Napendekeza bidhaa zipigwe kodi mara moja tu, njia ni hii

Nadhani kodi huwa inakatwa kwenye mapato yaaan kile kinachobaki au faida na sio manunuzi.
System ya TRA iko sawa ila wafanyabiashara hawakubali kuona faida inakatwa kodi na hvyo kuuza bidhaa kwa bei ya juu. Muathirika wa kodi ni mfanyakazi aliyeajiriwa maana no wayout atakatwa kodi (PAYE) na bado katika kila bidhaa anayonunua atajikuta anamsaidia mfanyabiashara kulipa kodi(sababu atanunua kwa bei ya juu).
Mfanyakazi aliyeajiriwa analipa kodi mara moja tuu na katika manunuzi huwa halipi bali muuzaji ndiye anayetakiwa kulipa katika faida ndio maana unapodai risiti wanakasirika.
 

Vichwa vilivyojaa A za makaratasi
 
Sina hakika kama umenielewa nilichosema juu ya mfumo kuleta mlolongo mrefu bila sababu.
 
Kiukweli haya mawazo nayaunga mkono kwa 100%. Ningekuwa na Uwezo ningelipia kipindi japo kimoja kwenye TV ukatoa somo. Naamini kupitia TV huenda waliopewa mamlaka na rais wangu wakapata taarifa na wakaelewa ili waamke waache kudhoofisha sekta ya biashara.

Ona kama maajabu ya EFD, unaambiea nunua mwenyewe eti baadae kwenye mahesabu utarejeshewa. Maelezo ya kamishina akiwa bunda wakati anapita kwenye maduka kukagua EFD. Sasa kama baadae utarejeshewa kwanini mwananchi apewe presha ya kusaka laki7 kwa nguvu, kwanini wasizitoe bureeee.

Kiukweli kabisa mfumo wa kodi kila siku ninasema ni wa kikoloni. Ni utaratibu uliowekwa na mkoloni mzungu kumnyonya mwananchi ili asinyanyuke kiuchumi.

Nakupongeza kwa dhati ya moyo wangu, nakuomba huu Uzi uwe unaukumbusha kumbusha kila wiki. Huu ni mchango Mkubwa wa mawazo.
 
Duuh, highly appreciated!
 
Nadhani hii itapunguza hata beauracracy kwenye kulipa kodi
 
Changamoto za multiple taxation
1. Lisiti moja ya EFD kutumika zaidi ya maramoja kwa bidhaa zenye bei ya kufanana
2. Unanua bidhaa za 1,000,000/= mfanya biashara ananegoshieti na mnunuzi anaandikiwa Lisiti ya 200,000/= .....anamtoa mnunuzi kiasi kidogo chini ya kodi aliyopaswa kulipa.
3. Mnunuzi na muuzaji kujilipua kuuziana biashara nje ya mfumo wa EFD
4. Kuwindana mtaani bila sababu eti una EFD au hauna
 
Ni kweli, ni shida sana
 
Update: 04/04/2021
Mwigulu Nchema amesema wanaangalia namna tofauti ya kukusanya kodi
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…