Napendekeza bidhaa zipigwe kodi mara moja tu, njia ni hii

Napendekeza bidhaa zipigwe kodi mara moja tu, njia ni hii

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
==========================
UPDATE: 27/06/2024

View: https://www.instagram.com/reel/C8tOKmmqjWh/?igsh=MWJhZWFjNTNhajNtcg
=======================

52F3690E-9F33-4AAF-966A-B1919BD4A85D.jpeg

TRA Tanzania
Tanzania tuna mfumo wa kodi ambao naweza kuuita ni 'Tax chain system'. Yaani ni kwamba bidhaa moja inaweza ikapigwa kodi hata mara kumi halafu wale watu walioilipia kodi mara ya 2 hadi ya 10 wanatakiwa wapeleke mahesabu TRA ili warudishiwe kodi yao;kivipi?

Mfano bidhaa imezalishwa kiwandani, mnunuzi wa kwanza atakayenunua atalipa 18% Vat, na hii tu ndio halali ya TRA kwa bidhaa hiyo, lakini kama huyu mnunuzi wa kwanza ataenda kuiuza itabidi atoe risiti ya EFD na atamlipisha tena mteja 18% Vat ambayo TRA itamdai, huyu nae akienda kuiuza itabidi atoe risiti ya EFD ambapo atamchaji tena mteja 18% VAT ambayo nayo itatakiwa kupelekwa TRA, and so on hata mara 10.

Ili kuepuka kulipa VAT mara mbili kila mfanyabiashara atapeleka mahesabu na risiti za VAT (kwa waliounganishwa na VAT) ili kujua kiwango cha ziada cha kile ambacho ameshalipa, na hicho tu ndicho atapaswa kulipa; hii process inaleta mlolongo mgumu na very complicated, yaani ni mfumo mgumu sana bila sababu, nadhani wote mnofuatilia haya masuala mtajua.

Lengo la TRA kung'ang'ania huu mfumo ni ili kupata 18% ya faida ya kila hatua ya uuzaji wa bidhaa, hata ikiuzwa mara 10 TRA hawajali, wanataka 18% ya ile faida (gross profit) ya kila mfanyabiashara katika kila chain link ya uuzaji wa bidhaa husika, hadi kwa final consumer, yule wa mwisho kabisa. (Wanakaba hadi penalti).

Hii inaweza kuonekana ni nzuri ukiitazama kwa juu juu, lakini in reality hii ni sawa na kutumia risasi kuwinda smaki baharini, unatumia 10shs. kukusanya shs.8, yeees, ukweli ndio huu. Badala ya kusababisha such an expensive practical complexity ni kwanini TRA isiwekeze instead kuhakikisha kodi yote ya kila bidhaa inalipwa palepale kiwandani bidhaa inapozalishwa au bandarini mzigo unapoingizwa, hata kama kodi ikiongezwa sio mbaya lakini ilipwe yote infull palepale kiwandani / bandarini.

Hebu fikiria tu harassment wanayopata wateja wanaposafirisha mizigo barabarani, watu husimamishwa hovyo hovyo na mapolisi 'Tigo' wale wenye silaha za kivita as if wanasimamisha jambazi, kumbe umebeba T.V tu ndio imekuwa nongwa, kwani hii T.V si imepitia bandarini??! Si mchukue kodi yenu yote huko huko muache wananchi waishi kwa amani?

Mateso kama haya walikuwa wanayapata wamiliki wa magari ambapo kila mwaka walipanga foleni TRA na office za MXMALIPO kulipia road license, tena barabarani TRA walipoteza nguvu kazi kubwa ya wasomi wenye madegree kusimamabarabarani eti kukagua sticker za road license, as if hizo gari hazitumii mafuta ambayo tayari yana kodi lukuki, binafsi nilianzisha uzi wa kupendekeza kodi hiyo nayo iunganishwe tu humo humo kwenye mafuta(Hivi ni kwanini road license isilipiwe kwenye mafuta?) watu waligoma goma ili mwishowe logic and common sense emerged victourious, serikali ikahamishia kodi hiyo kwenye mafuta na sasa hii kero imeisha

Muda mwingine umasikini tunajitafutia wenyewe kwa kukariri vitu vilivyopitwa na wakati, technolojia imekuwa, ni rahisi sana kukata kodi yote in full kwenye viwanda / bandarini, tubadilike bwana; nakaribisha maoni.

