Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kutokana na changamoto ninazoziona kwa wazee au wakubwa zangu walionitangulia, hasa wenye umri mkubwa wanavyoishi, nimeazimia kutengeneza 'empire' kama mazingira yataniruhusu.
Wazee wengi wamekuwa wakiishi kinyonge, kutokana na watoto wao kuwa mbali nao; unakuta mzee alipambana kuwakuza watoto wake ili kwenye uzee wake aishi kwa faraja au kuwa karibu nao; mwisho wa siku watoto wanafanikiwa katika maisha na kuishi mbali na wazazi wao.
Mfano mzee, ana watoto 5; chukulia watoto wote wako kwenye miji yao, labda wengine nchi za mbali n.k na mzee ameachwa nyumbani na mkewe pamoja na wasaidizi wa kazi, ule ukaribu wa watoto wake unakuwa haupo; na wazee wanaitaji faraja pamoja na kuwa karibu na uzao wake.
Maisha yanakuwa hayana maana tena kama katika uzee wangu nitaishi na wasaidizi wa kazi, badala ya kuishi na uzao wangu. Kwa sababu mimi / wewe ni wazee watarajiwa, kwangu binafsi napenda katika uzee wangu niwe karibu na uzao wangu, ili zile 'stress' za uzeeni zipungue.
Kulifanikisha hilo wakuu, nitatumia formula wanayotumia wahindi; ukioa au ukiolewa na mtoto wangu utaishi kwenye himaya 'empire' yangu. Hata kama mtakuwa na uwezo wa kujenga nyumba yenu, hizo fedha mtatumia kukuza au kuanzisha miradi mipya ya kibiashara. Ila lazima muishi katika himaya yangu, wajukuu wazaliwe na wawe karibu na bibi/babu yao. Mambo ya kuishi na 'stress' uzeeni kama sikuzaa watoto, mimi kwangu sizitaki.
Nitapambana na vijana katika kuwawekea misingi ya kujiajiri na sio kuajiriwa, kwa sababu kuajiriwa pia ni sababu ya kufanya uzao kuwa mbali na wewe. Maisha ni haya haya hapa duniani; ukiamua uteseke mpaka uzeeni ni wewe tu, ukiamua watoto wakutelekeze ni wewe tu n.k
Wazo langu mnalionaje wakuu?