Napendekeza bidhaa zipigwe kodi mara moja tu, njia ni hii

Napendekeza bidhaa zipigwe kodi mara moja tu, njia ni hii

Mim nipo nje ya mada.chuma ulete mharibu hela.ushauri
Bot.toen elim kwa umma. Wanaharibu hela
20221226_170137.jpg
 
Kwani kodi ikilipwa yote mara moja kwenye source, yaani yote kabisa, halafu wanachi wakaachwa waishi kwa amani kuna tatizo gani?
 
Itabidi kubadilisha mifumo ya EFD kulingana na biashara chain inapoanzia.

Kama kiwanda kinatoa risit basi huko mpaka kwa muuzaji mashine yake inatakiwa kuwa tofauti kabisa na asilimia ya mwisho ya muuzaji hiwe 2% kwenye risiti
 
Tanzania tuna mfumo wa kodi ambao naweza kuuita ni 'Tax chain system'. Yaani ni kwamba bidhaa moja inaweza ikapigwa kodi hata mara kumi halafu wale watu walioilipia kodi mara ya 2 hadi ya 10 wanatakiwa wapeleke mahesabu TRA ili warudishiwe kodi yao;kivipi?

Mfano bidhaa imezalishwa kiwandani, mnunuzi wa kwanza atakayenunua atalipa 18% Vat, na hii tu ndio halali ya TRA kwa bidhaa hiyo, lakini kama huyu mnunuzi wa kwanza ataenda kuiuza itabidi atoe risiti ya EFD na atamlipisha tena mteja 18% Vat ambayo TRA itamdai, huyu nae akienda kuiuza itabidi atoe risiti ya EFD ambapo atamchaji tena mteja 18% VAT ambayo nayo itatakiwa kupelekwa TRA, and so on hata mara 10.

Ili kuepuka kulipa VAT mara mbili kila mfanyabiashara atapeleka mahesabu na risiti za VAT (kwa waliounganishwa na VAT) ili kujua kiwango cha ziada cha kile ambacho ameshalipa, na hicho tu ndicho atapaswa kulipa; hii process inaleta mlolongo mgumu na very complicated, yaani ni mfumo mgumu sana bila sababu, nadhani wote mnofuatilia haya masuala mtajua.

Lengo la TRA kung'ang'ania huu mfumo ni ili kupata 18% ya faida ya kila hatua ya uuzaji wa bidhaa, hata ikiuzwa mara 10 TRA hawajali, wanataka 18% ya ile faida (gross profit) ya kila mfanyabiashara katika kila chain link ya uuzaji wa bidhaa husika, hadi kwa final consumer, yule wa mwisho kabisa. (Wanakaba hadi penalti).

Hii inaweza kuonekana ni nzuri ukiitazama kwa juu juu, lakini in reality hii ni sawa na kutumia risasi kuwinda smaki baharini, unatumia 10shs. kukusanya shs.8, yeees, ukweli ndio huu. Badala ya kusababisha such an expensive practical complexity ni kwanini TRA isiwekeze instead kuhakikisha kodi yote ya kila bidhaa inalipwa palepale kiwandani bidhaa inapozalishwa au bandarini mzigo unapoingizwa, hata kama kodi ikiongezwa sio mbaya lakini ilipwe yote infull palepale kiwandani / bandarini.

Hebu fikiria tu harassment wanayopata wateja wanaposafirisha mizigo barabarani, watu husimamishwa hovyo hovyo na mapolisi 'Tigo' wale wenye silaha za kivita as if wanasimamisha jambazi, kumbe umebeba T.V tu ndio imekuwa nongwa, kwani hii T.V si imepitia bandarini??! Si mchukue kodi yenu yote huko huko muache wananchi waishi kwa amani?

Mateso kama haya walikuwa wanayapata wamiliki wa magari ambapo kila mwaka walipanga foleni TRA na office za MXMALIPO kulipia road license, tena barabarani TRA walipoteza nguvu kazi kubwa ya wasomi wenye madegree kusimamabarabarani eti kukagua sticker za road license, as if hizo gari hazitumii mafuta ambayo tayari yana kodi lukuki, binafsi nilianzisha uzi wa kupendekeza kodi hiyo nayo iunganishwe tu humo humo kwenye mafuta(Hivi ni kwanini road license isilipiwe kwenye mafuta?) watu waligoma goma ili mwishowe logic and common sense emerged victourious, serikali ikahamishia kodi hiyo kwenye mafuta na sasa hii kero imeisha

Muda mwingine umasikini tunajitafutia wenyewe kwa kukariri vitu vilivyopitwa na wakati, technolojia imekuwa, ni rahisi sana kukata kodi yote in full kwenye viwanda / bandarini, tubadilike bwana; nakaribisha maoni.

=================================
Update: 04/04/2021
Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, amesema wanaangalia namna ya kutumia mfumo mpya wa ukusanyaji kodi

==========================
Update: 23/09/2022

===========================

value added tax kwa kimombo aina hii ya tax inaingia katika kundi la indirect tax nikisema indirect tax namaanisha mlipaji haumii kulipa kodi kwani kodi inakuwa tayari ndani ya bei ya bidhaa,na sifa moja wapo ya V.A.T inaelipa ni mtumiaji wa mwisho mfano ukinunua vocha ya Tsh 500 ukajiunga kifurushi ukisoma vizuri kuna V.A.T ndani yake. Baadhi ya sifa za mfanyabiashara mpaka anakuwa V.A.T register ni.(ntasahihishwa kama sifa zimebadilika)
1. awe na turnover ya mil 100 kwa mwaka
2. mtaji wake uwe kuanzia mil 14.
3. awe anauza bidhaa zilizopo katika kundi la V.A.T.
ukija katika mfumo wa usambazaji wa bidhaa (chain of distribution) kuna stage nne ambazo ni.
1.producer atamuuzia wholesaler. (producer ni mzalishaji)
2.wholesaler atamuuzia retailer. (wholesaler ni muuzaji wa vitu kwa ujumla)
3.retailer atamuuzia final consumer.(retailer ni wauzaji wa rejareja)
4.final consumer.(ni mtumiaji).
ukiona hiyo distribution chain na ukiangalia sifa za kuwa mfanyabiashara ambae unalipia V.A.T mara nyingi inakomea katika stage two ambapo unawapata producer na wholesaler, nafikili nimeeleweka.
kama nilivyoesema kule juu V.A.T anaelipa ni mtumiaji wa mwisho, ipo hivi.
Producer akiuza bidhaa akakata V.A.T (hii itakuwa ni Input tax) na yeye akanunua bidhaa akakatwa V.A.T (hii itakuwa ni output tax). sasa V.A.T itakayolipwa na huyu mfanyabiashara itakuwa input tax-output tax moja kwa moja bidhaa aliyotumia katika uzarishaji itajifuta mfano alinunua vifaa kwa ajili ya kutengeneza simu (output tax) na hiyo simu akaiuza (input tax) umeona sasa ila angenunua kwa matumizi binafsi asingekuwa na input tax ya kufutia hiyo kodi.
Nawasilisha kwa kuongeza maarifa zaidi
 
Ahsante kwa kukazia uzi
 
Mkeka huo ni sawa so as long as huku mtaani hamta bughudhi watu kudai receipt, bidhaa ziuzwe free
 
Back
Top Bottom