=================================
Update: 04/04/2021
Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, amesema wanaangalia namna ya kutumia mfumo mpya wa ukusanyaji kodi

==========================
Update: 23/09/2022

===========================

===========================
Update: 05/01/2023

Mlioalikwa msituangushe

==========================
Update: 14/05/2023

DEAE9FD2-4B4E-47FA-A5C9-5BDEDAA18F13.jpeg

==========================
Update: 28/07/2023
 
Ninaunga mkono hoja. Kingine, ule ushauri wako kuhusu pendekezo la kuanzisha TRA EFDs app nalo lilikuwa bomba sana. Mwisho-nakushauri thread zako za kiushauri uwe unaziweka chini ya thread mpya unayoifungua ili ziwe zinaonekana kwa urahisi.
 
Tanzania kuokoa shs. trillion moja kwa kuanzisha TRA EFD app

==========================
1.) Hivi ni kwanini road license isilipiwe kwenye mafuta?

2.) Je, kutumia sh.50,000/= kulipa TRA kodi Nyumba ya sh.10,000/= ni akili au matope?

3.) Hivi ni kwanini nguzo za zege hazitumiki kama nguzo za umeme?

4.) Napendekeza taa za mwanga barabarani na nyaya za simu zifungwe kwenye nguzo za umeme

5.) Tanzania kuokoa shs. trillion moja kwa kuanzisha TRA EFD app

6.) Fahamu hatari kubwa zinazozikabili nchi zinazotumia mifuko ya plastiki

7.) Napendekeza stika za Wiki ya Nenda kwa Usalama zilipiwe kwenye bima, ukikata bima ukague na gari kabisa na vyote ulipie kwa mara moja

===========================

1.) Napendekeza bidhaa zipigwe kodi mara moja tu, njia ni hii

2.) Napendekeza namba moja ya wakala kwa mitandao yote ya simu

3.) Napendekeza king’amuzi kimoja kwa kampuni zote za ving’amuzi

4.) Napendekeza meter za maji zifungwe mifumo ya ‘LUKU’

5.) Naomba kuelimishwa: Matrillioni ya pesa yanayokusanywa na makampuni ya Bima kupitia mawakala wao mitaani, ni za serikali au ni za nani?

6.) Napendekeza mfumo wa ‘Randomizer’ kwenye usajili wa ‘plate number’ za magari nchini

7.) Napendekeza wavuta sigara wapewe leseni kama za magari, na warenew kila mwaka

8.) Nyumba moja kuwa na meter kumi za LUKU haina maana, Napendekeza LUKU moja iwe na line nyingi kama simu

9.) Napendekeza serikali ifunge projector madarasa yote shule za msingi badala ya kuajiri walimu, hii itasaidia kuokoa takriban trillion 3 Kwa mwaka

10.) Napendekeza kura za uchaguzi mkuu zipigwe kwa kutumia Tigo pesa
 
Mkuu, naunga mkono hoja, siku moja nilienda kununua godolo lakini bei niliyoambiwa ilikuwa kubwa sana kuliko kawaida ikanibidi nimhoji muuzaji kama atanipa na risiti ya EFD jibu alilonipa nikuwa eti magodoro hulipiwa kodi ya 18% pale pale kiwandani lakini mimi nikawa najiuliza mbona tulipata taarifa kupitia jf kuwa kule Moshi mwezi Dec 2017 TRA waliweka kambi kwenye ma baar kukusanya kodi ya vinywaji?

Ukweli hakuna bidhaa inayokatiwa kodi mara moja katika nchi hii, kodi mara moja kiwandani au bandarini au mipakani inatosha vinginevyo ni kero kwa wananchi.
 
Mkuu, naunga mkono hoja, siku moja nilienda kununua godolo lakini bei niliyoambiwa ilikuwa kubwa sana kuliko kawaida ikanibidi nimhoji muuzaji kama atanipa na risiti za EFD jibu alilonipa nikuwa eti magodoro hulipiwa kodi ya 18% pale pale kiwandani lakini mimi nikawa najiuliza mbona tulipata taarifa kupitia jf kuwa kule Moshi mwezi Dec 2017 TRA waliweka kambi kwenye ma baar kukusanya kodi za vinywaji?

