Napenda kuishi karibu na uzao wangu hasa katika uzee wangu

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Kutokana na changamoto ninazoziona kwa wazee au wakubwa zangu walionitangulia, hasa wenye umri mkubwa wanavyoishi, nimeazimia kutengeneza 'empire' kama mazingira yataniruhusu.

Wazee wengi wamekuwa wakiishi kinyonge, kutokana na watoto wao kuwa mbali nao; unakuta mzee alipambana kuwakuza watoto wake ili kwenye uzee wake aishi kwa faraja au kuwa karibu nao; mwisho wa siku watoto wanafanikiwa katika maisha na kuishi mbali na wazazi wao.

Mfano mzee, ana watoto 5; chukulia watoto wote wako kwenye miji yao, labda wengine nchi za mbali n.k na mzee ameachwa nyumbani na mkewe pamoja na wasaidizi wa kazi, ule ukaribu wa watoto wake unakuwa haupo; na wazee wanaitaji faraja pamoja na kuwa karibu na uzao wake.

Maisha yanakuwa hayana maana tena kama katika uzee wangu nitaishi na wasaidizi wa kazi, badala ya kuishi na uzao wangu. Kwa sababu mimi / wewe ni wazee watarajiwa, kwangu binafsi napenda katika uzee wangu niwe karibu na uzao wangu, ili zile 'stress' za uzeeni zipungue.

Kulifanikisha hilo wakuu, nitatumia formula wanayotumia wahindi; ukioa au ukiolewa na mtoto wangu utaishi kwenye himaya 'empire' yangu. Hata kama mtakuwa na uwezo wa kujenga nyumba yenu, hizo fedha mtatumia kukuza au kuanzisha miradi mipya ya kibiashara. Ila lazima muishi katika himaya yangu, wajukuu wazaliwe na wawe karibu na bibi/babu yao. Mambo ya kuishi na 'stress' uzeeni kama sikuzaa watoto, mimi kwangu sizitaki.

Nitapambana na vijana katika kuwawekea misingi ya kujiajiri na sio kuajiriwa, kwa sababu kuajiriwa pia ni sababu ya kufanya uzao kuwa mbali na wewe. Maisha ni haya haya hapa duniani; ukiamua uteseke mpaka uzeeni ni wewe tu, ukiamua watoto wakutelekeze ni wewe tu n.k

Wazo langu mnalionaje wakuu?
 
Wazo sahihi sana kwani ukiwa bachela aka msela mpaka uzeeni utafia chumbani na hakuna atakayejua
 
1: Tafuta hela na uweke akiba ya kutosha

2:uwe na watoto wengi na hakikisha wamepata elimu na malezi ya kiroho

3: hakikisha hao watoto unashirikiana nao kwenye miradi yako tangu wakiwa wadogo.

Zaidi ya hapo kama unataka kuwa na watoto uzeeni wasio na ajira wala elimu lakini una mali, watakusaidia safari ya kaburini iwe ya haraka zaidi
 
Kusanya wajukuu ukae nao wewe wanao watakutembelea tu.
Nb. Uwe na uwezo wakuwahudumia wajukuu shule na matibabu na matumizi muhimu usiwafanye sababu ya kutumiwa fedha na wanao na uishi mjini ili waende shule nzuri otherwise watapelekwa boarding schools
 
Wewe unataka hivyo, ila yawezekana wanao wasitake hivyo na wakataka maisha ya tofauti na hayo.
 
umewaza mbali mkuu,ngoja na Mimi nifuatilie comment za wachangiaji hope nitatoka na kitu hapa.
 
Back
Top Bottom