmu kibao vinachukua pesa na bidhaa
 
Njoo PM tuyajenge mkuu, me ni kijana muaminifu kabisa, muhimu tuandikishane kisheria ili chochote kikitokea mtu akashitakiwe
 
Wakuu habari za majukumu ya kutwa mzima.

Mimi ni kijana wa kiume (31) nina ham ya kutaka kufanya biashara lakini kila ninae muamini na kumuachia mtaji anakula mazima yaani mpaka nashindwa kumuamini tena mtu yeyote hata kama hana nia mbaya na mimi.

* Wa kwanza tulikubaliana biashara fulani nikampa mtaji wa laki 4 lakini hadi leo sikuona mtaji wala faida.

* Wa pili na yeye nilimpa laki 5 na yeye hadi leo sikuona faida wala mtaji.

* Wa tatu na yeye nilimpa laki 3 lakini alijiongezea yeye kwenye biashara zake yeye nilimbana akarudisha pesa zangu.

Sasa hapa nilipo nimekaa nawaza tena nianzishe biashara lakini kuna mdau mmoja alinambia ni bora utoe vitenge Kigoma na kuleta Dar aidha kwa cash au mkopo.
Iwapo kama wateja watakua waaminifu ( wa mkopo).

Ila changamoto iliyopo ni kukosa mtu mwaminifu wa kutoa kule na kuleta sehemu husika.
Napenda kusaidia mtu kwa njia kama kama hiyo ili na yeye apate chochote lakini watu wa sasa hawafadhiliki.

Hapa nilikua nataka nitoe fursa ya shilingi laki 5 ya kuanzia lakini ndo mpaka sasa naumiza kichwa nani nimpe afanye hiyo biashara.
Kazi yake aende akavichukuwe na kuja navyo Dar.
Kama hana wenyeji atakua analala guest gharama juu yangu ilimradi vyuma vilegee.

Sasa wakuu nimeona nije hapa nipate ushauri wowote kwenu maana hapa pana watu wana maoni ya mbali kuliko hata mitaani.
Na pia najua kuna watu watabeza ila mnaruhusiwa ila siruhusu matusi tu......karibuni.
Mkuu em nifuate pm mi siwez sema ni muaminifu ila njoo pm tu.
 
Wazo lako ni zuri lakini kiuhalisia utapata hasara!...kwa mtaji wa laki5 huwezi kufanya biashara ya vitenge kutoka kigoma kwa kumtuma mtu asiyekuwa na uzoefu,tena umgharamie chakula na malazi aende kufuata pea 10 za vitenge then ukopeshe uanze kudai!!!!...utaishia kujuta kumbe tatizo ni mipango!

Kwa bei ulizozitaja unaoneka hujafanya utafiti wowote kuhusu biashara ya vitenge kwenye mikoa ya karibu...mfano Dar...Dom..vitenge vya wax pc3 bei za jumla ni 20000-22000,sasa kwann uende kigoma kwa mtaji wa laki5!?tena unatuma mtu badae ukopeshe!

Hujasema unafanya kazi gani lakini
Ushauri wangu:
Kwa mtaji ulionao unafaa ufanye biashara ya nafaka:uza mchele bei za jumla maeneo ya uswahilini,tafuta watu wawili committed wenye maduka au vibanda vya mtaani msaini mkataba uwe supplier wao, laki5 unaeza kuanza na gunia 2(kg200)ukipata Faida ya 150-200 kwenye kg1 si chini ya 30000kwa wiki×4=120,000.
Ukitoa gharama za bodaboda wa kupeleka mzigo madukani na dharura hata ukipata elfu80 kwa mwezi, hii ni sawa na mifuko mitano ya cement!!

Au vinginevyo tafta eneo dogo la wazi isiwe mbali sana na makazi yako..(unaeza ukakodi) lima mbogamboga za fasta (mchicha,chinese,pilipili)anzisha kilimo cha umwagiliaji then mweke kijana (cheap labor)asimamie uzalishaji alafu mwingine asimamie mauzo nyakati za asubuhi na jion(hakikisha ni mtu wa karibu na mwaminifu)usipotoka Nenda katubu!
Ushauri nzuri sana!
 
Back
Top Bottom