Ukweli hakuna bidhaa inayokatiwa kodi mara moja katika nchi hii, kodi mara moja kiwandani au bandarini au mipakani inatosha vinginevyo ni kero kwa wananchi.
Nimefurahi kuona kwamba unamtazamo sawa na wangu, ila je, ni kweli kwamba magodoro hulipiwa 18% Vat pale pale kiwandani, wanashindwa nini kwa bidhaa zingine zote?
 
Zambia wamefanikiwa kwa mfumo huo unaozungumzia kodi ipo mpakani na sio kubwa ukilipa basi kuna bidhaa nyingi na Mpya kwa hizi za matumizi ya kawaida hata SA ukilipa kodi mpakani vizuri hawana shida na wewe tena Bongo ni kero bidhaa hakuna ni used nyingi lakini mtiririko wa kodi hadi hatari kumbe inatakiwa wawe na wigo Mkubwa wa kukusanya kodi kiasi kidogo kwa wafanyabiashara wengi wanapata mapato mengi zaidi wao wanataka wafanyabishara wachache walipe kodi kubwa kitu ambacho ni kigumu kwa wafanyabiashara.
 
Zambia wamefanikiwa kwa mfumo huo unaozungumzia kodi ipo mpakani na sio kubwa ukilipa basi kuna bidhaa nyingi na Mpya kwa hizi za matumizi ya kawaida hata SA ukilipa kodi mpakani vizuri hawana shida na wewe tena Bongo ni kero bidhaa hakuna ni used nyingi lakini mtiririko wa kodi hadi hatari kumbe inatakiwa wawe na wigo Mkubwa wa kukusanya kodi kiasi kidogo kwa wafanyabiashara wengi wanapata mapato mengi zaidi wao wanataka wafanyabishara wachache walipe kodi kubwa kitu ambacho ni kigumu kwa wafanyabiashara...
Wacha bwana, kumbe Zambia wanatumia huu mfumo tayari, nilijua ni mimi tu ndie nina mawazo revolutionary kama haya; bahati mbaya sana hii wizara yetu ya mipango vimejaa vichwa vilivyolala usingizi wa pono, inasikitisha sana. Ila si mbaya kama wakaunda kamati ya kwenda Zambia kujifunza jinsi wanavyotekeleza mfumo huu, faida na changamoto zake, kisha waje washauri how best tunaweza kuitumia huku kwetu. Huu urasimu wa multiple taxation ni kikwazo kikubwa sana kwa ustawi wa biashara na uchumi kwa ujumla.

Na kwa mfumo wa kukusanya Vat bandarini / mpakani / viwandani ni kwamba hadi machinga anaeuza soksi barabarani atalipa vat, ambapo kwa sasa machinga wanauza vitu vingi mkononi Vat free na kuisababishia serikali upotevu mkubwa wa mapato.
 
Tena ikiwezekana hilo Wazo lako ungeenda lisajili hawakawi Jamaa Wale wakaja kulifanyia kazi,Yaani wakalipata kiubwetee tu mkuu

Ova
Hahah..., mimi hata sina shida nalo, wakitekeleza tu kwangu ni malipo tosha
 
Mkuu, naunga mkono hoja, siku moja nilienda kununua godolo lakini bei niliyoambiwa ilikuwa kubwa sana kuliko kawaida ikanibidi nimhoji muuzaji kama atanipa na risiti za EFD jibu alilonipa nikuwa eti magodoro hulipiwa kodi ya 18% pale pale kiwandani lakini mimi nikawa najiuliza mbona tulipata taarifa kupitia jf kuwa kule Moshi mwezi Dec 2017 TRA waliweka kambi kwenye ma baar kukusanya kodi za vinywaji?

