Napendekeza aina hii ya tozo kwamba kila mwenye gari alipie tsh 1,000/= kila mwezi

Napendekeza aina hii ya tozo kwamba kila mwenye gari alipie tsh 1,000/= kila mwezi

Moja kwa moja kwenye Mada.

Napendekeza aina hii ya tozo kwamba kila mwenye gari alipie tsh 1,000/= kila mwezi kwa mwaka tsh 12,000/= kwa kila gari moja,

INALIPWAJE?

Ilipwe katika vituo vya mafuta, pale gari linapoenda kujaza mafuta, ikatwe hapo hapo kama vile jinsi tunavyolipia luku,

Ukitoa tsh elfu 10, ili ujaze mafuta ya kiasi hicho utapata mafuta ya tsh elfu tisa, reference ni plate namba ya gari, elfu moja itaenda kuchangia maendeleo.

Nawasilisha
Umasikinii tuu ndio unakusumbua

Mkiaminishwa wenye magari ndio wenye hela.

Kama wenzako walivyoanzisha tozo za simu wakiamini watuma pesa ni wenye pesa .

Fikra za kimaskini hizo ,na hili unalisemea kwa sababu huna gari siku ukipata gari utodhubutu kilitaja na sizani kama utakuja kuwa na gari kwa akili hizi mfuu
 
Ona mawazo mengine ya kichawi haya!

Tuna kila aina ya raslimali kama Taifa! Badala ya kuzitumia vizuri ili kuwanufaisha wananchi wote, viongozi wako wanazigawa tu bure au kwa kupewa 10% kwa Wazungu, Waarab, na wachina!

Halafu mwisho wa siku mnakuja kuwaumiza wananchi wa kawaida kupitia hizi tozo zenu za kipuuzi! Hovyo kabisa.
Atakuwa UVCCM aliyekatwa kwenye uchaguzi wao huko,sasa analeta uchawi . wake kwa watu wenye magari

Na huko ndiko wanapojifunza huu uchawi,anashindwa kumwambia huyo Bibi apunguze matumizi kwenye Safari na misafara yake analeta wivu hapa
 
Huyo mshika pump anafaidika na nini au kuna mfumo gani unaomlamisha awe na huo uzalendo wa kuingiza plate number kwenye sytem
 
Back
Top Bottom