Ukweli hakuna bidhaa inayokatiwa kodi mara moja katika nchi hii, kodi mara moja kiwandani au bandarini au mipakani inatosha vinginevyo ni kero kwa wananchi.
Kuna muhindi aliniambia mama nikipe godoro Bei nafuu unaweza kuwa msiri ?[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Bandiko ni zuri, na Umefunguka kwa Mantiki.
But labda nikurekebishe tu kitu kimoja, sio mizigo yote ya TRA inapititia bandarini lakini pia ipo inayopitia bandarini lakini kwa sababu za umakini hazipigwi Kodi. Sasa tuache hizo zinazopitia Bandarini, Tuje kwenye hizi ambazo watu wasio wazalendo wanapitisha mizigo hiyo bila kufuata utaratibu(kwa kukwepa kodi). Sasa ni vizuri unapotoa hoja hiyo utoe pia na wazo ni namna gani TRA itapata kodi kwenye mizigo ambayo ilipitishwa kinyume na Utaratibu? Hapo utakuwa umewasaidia.

So far, Bandiko ni zuri, lina logoc ndani yake ni hayo tu.
 
Ungekuwa unapeleka na shilawadu wangeliona haraka, walisema huwa wanakesha wakiangalia hicho kipindi. Ni wazo kuufikisha ujumbe mapema.
 
Bandiko ni zuri, na Umefunguka kwa Mantiki.
But labda nikurekebishe tu kitu kimoja, sio mizigo yote ya TRA inapititia bandarini lakini pia ipo inayopitia bandarini lakini kwa sababu za umakini hazipigwi Kodi. Sasa tuache hizo zinazopitia Bandarini, Tuje kwenye hizi ambazo watu wasio wazalendo wanapitisha mizigo hiyo bila kufuata utaratibu(kwa kukwepa kodi). Sasa ni vizuri unapotoa hoja hiyo utoe pia na wazo ni namna gani TRA itapata kodi kwenye mizigo ambayo ilipitishwa kinyume na Utaratibu? Hapo utakuwa umewasaidia.

So far, Bandiko ni zuri, lina logoc ndani yake ni hayo tu.
Ni kweli, na ndio maana nikasema TRA iwekeze badala yake kwenye kuhakikisha mizigo yote inalipiwa 18% vat kabla ya kuingia nchini, huu ni uwekezaji mkubwa sana unaobidi ufanyike mipakani, nadhani watu wa wizara ya mambo ya ndani hili ni eneo lao murua la kuonyesha ni namna gani wanaweza kudhibiti magendo.
 
Nimefurahi kuona kwamba unamtazamo sawa na wangu, ila je, ni kweli kwamba magodoro hulipiwa 18% Vat pale pale kiwandani, wanashindwa nini kwa bidhaa zingine zote?
Bidhaa nyingi hulipiwa kodi viwandani na ndio maana huwa tunatangaziwa na serikali kila wanapozipandishia kodi hasa hasa katika bunge la bajeti, hivyo hutozwa kodi viwandani na huku tena mitaani rungu la kodi linaendelea kama kawainda mara mbili au hata zaidi.
Mkuu, naunga mkono hoja, siku moja nilienda kununua godolo lakini bei niliyoambiwa ilikuwa kubwa sana kuliko kawaida ikanibidi nimhoji muuzaji kama atanipa na risiti ya EFD jibu alilonipa nikuwa eti magodoro hulipiwa kodi ya 18% pale pale kiwandani lakini mimi nikawa najiuliza mbona tulipata taarifa kupitia jf kuwa kule Moshi mwezi Dec 2017 TRA waliweka kambi kwenye ma baar kukusanya kodi ya vinywaji?

Ukweli hakuna bidhaa inayokatiwa kodi mara moja katika nchi hii, kodi mara moja kiwandani au bandarini au mipakani inatosha vinginevyo ni kero kwa wananchi.
 
Bidhaa nyingi hulipiwa kodi viwandani na ndio maana huwa tunatangaziwa na serikali kila wanapozipandishia kodi hasa hasa katika bunge la bajeti, hivyo hutozwa kodi viwandani na huku tena mitaani rungu la kodi linaendelea kama kawainda mara mbili au hata zaidi.
Sasa kwa mfano bia hua zinatangazwa bungeni kwamba zimepandishiwa kodi; je, ni kwanini sasa ma bar mengi yanalazimishwa yatoe risiti za EFD, kama
ni kwa ajili ya income tax na service levy ziunganishwe zote zilipwe hapo hapo kiwandani mara moja na kwa mkupuo, ili ikiingia sokoni watu wawe huru kuishi kwa amani.
 
Back
Top Bottom